NDOTO ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.
NDOTO ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA. Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu, Nisiku nyingine tena tunakutana katika jukwaa ili la ujasiliamali ili tuweze kupeana elimu tena. Leo nitapenda tuweze kutazama mbinu na taratibu za kuweza kufikia mafanikio yetu. Siku zote katika maisha lazima uwe na ndoto kama wewe ni mwana maendeleo halisi, Natumai ndugu yangu una ndoto ulizonazo,na unatamani siku moja uzifanikishe. sasa nataka nikwambie kitu ambacho kitakusaidia ili uweze kuzifanikisha ndoto zako. Waswahili husema mali bila kalamu huisha bila habari,usemi huu nimekuwa nikiutumia katika maisha yangu ya kila siku. Mimi nautumiaje? Jinsi ninavyo utumia usemi huu ni tofauti na jinsi maana ya usemi wenyewe. mimi huutumia usemi huu kuandika kile ambacho ninaota kukifikia. ndugu yangu ukitaka kufikia ndoto zako nilazima ufuate aya: Chukua kalamu na Karatasi/Diary yako kisha anza kuandika,andika aya, Andika tarehe ya leo, Andika malendo yako yote ...