KANSA YA TITI (BREAST CANCER)
KANSA YA TITI.
Huu ni uvimbe ambao unatokea kwenye titi ambao huathiri ukuaji wa seli zinazounda titi na kusababisha zikue kwa kasi kubwa isivyo kawaida.
Seli hizi hutokea ambazo huathiriwa ktk ukuaji hupatikana sehemu zifuatazo:
~Kwenye tezi za titi
(Lobular carcinoma)
~kwenye mirija ya maziwa (tubular carcinoma)
~Kwenye chuchu ya titi
(Pagets disease of the nipple)
Hizo ni sehemu kuu tatu ambazo seli za titi huathirika na kuwa seli za kansa.
Hivyo basi kwa ujumla unaweza kusema kuwa kuna aina kuu tatu za kansa za titi kama nilivyo changanua hapo juu msomaji.
UTOFAUTI KATI YA KANSA YA TITI NA UVIMBE WA KAWAIDA KWENYE TITI.
~Uvimbe ambao ni kansa ukuaji wake ni wa kasi sana ukilinganisha na uvimbe wa kawaida.
Mfano:Anaweza kuja rafiki yako anakueleza huu uvimbe upo hapo tangu miaka 5 iliyopita huwa unaongezeka lkn kidogo mno. Hapo utajua sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu.
Lakini pia rafiki yako anaweza kuja anakueleza nina uvimbe hapa akifunua unakuta titi limevimba sana na limekuwa kubwa ukimuuliza tangu lini huu uvimbe mbona unatisha...atakwambia umenianza miezi kumi tu uliopita ila linakuwa kwa kasi sana.
Huo uvimbe lazima ufikilie kuwa ni kansa labda uhakikishwe kwa vipimo vya maabara.
~Pia sio kila mtu anaye lalamika titi limevimba ni cancer sio ukweli.
Inaweza kuwa amepata maambukizi ya bakteria tu na kusababisha kuvimba kwa titi tunaita mastitis. Au inaweza kuwa ana jibu kwenye titi (breast abscess)
Hivyo haya yote unatakiwa uhakikishe mgonjwa wako hana ili kuhakikisha kuwa yale unayofikilia kuwa ni kansa ya titi kuwe na ukweli ndani yake.
Pia unatakiwa kumuuliza chanzo cha titi kukua au kuvimba kiasi hicho inaweza kuwa kuna ugomvi ulitokea ikapelekea mtu kupigwa na kuumizwa.
Hivyo usifikilie mbali tu kwamba kila uvimbe sasa unawaza huyu mtu ana kansa.
~Pia uvimbe wa kansa ukuaji wake ni kasi sana hata ukimuuliza mgonjwa atakusimulia historia fupi ya ugonjwa ukilinganisha na uvimbe mwingine ambao sio kansa.
Napenda nikwambie kuwa leo basi ukizingatie elimu hii unaweza ukawa tabibu mzuri wa familia yako kupitia elimu hii.
Pia uvimbe ambao ni kansa mwanzoni huwa hauna maumivu kabisa lakini ukisha fika hatua mbaya utakuwa na maumivu makali sana.
kwa sababu ukitaka kujua hii sio kansa mwanzo ni KUTUMIA DALILI YA MAUMIVU.
Unakuta titi linauma na limeng'aa hapo moja kwa moja utajua kuwa inaweza kuwa ana maambukizi tu yani mastitis au ana jipu kwenye titi breast abscess.
Hivyo basi kwa hatua za mwanzo uvimbe wa kansa huwa hauna maumivu yoyote mpendwa msomaji wangu. Na ukikuta unapata dalili zenye maumivu makali na una kauvimbe na ni siku chache tu kametokea usianze kuhangaika na kupatwa na msongo wa mawazo kuwa una uvimbe kama KANSA.
VISABABISHI VYA KANSA.
Mpendwa napenda nikwambie kuwa hadi sasa ninavyo andika hii makala bado kisabanishi mahususi cha kansa ya titi hakijulikani kabisa ni nini!!!!
Hivyo basi kutokana na hayo napenda nikupe makundi ya watu ambao wapo hatarini kupata kansa ya titi hapa duniani.
~Mwanamke yupo hatarini kuzidi mwanaume
~Mwanamke yeyote ambaye yupo kwenye umri wa kubarehe hadi kikomo cha hedhi.
~Wanawake wazungu wapo hatarini kuzidi africa(lakini mwanamke wa kiafrica yuko hatarini kupata kifo cha kansa ya titi kuliko mzungu)
~Mwanamke ambaye aliwahi sana kuingia kwenye kubarehe.
~Mwanamke ambaye amechelewa kufikia kikomo cha hedhi
~Mwanamke mwenye UZITO MKUBWA KUPITA KIASI
~Mwanamke anayependelea kula vyakula vya mafuta mabaya....bad cholesterals(mafuta yatokanayo na nyama)
~Wenye magonjwa km HIV,KISUKARI ambayo hushusha kinga ya mwili.
~Kuchelewa kupata mtoto na kutokupata mtoto kabisa
~Nchi zilizo endelea zipo hatarini sana kupata aina hii ya kansa kuliko nchi zinazo endelea km tanzania.
~kurithi kama kuna mtu katika ukoo wenu ana aina hii ya kansa unaweza kupata chembe chembe za urithi ya kansa hii ambavyo ni BRCA1 na BRCA 2.
~Kuwa na VICHOCHEO VYA ESTROGEN VINGI NDANI YA MWILI WAKO KWA MUDA MREFU.
~Ulaji wa vyakula vya viwandani hasa vyenye sukari nyingi, rangi na vilivyowekewa radha na kusindikwa.
Hivyo ni baadhi ya VITU HATARISHI VINAVYOWEZA KUKUSABABISHIA KUPATA KANSA YA TITI.
NOTE: Ndugu msomaji hivyo hapo juu sio visababishi ni VIHATARISHI VYA WEWE KUPATA AINA HII YA KANSA.
Hivyo basi endelea kujua kuwa kuepuka aina hii ya kansa ni kuviepuka hivyo visababishi.
KUSAMBAA KWA KANSA YA TITI.
Ndugu mpendwa ninapo ongelea kusambaa kwa kansa ya titi nitakuwa mchoyo sana wa elimu km nisipokuambia namna gani kwanza unaweza kuzuia kansa yako isifikie hapa.
~TUNAKUSHAURI UPATE KIPIMO TUNAKIITA MAMMOGRAPHY ambacho ni SCREENING TEST.
Lugha nyepesi ya neno screening ni kitendo cha kubaini ugonjwa kutoka kwa watu wazima.
Mfano:Unaweza ukawakusanya watu mia moja wamejipanga ukaanza kuwafanyia hicho kipimo..miongoni mwao watabainika na kansa ya titi hatua ya mwanzo lakini walikuwa hawajijui kuwa ni wahanga wa huu ugonjwa.
Hivyo kitendo cha kubaini watu wagonjwa kutoka kwenye watu wazima ambao hawana dalili zozote tunaita screening.
Sasa kuna kifaa ambacho hutumika kubaini wagonjwa wa kansa ya titi katika hatua za mwanzo kabisa ambapo inaweza kutibika kutoka kwa watu wazima tunaita ni MAMMOGRAPHY (PICHA YA TITI.) Hiki kipimo kinatumika kubaini uvimbe wa hatua za mwanzo kabisa hivyo kwa teknolojia yetu ndicho ambacho tunatumia.
Nakushauri ujijengee tabia ya kucheki afya yako ya titi kila mwaka ili kujiepusha na matatizo haya.
INGAWAJE!!!
Hadi sasa wenzetu wenye technolojia za juu katika tiba bado wamefikia kusema kuwa kipimo hiki hakina msaada sana tofauti na KUBADILI MWENENDO WA MAISHA.
Maana hata km ukipimwa ukikutwa na kansa hakuna kitakacho fuatia tofauti na kuhangaika kuitibu na usipofanikiwa basi.
Hivyo kikubwa ni KUBADILI MWENENDO WETU KUYAEPUKA YALE NILIYO YATAJA.
Sasa endapo ukachelewa kubaini uvimbe huu unaweza kusababisha kusambaa sehemu mbali mbali km kifuani,kwenye ubongo,kwenye mifupa nk.
Hivyo tujitahidi KUCHEKI AFYA ZETU KILA MWAKA KUBAINI UVIMBE HUU HATARI MAPEMA UKIWA HATUA ZA MWANZO.
DALILI ZA KANSA YA TITI.
~Uvimbe wowote ule kwenye titi hakikisha unautilia maanani kujua ukweli wake
~Kutokwa na maziwa, usaha na damu au damu imechanganyika na usaha.
~Titi kubalika rangi linakuwa linang'aa na kupoteza vinyweleo
~Pia titi linaweza kubadirika na kuwa jeusi sana
~Kupata maumivu makali km imefikia hatua mbaya.
DALILI ZINAZO ONESHA KANSA IMEANZA KUSAMBAA HATUA MAHUSUSI ZICHUKULIWE
~Kukohoa sana na upumuaji wa shida.
(Inaonesha kansa imesambaa kifuani kwenye mapafu)
~Mifupa kudhoofika na kuuma.
~Kupata matitizo ya ubongo (kupoteza fahamu, kupalalaizi nk)
~Kuvimba kwa tezi za mfumo wa kinga za mwili..kwapani na sehemu zingine
Hizo ni dalili ambazo
zinaonesha kansa imesambaa kwenye mapafu,mifupa na ubongo.
NOTE: UNAPOSEMA KANSA IMESAMBAA LAZIMA KUWEPO NA UVIMBE UNAONESHA KUWA MTU ANA KANSA YA TITI (CHANZO) NDIPO TUNAWEZA KUSEMA IMESAMBAA MAANA CHANZO KIPO.
KIPIMO AMBACHO UNAWEZA KUPIMA KANSA IMEFIKIA PABAYA.
Kuna vipimo vya aina mbali mbali au naweza kusema ni vigezo ambavyo jopo la wana sayansi walikaa na kukubaliana kwa pamoja ili duniani kote vigezo hivyo vikitamkwa vitambulike na kila mtaalamu wa afya.
Sasa rafiki yangu usije ukasema niliambiwa na Frank bali ujue kuwa haya ni makubaliano ya wanasayansi duniani kote.
leo nataka nikufundishe kigezo kimoja CHEPESI KABISA.
Hiki ni kigezo ambacho kinapima jinsi gani kansa imefikia katika mwili wako rafiki.
Ambapo sasa inachunguza vigezo 3.
1.Ukubwa wa UVIMBE KATIKA TITI
2. TEZI ZILIZOFIKIWA NA KANSA.
3. KUSAMBAA KWA KANSA.
MCHANGANUO HUU UNAITWA KITAALAMU TMN CLASSIFICATION
T~Tumor (uvimbe)
N~Lymph nodes(Tezi)
M~Metastasis(kusambaa kwa seli kansa )
1. UKUBWA WA UVIMBE
Ukubwa wa uvimbe umechanganuliwa nao kwa kutumia vigezo vyake rafiki km ifuatavyo
T0~Huyu hana uvimbe kabisa kwenye titi hata kwa kutumia kile kifaa cha screening.
Tx~Huyu ana uvimbe lakini tunashindwa kuufikia kwenye titi
T1-Huyu ana uvimbe ambao ni chini ya sm 2
T2-Huyu ana uvimbe ambao ni kati ya sm 2-sm 5
T3-Huyu ana uvimbe ambao ni zaidi ya sm 5
T4- huyu ana uvimbe ambao ni mkubwa mno umeanza kuvamia hadi misuli ya kifuani.
2. TEZI
Basi tunapenda kujua pia kama kansa hii ya titi imeanza kusambaa au laa.
Tunaweza kubaini hii hali kwa kuchunguza kuvimba kwa tezi za kwapani.
Napo kuna mchanganuo wake na una maana yake wapendwa
N0- Hakuna kabisa tezi hizi hazifikiwa
Nx- tezi hizi zimefikiwa lakini hazijakua
N1- Tezi za upande mmoja wa titi husika zimefikiwa na zipo zinacheza ukizigusa
N2: Tezi za upande mmoja zimefikiwa na hazichezi
N3 - TEZI ZA UPANDE WOTE WA TITI KWAPANI ZIMEFIKIWA.
Basi naomba nihamie kwingine.
3. KUSAMBAA KWA KANSA.
Hapa tunatumia michanganuo miwili tu.
M0: Kansa haijasambaa
M1: Kansa imesambaa kwenda labda kwenye mapafu,ubongo,mifupa n.k
DHUMUNI LA KUJUA MCHANGANUO HUO NI KM IFUATAVYO
~Unatuwezesha kujua hatua ya ugonjwa ulipo fikia
~Unatuwezesha kujua namna gani huyu mgonjwa tumtibu.
MFANO:
~MTU KAPIMWA KAAMBIWA ANA MAJIBU HAYA
T0N0M0
Maana yake huyu yupo poa kabisa
T1N0M0
Maana yake huyu ana uvimbe upo chini ya sm 2 lakini tezi hazifikiwa na kansa haijasambaa.
Nazani mpendwa msomaji UNAWEZA KUWA UMEPATA PICHA NAAMANISHA NINI KUHUSU KUJUA MCHANGANUO HUU...NILITAKA KUKUPA PICHA WANAPOSEMA KUWA KANSA STAGE 1,2,3,4 HUWA WANA MAANISHA NINI KWA UJUMLA NA HUWA WANACHUNGUZA VIGEZO GANI. NAZANI KUPITIA MAKALA YANGU HII UMEJIFUNZA KITU RAFIKI.
Kuna aina nyingi sana za kuchanganua kansa pia kuna kuchanganua kwa kutumia majibu ya maabara lakini sitapenda kuzungumzia sana maana picha halisi umepata ndugu yangu.
STAGE 1~~ T1N0MO,T2N0M0
STAGE TWO~ T2N1M0
AU T3N1M0
STAGE THREE
T3N2MO au T3N2M1
STAGE FOUR
TAYARI KANSA IMESAMBAA NA HAKUBA NAMNA.
KIDOGO HAPO JUU UNATAKIWA UKAE UTULIE MSOMAJI WA MAKALA ZANGU.
LAKINI LENGO PALE NILITAKA KUKUONESHA VIGEZO VINAVYOTUMIKA KUSEMA HII NI KANSA STAGE FLANI WANAZINGATIA VIGEZO VITATU KM NILIVYOSEMA HAPO JUU.
MATIBABU;
Kwa ujumla kansa hutibiwa kwa njia kuu nne kulingana na stage rafiki msomaji.
~Njia ya operation
Kuna operation ndogo ya kuondoa kauvimbe kadogo (lampectomy) au kuna operation kubwa ya kuondoa titi lote (mastectomy)
~Njia ya dawa za kansa
Kama Cyclophosphamide, flurouracil na Methotreaxate.
Dawa hizi pia hupewa wagonjwa baada ya operation kumaliza chembe chembe za seli za kansa zilizobaki
~Njia ya mionzi.
Hii ni mionzi mikali ambayo huruhusiwa kugonga moja kwa moja kwenye uvimbe husika na kuua seli za kansa. pia njia hii hupatiwa watu baada ya kupata operation au ambao wapo hatua mbaya ya kansa
~Njia ya mwisho ni NJIA YA KUTIBU DALILI TU KUKUWEZESHA UISHI ANGALAU MIAKA MICHACHE MBELE (PALLIATIVE CARE)
Hapa utakuwa unapata dawa za maumivu,utapewa mionzi na dawa za kansa lakini hali ndivyo mbaya.
NOTE:
Dawa hizi za kansa huja na madhara mengi sana
~Kushusha kinga ya mwili
~Kunyonyoa nywele
~Kumaliza damu
~kumaliza nguvu za kiume
Na madhara mengine mengi hivyo na hizi dawa HUTUMIKA MAISHA YAKO YOTE MAANA DAWA HIZI NDIO UHAI WAKO.
LAKINI KUTOKANA NA CHANGAMOTO ZIFUATAZO
~Dawa za kansa ndio dawa pekee ambazo ni za gharama kuzidi dawa za aina yoyote duniani.
~Dawa za kansa ni dawa zenye madhara makubwa kuzidi dawa za aina yoyote hapa duniani
Tafiti zinazidi kuongezewa hadi sasa nchi zinazo endelea zinazidi kushindana na kupunguza kasi ya kukua kwa makampuni ya kibillionaire yanayo zalisha vidonge vya kansa kwa kuanza kuzalisha mbadala wake
~BEI RAHISI
~HAZINA MADHARA KWA MTUMIAJI
~ZENYE KUBORESHA KINGA YA MWILI NA SIO KUBOMOA.
Unaweza kupata bidhaa mbali mbali na ukazisoma kwa kina au kutembelea ktk ofisi zetu utakuja ujifunze bidhaa mbali mbali za ASILI KUTOKA CHINA NA THAILAND ZINAVYOWEZA KUUA SELI ZA KANSA BILA MADHARA MAKUBWA KM DAWA ZA KEMIKALI.
BIDHAA HIZI NI KAMA ZIFUATAZO
~Unga wa ginsenoside wenye viini vikubwa kama RG3 Na RH3
Vina uwezo mkubwa wa kuangamiza kuangamiza seli za kansa bila kuathiri kinga ya mwili.
Viini hivi vinajulikana kama MFALME WA UVIMBE Baada ya nchi kama chini kutumia kwa muda mrefu sasa mimea hii inapatikana katika mfumo wa vidonge wa kisasa kabisa.
Mbali na kuangamiza seli za kansa pia HUONGEZA KINGA YA MWILI NA KUIMARISHA AFYA.
Pia rafi yangu tutakupatia vidonge 60 vya uyoga mwekundu maana nimekwambia mwanzo mafuta mabaya ya cholesteral ni chanzo cha uvimbe huu, mbali na kuondoa cholesteral uyoga mwekundi unatibu magonjwa mengi mno na kurudisha afya yako na kinga ya mwili wako ulio dhoofika.
Sitasahau pia KUKUPATIA BIDHAA ADIMU SANA AMBAYO NDIO IMESHIKA NAFSI ZA JUU KABISA KWENYE JUKWAA LA MATABIBU KATIKA KUTUMIA KIINI CHEKUNDU YANI LYCOPENE KATIKA KUZUIA KANSA NA KUTIBU KANSA.
SASA UTAPATA VIDONGE VILIVYO TENGENEZWA KWA KUTUMIA KIINI CHEKUNDU CHA NYANYA HAPA HAPA TANZANIA.
Nitapenda UWE MMOJA YA WATU WANAOFURAHIA BIDHAA ZETU RAFIKI, KANSA INATIBIKA, WAHI MAPEMA KABLA HAIJAFIKIA HATUA MBAYA KABISA.
BIDHAA ZETU UNAWEZA KUTUMIWA MKOA WOWOTE ULIPO RAFIKI HAIHITAJI KUSAFILI KUFUATILIA TIBA.
DOSE: INATEGEMEA NA HATUA YA UGONJWA WAKO BAADA YA KUJADILI NA MIMI KUPITIA SIMU/ANA KWA ANA NITAKUPA MAELEKEZO.
Imeandaliwa na kutolewa
Frank Alfred
Pole sana kwa kuugua au kuuguliwa.
Asante.+255785494456
Comments
Post a Comment