NDOTO ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.
NDOTO ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.
Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu, Nisiku nyingine tena tunakutana katika jukwaa ili la ujasiliamali ili tuweze kupeana elimu tena. Leo nitapenda tuweze kutazama mbinu na taratibu za kuweza kufikia mafanikio yetu.
Siku zote katika maisha lazima uwe na ndoto kama wewe ni mwana maendeleo halisi, Natumai ndugu yangu una ndoto ulizonazo,na unatamani siku moja uzifanikishe. sasa nataka nikwambie kitu ambacho kitakusaidia ili uweze kuzifanikisha ndoto zako. Waswahili husema mali bila kalamu huisha bila habari,usemi huu nimekuwa nikiutumia katika maisha yangu ya kila siku. Mimi nautumiaje? Jinsi ninavyo utumia usemi huu ni tofauti na jinsi maana ya usemi wenyewe. mimi huutumia usemi huu kuandika kile ambacho ninaota kukifikia. ndugu yangu ukitaka kufikia ndoto zako nilazima ufuate aya:
- Chukua kalamu na Karatasi/Diary yako kisha anza kuandika,andika aya,
- Andika tarehe ya leo,
- Andika malendo yako yote unayo taka kuyafikia katika maisha akikisha umetenga malengo yako katika makundi mawili maana kuna malengo ya muda mfupi na malengo ya muda mrefu.Katika malengo ya muda mfupi onyesha muda ambao ungependa uwe umeya fikia pia ya muda mrefu vilevile.
Ukisha maliza ayo basi akikisha kuwa una yazingatia na ukitaka uwe unayakumbuka yaweke katika sehemu ambayo utakuwa unayaona kila mala,au ikiwezekana bandika karatasi iyo chumbani kwako ili uweze kuwa unayaona kila mala uingiapo na utokapo.
kitendo cha kuwa unayaona mala kwa mala kitakufanya uwe na molali ya kuyafanikisha na endapo utakuwa unafanya kitu kinacho kurudisha nyuma ukiyakumbuka au kuyaona basi utaweza kurudisha molali ilio potea
Baada ya kuwa umeorozesha malengo yako basi tengeneza mikakati ya kuweza kuyafikia malengo ayo,apa sasa ndio unatakiwa kuwa makini akikisha unaweka mbinu za kutosha ili uweze kufikia malengo, Kama lengo lako ni kuwa tajiri mkubwa basi anza kuweka akiba kidogokidogo,anza kuudhulia semina za ujasiliamali,tafuta fursa zisizo itaji mitaji mikuwabwa,watafute watu walio kwisha fanikiwa kisha jifunze kwao ni mbinu gani walizitumia kisha wakafanikiwa. vivyoivyo katika njia zingine,yawezekana unataka kuwa muhamasishaji wa kimataifa,au mtoa elimu ya ujasiliamali mkubwa kama mimi,fanya ivyo ivyo,pia husisahau kusoma vitabu ili uweze kuji funza zaidi
Njia ya mwisho unayo paswa ufanye ili ufanikiwe katika maisha ni kuamua kufanya kwa vitendo sasa. baada ya kuwa umeweka mikakati ya kutosha sasa unaingia katika kutenda,akikisha unazitumia fursa zilizopo ili usije ukajikuta unashindwa kufikia malengo kwa kujihusisha na fursa zilizo pitwa na wakati, kwakuzingatia malengo na ndoto zako anza kuteda kwa kasi ili mwisho wa siku uweze kufanikisha lile ulilo lilenga. kipindi iki huwa kigumu sana mana changamoto huwa nyingi unachotakiwa kufanya ni kutokata tamaa,maana kuna watu walianza kuzielekea ndoto zao lakini walikumbana na vikwazo vingi ila kati yao kuna walio kata tamaa na kushindwa kuendelea ila wale walioendelea tena ndio waliofanikiwa zaidi. jifunze kwa walio fanikiwa husiwafuate walio shidwa watakukatisha tamaa.
Ndugu yagu zingatia ayo kisha utafanikiwa,namalizia kwakusema,Juhudi na maarifa ndio zitakazo kufikisha pale utakapo. kwa ushauri zaidi wasiliana nami whatsapp/text +255 785 494 456 pia tunatoa semina za biashara na ujasiliamali kupitia whatsapp kwa gharama nafuu tumia namba iyo apo juu kwa maelezo zaidi
Comments
Post a Comment