HACHA KUIHUKUMU NAFSI YAKO. Kila mtu analo jambo la kufanya na tunayo malengo ya kutimiza, ila tatizo ni kuwa mioyo yetu imejaa hukumu zisizo za msingi ndio maana tunashindwa kutimiza malengo yetu. Tunatanguliza kushindwa, aliekwambia kuwa huwezi kumiliki biashara yako nani, nani alikwambia kuwa huwezi kumiliki kampuni? Nani alikwambia huwezi kuwa kiongozi bora, unafikiri mafanikio watu wanazaliwa nayo? Yote yanatafutwa hapa hapa duniani. Hacha kujihukumu bure kuwa huwezi jambo fulani,kwani wewe ni nani usiweze, wanaoweza wana nini cha ajabu? Biashara zetu zinashindwa kustawi kutokana na minyororo iliopo ndani yetu maana tumeifunga kisawa sawa. Mtu wazo la kufanya biashara au jambo fulani unalo ila hutaki kufanya unategemea nani akufanyie sasa, au unataka jirani yako aje afanye badala yako? Hachana na mawazo hayo ya kuifunga nafsi yako, punguza hiyo hukumu na upe mwili wako nafasi ya kufanikiwa, ni kuamini kwamba unaweza, kuondoa mambo yasiyo ...