Posts

Showing posts with the label ujasiriamali

UMUHIMU WA BUSINESS PLAN KWA MFANYABIASHARA

Image
UMUHIMU WA BUSINESS PLAN KWA MFANYABIASHARA. Business Plan (mpango biashara) ni nini? Business Plan ni taarifa iliyoandikwa ambayo huonyesha lengo la biashara husika kwa kuonyesha hatua muhimu za kupitia ili kufikia lengo. Hapa unapata picha kuwa, ni wapi ulipo, unaenda wapi na jinsi gani utafika ulipo kusudia kufika. *Umuhimu wa business plan kwa mfanya biashara.* Tuangalie umuhimu wa mpango biashara kwa mfanya biashara. Mpango biashara ina umuhimu mkubwa sana kwa mfanya biashara /mjasiriamali yeyote ambapo faida zake ni kama ambavyo tutazitazama hapa chini. i) Humsaidia mfanya biashara kuepukana na uwezekano wa kuingia katika biashara yenye uwezekano wa kufa. Kama tulivyo ona katika makala zetu zilizo tangulia, business plan inakuwa kama ramani ya kukuonyesha njia sahihi ya kupitia. Hivyo ukiitumia kwa usahihi utakuwa na biashara au mradi endelevu. ii) Humsukuma mfanyabiashara kuongeza umakini katika usimamizi wa biashara yake. Muda, juhudi, utafiti na nidhamu hutumika ha...

UMUHIMU WA BUSINESS PLAN

Image
*UMUHIMU WA BUSINESS PLAN.* Business Plan (mpango biashara) ni nini?  Business Plan ni taarifa iliyo andikwa ambayo huonyesha lengo la biashara husika kwa kuonyesha hatua muhimu za kupitia ili kufikia lengo. Hapa unapata picha kuwa, ni wapi ulipo, unaenda wapi na jinsi gani utafika ulipo kusudia kufika. *Umuhimu wa business plan* i)  Mpango huo unaelezea njia ambayo mfanya biashara au mjasiriamali anayopaswa kupitia kipindi chote cha uendeshaji wa biashara yake. Katika biashara lazima kuwepo na kanuni na taratibu, hivyo basi ili biashara yako ikue lazima kuwe na njia unazopaswa kupitia, na kupitia business plan kila kitu kitakuwa kimejipambanua humo. ii) Husaidia wawekezaji, watu wa mabenki na wafadhili wengine kuelewa na kumkubali mfanya biashara kwa ajili ya uwekezaji wao katika biashara yake.  Lazima utambue kuwa popote utakapo hitaji kwenda kupata msaada wa kuongeza mtaji (mkopo) kwa ajili ya kukuza biashara yako lazima uwe na mpango kazi huu ili kumuwezesha hu...

HABARI NJEMA KWAKO MWANA DAR ES SALAAM

Image
HABARI NJEMA KWAKO MWANA DAR ES SALAAM. Najua kila mtu anatamani kuniona na kujifunza mengi kutoka kwangu.  Sasa fursa ni hii.  NJOO UBUNGO PLAZA, GHOROFA YA PILI, OFFICE NAMBA 202. Nitakuwepo kukufunza juu ya uanzishaji biashara kwa mitaji midogo.  Najua kila mtu anatamani kuwa na biashara yake ila tatizo kubwa limekuwa ni mitaji. Sasa basi, njoo siku ya Ijumaa, Tarehe 24/06/2016 Kuanzia saa 12:00 Mchana mpaka saa 05:00 Jioni. Ili nikupe mbinu hizi adimu kabisa. Njoo, kiingilio ni bure na nitakufundisha bure. Unaruhusiwa pia kuja na mwenzako. By,  Frank A. Ndyanabo - FAN

TANGAZO LA AJIRA

Image
TANGAZO LA AJIRA. NYUMBANI BUSINESS PLAN ENTERPRISES Inakutangazia nafasi ya kazi katika idara ya afisa mauzo kwa watu wote waishio MWANZA. SIFA ZA MUOMBAJI. ••Awe ni muhitimu wa kidato cha nne Au sita. ••Awe na shahada,stashahada au cheti cha Masoko(marketing), Sayansi ya jamii(sociology), usimamizi wa biashara(business administration), fedha (finance), kibenki(banking) KAZI ZA AFISA MAUZO. 1.Kutafuta na kutengeneza masoko mapya ya bidhaa. 2.Kuandaa taarifa ya mauzo kila siku, kwa wiki na mwezi. 3.Kufuatilia na kukusanya mauzo ya kila siku. 4.Kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa msimamizi(supervisor) wake kila siku. MSHAHARA MNONO UTATOLEWA TUMA MAOMBI: Tuma maombi yako kwenda kwa Afisa Utumishi wa Nyumbani Business Plan. Email: nyumbanibusinessplan@gmail.com Kwa Mawasiliano zaidi. • +255 753 183 583 • +255 684 459 947 MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 30/06/2016

JE WEWE UNAWAZA KUFANIKIWA BAADA YA MUDA GANI?

Image
Najua huu umekuwa ni ugonjwa kwa tulio wengi hasa pale tunapo anzisha miradi mbalimbali. Kwa kuwaza kufanikiwa kwa kutumia muda mfupi. Jana katika semina yangu na wajasiriamali wa mwanza niliweza kulizungumzia hili swala kwa mapana zaidi, naamini wale walioshiliki kwa siku ya jana naamini walijifunza kitu. Mafanikio hayaji kirahisi bali yanakuitaji uvumilivu na jitihada zaidi na hatupaswi kukata tamaa. Jambo hilo analizungumzia tena hapa bilionea wa kiafrika bwana Dangote,mafanikio sio ndoto ya muda mfupi, ikiwa yeye imemchukua miaka 30 mpaka apo alipo,iweje wewe utake kufanikiwa kwa miezi kadhaa. Futa mawazo hayo na anza kujituma na husikate tamaa.

FUNGUA MLANGO WA MAFANIKIO YAKO.

Image
FUNGUA MLANGO WA MAFANIKIO YAKO. Siku mwanadamu atakapo kuja kugundua kuwa siri ya mafanikio yake yako mikononi mwake basi ndio utakuwa mwisho wa umaskini wake. Tutakuwa tunajiuliza maswali mengi juu ya umaskini na utajili. Niwakati gani unamwita mtu tajiri na mwingine unamwita maskini? Hii maana yake huwezi kutambua kuwa fulani ni tajili na fulani ni maskini pasipo kuwalinganisha kati yao. Ikitokea watu wote wakawa na kipato kimoja na maisha sawa apo huwezi tambua yupi maskini wala tajili. Apo ndio utagundua ili utofautishe jambo fulani eidha kwa ubora au kwa uzuri lazima uwe na chakulinganisha nacho. Sasa ndio maana kila mtu anatofautiana katika njia za utafutaji wake na hii kila mtu anamlango wake alio fungua maishani mwake ila inatofautiana kwa kiasi kikubwa mpaka kupelekea kuwa na makundi ya watu maskini na watu tajili. Nataka nikwambie kitu ndugu yangu kuwa,iwe unataka kuwa maskini au tajili funguo ziko mikononi mwako kuweza kuufungua mlango sahihi wa maisha yako.  Na uta...

NDOTO ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.

Image
NDOTO ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA. Habari  yako ndugu msomaji wa makala zangu, Nisiku nyingine tena tunakutana katika jukwaa ili la ujasiliamali ili tuweze kupeana elimu tena. Leo nitapenda tuweze kutazama mbinu na taratibu za kuweza kufikia mafanikio yetu. Siku zote katika maisha lazima uwe na ndoto kama wewe ni mwana maendeleo halisi, Natumai ndugu yangu una ndoto ulizonazo,na unatamani siku moja uzifanikishe. sasa nataka nikwambie kitu ambacho kitakusaidia ili uweze kuzifanikisha ndoto zako. Waswahili husema mali bila kalamu huisha bila habari,usemi huu nimekuwa nikiutumia katika maisha yangu ya kila siku.  Mimi nautumiaje? Jinsi ninavyo utumia usemi huu ni tofauti na jinsi maana ya usemi wenyewe. mimi huutumia usemi huu kuandika kile ambacho ninaota kukifikia. ndugu yangu ukitaka kufikia ndoto zako nilazima ufuate aya: Chukua kalamu na Karatasi/Diary yako kisha anza kuandika,andika aya,  Andika tarehe ya leo,   Andika malendo yako yote ...
Image
NJIA ZA KUKUTOA KATIKA KIFUNGO CHA UMASKINI. Habari za leo ndugu msomaji wangu. Nisiku nyingine tena tunakutana apa kwa lengo la kuelimishana na kuabalishana ili tuweze kuakikisha tunamtokomeza adui yetu mkubwa UMASKINI. Katika dunia ya leo tumekuwa tukishindwa kufikia malengo yetu kutokana na sababu mbali mbali zinazo tukabili katika maisha yetu ya kila siku. Sababu ni nyingi ila kwa leo sitazizungumzia bali ninapenda kwa nafasi ya pekee niweze kuzungumzia njia ambazo ndio muongozo katika maisha yetu ili tuweze kukabiliana na changamoto zinazo tukumba kilahisi. Ukiwa kama kijana unaye taka kuleta mabadiliko katika maisha yako inatakiwa mambo yafuatayo uyazingatie sana: 1. AMINI UNAWEZA. Kati ya mambo makubwa yanayotukwamisha katika kufikia ndoto zetu ni kuhisi kuwa hatuwezi kufanya jambo fulani. Ondoa katika fikra izo maana pindi unapo hofu kuwa huwezi kumbuka unateketeza ndoto zako. Jiamini kuwa unaweza,hakuna mtu anaye weza kuja kubadili maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe. 2. ...
Image
MAMBO 17 AMBAYO TAJIRI NA MASKINI HUTOFAUTIANA KATIKA KUFIKILIA KWAO. Habari za leo,natumai umzima kabisa na umejaa rehema za Mwenyezi Mungu. Karibu tena katika makala yangu ya leo ninapo kwenda kukupa mtazamo kati ya TAJIRI na MASKINI,zifuatazo ni baadhi ya tofauti zilizopo kati ya makundi aya mawili. 1.TAJIRI huamini kuwa maisha yake ameyatengeneza mwenyewe,wakati MASKINI yeye huamini kuwa maisha hujitokeza tu. 2. TAJIRI hutumia pesa ili kushinda,wakati MASKINI hutumia pesa ili kushindwa. 3. TAJIRI hujituma ili kuwa tajiri,wakati MASKINI yeye hutamani kuwa tajiri bila kutenda 4. TAJIRI hufikiria mambo makubwa,wakati MASKINI huwaza mambo madogo. 5. TAJIRI hutizama fursa zilizoko mbele yake,wakati MASKINI yeye utizama vikwazo vilivyoko mbele yake. 6. TAJIRI huwausudu matajiri wengine na watu waliofanikiwa,ila MASKINI huwachukia matajiri na watu maarufu. 7. TAJIRI hujihusisha na  watu wanye mafanikio,wakati MASKINI yeye hujiusisha na maskini wenzake. 8. TAJIRI hutumia pes...

MKAKATI WA MAFANIKIO MWAKA HUU

Image
Kwanza napenda nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuweza kutufikisha siku hii ya leo,pili nawashukuru wazazi wangu kwa kuweza kunileta duniani isitoshe wameweza kunilea kwakipindi chote sikuwa mzigo kwao bali walivumilia mapungufu yangu nakuweza kuninyoosha katika njia ilio njema mwisho nawashukuru wadogozangu kwa kuonyesha ushilikiano wa hali na mali katika maisha yetu ya kila siku. Kwa kuanza napenda kukukaribisha ndugu yangu msomaji katika makala yangu hii ya ujasiliamali, juu ya mada MKAKATI WA MAFANIKIO MWAKA HUU. Kwanza tujiulize ujasiliamali ni nini? ujasiliamali ni hali ya mtu kujitoa kwa hali na mali kutumia rasilimali zilizopo ili kuweza kujitengenezea kipato cha ziada.  Kabla yakuendelea Ebu tujiulize maswali yafuatayo: (i) wewe ulie ajiliwa mshahara unaopata katika ajila yako unakutosha? (ii) je unamudu maitaji yako ya kila siku? (iii)mshahara wako unatosha kulipa madeni ulio nayo? (iv) Kama mshahara wako kwa sasa haukutoshi je ukistaafu...

UTAJIKWAMUAJE KATIKA UMASKINI?

Image
Hatua za maendeleo katika maisha zinaitaji kujipanga. Ebujiulize toka mwaka umeanza umefanya mambo gani, na nimambo mangapi yamefanikiwa na nimangapi hayakufanikiwa? Kati ya yale ulioshindwa kuyafanikisha je umetambua sababu zilizosababisha ushindwe kufanikiwa? Je yale ulioyafanikisha umeweka mikakati gani ili yaweze kuendelea kudumu? Ebu jiulize kuwa katika shughuli zako za kila siku ni muda gani unautumia kufanya mambo ya msingi na ni muda gani unaupoteza kwa kufanya mambo yasiofaa? NA je muda wako umeugawaje,nimuda kiasi gani unautumia kufanya maendeleo ya kwako binafsi na ni muda gani unautumia kuwanufaisha wengine? Ndugu yangu kupitia FAN Company LTD Utaweza kuonyeshwa njia sahii itakayo kuingizia kipato kizuri pasipo kuwa na mtaji mkubwa maana najua vijana walio wengi ukimwambia kuhusu kujiajili anakwambia sina mtaji. Njoo FAN Compani LTD Tukupe suluhisho ambalo utajitengenezea kipato utakacho endelea kukipata mpaka mwisho wa maisha yako na bado kizazi chako kitaendel...

JE UNATAKA KUWA MJASIRIA MALI WA KISASA?

Image
Ujasiriamali ndio neno jipya. Kila mtu anaongelea habari za ujasiriamali. Pengine hii inatokana na wengi wetu kutambua kwamba nyakati zimebadilika na ujasiriamali ndio njia iliyo sahihi zaidi kama mtu anatamani mafanikio ya kweli maishani.Vijana ndio chachu zaidi ya ujasiriamali au naweza kusema ndio wanategemewa zaidi kuendeleza ujasiriamali hususani katika ulimwengu wa leo wa sayansi na tekinolojia. Pamoja na nia nzuri walizonazo vijana, pengine ukiwemo wewe unayesoma makala hii, kipo kizingiti ambacho ni lazima watu wajifunze mbinu mpya za kukivuka. Kizingiti hicho ni aina ya elimu itolewayo mashuleni. Kwa bahati mbaya elimu zitolewazo mashuleni bado hazijawekwa katika msingi unaomuwezesha kijana kujiajiri au kwa maneno mengine kuwa mjasiriamali pindi amalizapo masomo yake. Bado tupo katika ule mfumo wa kikoloni. Ukimaliza shule unachotakiwa ni kuanza kutafuta kazi. Zunguka jijini Dar-es-salaam kwa mfano, utakutana na vijana wengi wasomi waliohitimu katika vyuo vikuu mbalimbali...

HIZI NDIO SIRI KUPATA UTAJIRI HAPA DUNIANI

Image
Watu wengi hatujitambui tunaishi bila kujua maisha yetu binafsi yanakwenda wapi. Kutojitambua huko ndio chanzo cha wewe kubaki kila siku unahudumiwa na mama au baba kila kitu ukihisi  bado mtoto mdogo, ukilalamika pesa huku wewe ni muhitimu wa chuo, umelemewa na madeni huku una elimu,huna uhuru wa kula na kununua kitu kisa huna pesa. Ndugu yangu jitambue uko wapi na unaelekea wapi weka ndoto na malengo,weka jitihada,tenga muda,mkabidhi mungu,epuka watu wenye mtazamo hasi,jiamini unaweza tenda miujiza, amini mabadiliko ktk maisha yanawezekana bila mtaji mkubwa,acha kubagua kazi kisa una elimu kubwa. unapokuja kwenye suala la pesa ndg yangu elimu haina msaada sana kwani elimu ya pesa haifundishwi darasani na mitaala yetu inatuandaa na kutujengea fursa ya kutafuta ajira na wala sio kujiajili.  Sasa leo jitambue rafiki na ubadilike: 1. WATU WENYE MUDA MWINGI PESA HAWANA. ~Kundi hili linakera sana kwani ndio kundi pekee lenye mtazamo hasi katika jamii. Hawa watu wamekata tamaa n...

FUATA NJIA HIZI ILI USIFE NJAA WAKATI UNA ELIMU YAKO

Image
Ukipata nafasi ya kusoma na kuajiriwa, jamii zetu nyingi za Kiafrika zinakuwa na matazamio makubwa kuliko uwezo wako halisi. Kama unatokea kwenye familia zetu za kawaida(za hali ya mtu); wakisikia upo kazini na unalipwa tsh laki tano basi wanaona unapata mahela mengi sana.  Baba na mama wanataka uwajengee, wadogo zako wanataka uwasomeshe, ndugu wanataka uwe unawakumbuka kwa vi-MPESA, wanataka uhudhurie ama utume pesa katika misiba na sherehe zote za huko kwenu, hapo sijataja wale waliofeli shule nao wanatumwa kwako uone utawasaidiaje! Hayo tisa, kumi ni kwamba hao hao wanaokurundikia majukumu wanataka kuona unapata maendeleo; uwe na gari, nyumba, n.k.  Ukikwama utaanza kumiminiwa lawama na majungu, ohoo, ajira anayo lakini maendeleo hana! Mara ohoo, tangu apate kazi amewasahau kabisa hasaidii ndugu zake na mengine mengi! Masikini ya Mungu kumbe hawajui kuwa katika hako ka laki tano; laki nzima unalipa pango, laki mbili na ushee inakatika kwenye misosi, laki nyingine nauli...