KANSA YA TITI (BREAST CANCER)
KANSA YA TITI. Huu ni uvimbe ambao unatokea kwenye titi ambao huathiri ukuaji wa seli zinazounda titi na kusababisha zikue kwa kasi kubwa isivyo kawaida. Seli hizi hutokea ambazo huathiriwa ktk ukuaji hupatikana sehemu zifuatazo: ~Kwenye tezi za titi (Lobular carcinoma) ~kwenye mirija ya maziwa (tubular carcinoma) ~Kwenye chuchu ya titi (Pagets disease of the nipple) Hizo ni sehemu kuu tatu ambazo seli za titi huathirika na kuwa seli za kansa. Hivyo basi kwa ujumla unaweza kusema kuwa kuna aina kuu tatu za kansa za titi kama nilivyo changanua hapo juu msomaji. UTOFAUTI KATI YA KANSA YA TITI NA UVIMBE WA KAWAIDA KWENYE TITI. ~Uvimbe ambao ni kansa ukuaji wake ni wa kasi sana ukilinganisha na uvimbe wa kawaida. Mfano:Anaweza kuja rafiki yako anakueleza huu uvimbe upo hapo tangu miaka 5 iliyopita huwa unaongezeka lkn kidogo mno. Hapo utajua sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu. Lakini pia rafiki yako anaweza kuja anakueleza nina uvimbe hapa akifunua unakuta titi l...