ZIFAHAMU SIRI KATIKA KUZUIA MIMBA


Uzushi: Kujisafisha ukeni mara baada ya kufanya mapenzi huzuia mimba kutokea.  Ukweli: Mbegu za kiume zinaweza kuingia kwenye shingo ya mji wa uzazi mwanaume anapofikia mshindo, hauwezi kuondoa mbegu hizo kwa kujisafisha ukeni.
Uzushi: Mwanamke anayenyonyesha hana haja ya kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango. 

Ukweli: Mara nyingi kunyonyesha mara kwa mara na mfululizo kwa miezi 6 ya kwanza huzuia mimba. Hata hivyo sio kwa asilimia 100, kuna uwezekano mwanamke akapata mimba.
Uzushi: Mwanamke hawezi kupata mimba mara ya kwanza kufanya ngono. Ukweli: Mwanamke anaweza kupata mimba hata kama ni mara ya kwanza kufanya ngono.
Uzushi: Hauwezi kupata mimba ukifanya ngono huku umesimama. 
Ukweli: Unaweza kupata mimba hata kama ukifanya ngonoukiwa umesimama. Mbegu huingia na kufika kwenye mji wa mimba bila kujali mtindo wa mapenzi.
Uzushi: Kunywa vidonge vichache vya kuzuia mimba kabla au baada ya kufanya ngono ni njia ya uhakika ya kuzuiz mimba.
  Ukweli:Vidonge vya kuzuia mimba vinatakiwa kutumiwa kila siku ili vifanye kazi kwa ufanisi. Kunywa kabla au baada ya kufanya mapenzi kunaweza kusizuie mimba.
Uzushi: Kumwaga mbegu za kiume nje ya uke huzuia mimba kwa uhakika
Ukweli: Kiasi kidogo cha mbegu za kiume hutoka kabla ya mwanaume kufika mshindo. Mbegu hizi huweza kufika kwenye mji wa uzazi na kutunga mimba

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

ZIFAHAMU FAIDA KUMI NA NANE ( 18 ) ZA MTI WA MPAPAI