
NJIA ZA KUKUTOA KATIKA KIFUNGO CHA UMASKINI. Habari za leo ndugu msomaji wangu. Nisiku nyingine tena tunakutana apa kwa lengo la kuelimishana na kuabalishana ili tuweze kuakikisha tunamtokomeza adui yetu mkubwa UMASKINI. Katika dunia ya leo tumekuwa tukishindwa kufikia malengo yetu kutokana na sababu mbali mbali zinazo tukabili katika maisha yetu ya kila siku. Sababu ni nyingi ila kwa leo sitazizungumzia bali ninapenda kwa nafasi ya pekee niweze kuzungumzia njia ambazo ndio muongozo katika maisha yetu ili tuweze kukabiliana na changamoto zinazo tukumba kilahisi. Ukiwa kama kijana unaye taka kuleta mabadiliko katika maisha yako inatakiwa mambo yafuatayo uyazingatie sana: 1. AMINI UNAWEZA. Kati ya mambo makubwa yanayotukwamisha katika kufikia ndoto zetu ni kuhisi kuwa hatuwezi kufanya jambo fulani. Ondoa katika fikra izo maana pindi unapo hofu kuwa huwezi kumbuka unateketeza ndoto zako. Jiamini kuwa unaweza,hakuna mtu anaye weza kuja kubadili maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe. 2. ...