FAIDA ZA MMEA WA GINSENG
FAIDA ZA MMEA WA GINSENG.
Ginseng ,au maarufu kama “king of herb” (mfalme wa mimea). Mmea huu umekuwa moja ya maajabu ya dunia kutokana na uhodari wake katika matibabu. Mmea huu unapatikana hasa kaskazini mwa America na Mashariki mwa Asia(hasa kaskazini mwa china,Japani na Korea) hasa maeneo yenye baridi.
Kuna aina kuu mbili za mmea huu : American Ginseng(Panax quinquefolium) na Asian Ginseng au China ginseng(Panax ginseng)
American Ginseng ni zenya asili ya ubaridi( Ying energy) na Asian Ginseng ni zenye asili ya ujoto(Yang ginseng) , hivyo basi watu wenye asili ya ubaridi au waishio maeneo ya baridi wanashauriwa kutumia Asian ginseng ili waweze kupata joto na wale wenye asili ya joto au waishio maeneo ya joto wanashauriwa kutumia American ginseng kwaajili ya kuongeza baridi katika mili yao. Vinginevyo matatizo makubwa yanaweza kujitokeza hasa kwa watu wenye shinikizo la damu .
Mbali na utofauti wote huo lakini mimea yote ina kiungo cha GINSENOSIDE, ambacho ni kiambata kikuu cha tiba. Kuna aina nyingine inaitwa Siberia ginseng ,ila sio ginseng alisi bali ni mmea mwingine (Eleutherococcus senticosus) ambao ufanana kwa ukaribu kabisa na mmea tiba wa ginseng. Mmea huu wa Siberian ginseng una kemikali ya eleutherosides badaa ya ginsenosides.
Mmea wa ginseng (Asian na American ginseng) unahistoria ndefu sana ya kukumbukwa katika uponyaji wa magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya kawaida mpaka kansa. Nguvu ya uponyaji ya mmea huu wa ginseng inachangizwa na uwezo wake wa kuwa na asili ya viambata ambavyo uongeza kinga ya mwili mzima ,kwa kuongeza utendaji kazi wa viungo vya mwili na ubongo.
Nguvu ya uponyaji wa mmea huu wa ginseng inaufanya mmea huu kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa sugu kama uchovu wa kupindukia,kukosa nguvu mwilini,kukosekana kwa umakini mwilini,kukosa nguvu mwilini,kupoteza kumbukumbu,kukosa nguvu za kijinsia(nguvu za kiume na kike) pia uwezo mdogo wa kupona kwa haraka magonjwa na majeraha.
Sasa hebu tutazame uwezo wa mmea huu wa ginseng katika kutibu magonjwa mbalimbali:
1. Inapunguza Msongo wa Mawazo.
Ginsenoside ambayo inapatikana katika ginseng ina uwezo mkubwa wa kuuamsha ubongo na kuufanya uwe sawa wakati wote,uku ikiufanya kuwa katika usawa. Pia inasaidia kupambana na matatizo ya ubongo na kupambana na wasiwasi ambao mtu anaweza kuwa nao kutokana na misukosuko ya maisha. Unashauriwa kupata kidonge kimoja au viwili mara tatu kwa wiki ili kuuwezesha mwili wako kuwa active muda wote.
2. Kutibu ugonjwa wa sukari.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa mmea wa ginseng unauwezo mkubwa wa kushusha kiwango cha sukari mwilini hasa kwa mgonwa wa sukari daraja la pili. Mfano katika tafiti zilizofanyika mwaka 2000,ambapo watafiti waliweza kuwapatia wagonjwa wa sukari vidonge vya ginseng ambao walikuwa wakitumia tiba zingine zikiwemo na lishe. Lakini majibu yalionyesha kuwa wagonjwa waliotumia vidonge vya ginseng sukari ilishuka mpaka 59.1% ukilinganisha na wengine walioweza kutumia tiba zingine. Kutokana na uwezo wa mmea ginseng kuwa mkubwa bado haijajulikana mahusiano kati yake na tiba zingine ivyo inashauriwa mgonjwa anaye tumia ginseng hashauliwi kuchanganya kati ya tiba zingine na dawa za ginseng vinginevyo iwe kwa ushauri maalumu na uangalizi mkubwa.
3. Inaomgeza kinga ya mwili.
Kutokana na uwezo wa asilia wa mmea huu wa ginseng ,usaidia sana katika kudumisha na kuboresha kinga ya mwili kwakuongeza chembechembe nyeupe za damu(white blood cells) na kinga ya mwili katika damu.
4. Uzuia na kutibu Cancer(kansa)
Ginseng inakiambata cha ginsenoside yenyeuwezo wa kutibu magonjwa ya kansa. Ginsenoside uzuia viini sumu kuzaliana mwilini,ambavyo uzuia ukuaji wa viini kansa. Moja ya tafiti,wanasayansi walichunguza watu 4634 kwa kipindi cha miaka 5 nakugundua kuwa wale wote waliotumia dawa ya ginseng wana uwezekano mdogo sana wa kupata kansa ya mapafu,ini,ovary,kongosho na kansa ya tumbo. Na endapo umefanyiwa upasuaji kwa ajili ya kansa ni vyema kuonana na daktari kabla ya uanza kutumia ginseng.
5. Kuondoa mafuta mabaya mwilini.
Mmea wa ginseng umeweza kugundulika katika tafiti mbalimbali kuwa ina uwezo wa kuyapunguza mafuta mabaya mwilini. Watafiti wanaamini kuwa uwepo wa ginsenoside katika mmea wa ginseng basi uwezo wake wa kupunguza mafuta mabaya mwiini ni mkubwa.
6. Uwezo wa kuondoa uchovu mwilini.
Kutokana na uwezo asilia ,uliopo katik mmea wa ginseng,unauwezo wa kupambana na uchovu wote katika mwili wa mwanadamu na kufanya mishipa yote katika mwili kufanya kazi vizuri. Moja ya tafiti zilizofanyika kwa wauguzi waliokuwa wakifnya kazi kwa kubadilishana uko Britain, ginseng ilionekana kuwaongezea uwezo mkubwa wa utendaji kazi kutokana na kupungua kwa uchovu katika miili yao. Wauguzi hao pia waligundulika kuongeza ufanisi mkubwa katika shughuli zao za kila siku na kwa speed kubwa. Unashauriwa kumeza walau kidonge kimoja kila siku ili kuweza kujiweka katika mazingira ya kuwa na afya bora. Wataalamu wanashauri kutotumia ginseng kwa kipindi cha wiki moja(siku 7) ndani ya wiki tano ambazo unakuwa unatumia mmea huu,kufanya ivyo ni msaada kwa watu wenye matatizo ya ugonjwa wa insomnia na presha ya kushuka kuondokana na tatizo la kuwa waanga wa dawa hizi za ginseng.
7. Kuongeza Nguvu Mwilini.
Mbali na kuondoa uchovu lakini mmea wa ginseng uongeza nguvu na kuufanya mwili kuwa na stamina ya kutosha. Hivyo basi mmea wa ginseng umekuwa ukitumiwa kama dawa za kuongeza nguvu hasa kwa wana michezo.
8. Kuongeza Nguvu za Kiume.
Ginseng imekuwa ikitumiwa na watu wenye matatizo ya uhanithi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali. Mmea huu unasaidia sana katika uchajishaji na upevushaji wa nguvu za kiume na kuweza kumfanya mwanaume kuwa na uwezo mkubwa wa kushiliki tendo la ndoa bila shida yoyote. Tafiti zimeweza kuonesha kuwa Ginseng ina uwezo mkubwa wa kuwezesha uume kusimama vizuri na kuongeza uzalishaji wa mbegu za kiume na zenya ubora zaidi. Pia ni vyema kuonana na mtaalamu wa maswala ya afya kabla ya kuanza kutumia vidonge ivyo vya ginseng kwaajili ya ushauri zaidi.
9. Kuboresha Mmeng’enyo Tumboni.
Ginseng ni dawa sahihi kabisa ya kuweza kupambana na matitizo ya magonjwa ya tumbo kama kuhara,kukosa hamu ya chakula,kichefuchefu,kutapika na kuvimbewa.
10. Kutibu Magonjwa ya Moyo.
Faida nyingine kubwa ya utumiaji mala kwa mala wa mmea wa Asian ginseng, ni uwezo wake mkubwa wa kupambana na magonjwa ya moyo ikiwemo kuzifanya chembe sahani na kiwango cha mafuta katika moyo kuwa sawa. Baadhi ya tafiti zina pendekeza kuwa, ginseng inaweza kuwaadhili wenye shiniizo la damu. Ivyo basi ,wagonjwa wa shinikizo la damu wanashauriwa kuonana wataalamu wa afya kabla ya kuanza kutumia dawa ya ginseng.
Kwa matokeo bora unashauliwa kumeza giseng kwa mzunguko maalumu kwa kumeza kidonge kimoja kia siku kwa muda wa siku tano kwa wiki mbili mpaka tatu ,kisha unaacha kumeza kwa wiki tatu mfuluizo kisha unaanza tena.
By, Frank A. Ndyanabo-FAN
Je inachemshwa au
ReplyDeleteNiko Dar es Salaam.
ReplyDelete1. Napataje hii tiba? Pharmacy, au..?
2. Na kama naupata mmea wenyewe, nachemsha? Kwa muda gani mchemsho?
3. Kunywa/kula kiasi gani baada ya kupika?
Tafadhali. ASANTE.
••••••>> Barua-pepe yangu ni: pctarimu@gmail.com