MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO

MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO.

Karibu sana ndugu msomaji wa makala zangu za afya, nisiku nyingine tena Mwenyezi mungu ananikutanisha na wewe katika ukurasa huu kwaajili ya kukuhabarisha mambo mbalimbali yahusuyo afya yetu. Kama kawaida Naitw Frank A. Ndyanabo,leo tutaangalia zaidi madhala ya ugonjwa ulcers(vidonda vya tumbo). Niugonjwa unaoshika kasi Tanzania na duniani kwa ujumla ambayo unatokana na mifumo ya maisha yetu.

VIDONDA VYA TUMBO:
Huibuka baada ya kutokea vidonda kwenye kuta za utumbo mwanadamu ambavyo utokana na kuzidi kwa kiwango cha tindikali yenye kazi ya kuyeyusha chakula kiingiacho mwilini.

Endapo mgonjwa hata patiwa tiba mapema uweza kusambaa zaidi adi kufikia mishipa ya damu na kupelekea madhara makubwa zaidi katika mwili.

Ugonjwa huu usababishwa na mambo mbalimbali yanayotokana na tabia zetu za kila siku ikiwa ni vyakula tunavyokula,lakini kitaalamu ujonjwa huu usababishwa na bakteria ajulikanae kwa jina la Helicobacter pylori.

MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBA
Kama yalivyo magonjwa mengine,vidonda vya tumbo vina madhara endapo havitapatiwa tiba ya uhakika au endapo muhusika atashindwa kufuata maelekezo aliyopewa na daktari kwa ukamilifu wake. Yafuatayo sasa ni madhara yake.
1. Uwezo wa kufanya kazi kupungua
2. Kifo
3. Kufanyika kwa upasuaji ili kuondoa eneo lote lililoathirika
4. Kupungua kwa nguvu za kiume
5. Msongo wa mawazo.

Ayo ndiyo baadhi ya madhara ya ulcers.

Somo lijalo litausu dalili za vidonda vya tumbo na Tiba za asili kwa vidonda ivyo,husikose.
Imeandaliwa na kutolewa na mimi Frank A. Ndyanabo.
+255785494456

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG