THAMANI YA SHUKRANI
THAMANI YA SHUKRANI.
Shukrani au neno ASANTE ni neno dogo sana kimtazamo ila ni neno kubwa na lenye thamani kubwa katika maisha.
Ni mala ngapi unashukuru kwa kile ulichofanyiwa?
Ni mala ngapi umepokea shukrani kutoka kwa mtu ulie mtendea jema?
Neno la shukrani uleta furaha,ujenga matumaini,ujenga ujasiri na kujiamini. Mfano, wewe ni dereva wa basi ukapakia abiria kutoka mji mmoja na kwenda mji wa pili. Kisha baada ya kufika abiria wote wakakulipa kisha wakashuka, ila kati ya hao abilia akakufuata mmoja na kukwambia,"asante sana dereva kwa kutufikisha sarama na ubarikiwe sana" ebu wewe kama dereva utajisikiaje? Ni furaha tele itakujaa,maana uyo mtu kaona dhamani yako na kujali kwako. Lakini pia ata wewe utamuona abilia huyo wa dhamani sana,maana ni mtu pekee katika wengi.
Hivyo basi tujifunze kutoa shukrani kwa kila mmoja wetu kwa kutendeana mema lakini ata yale mabaya hatuna budi kushukuru maana nayo yana nafasi yake ili tujifunze.
Pindi unapotoa shukrani unauengea moyo wako amani na utivu,kama jinsi upokeavyo shukrani na kujihisi furaha vivyo ivyo pindi utoapo. Ebu tuyafanye maisha kuwa na furaha kwa kumdhamini kila mmoja wetu,japo asante kwa kile kidogo anachokutendea. Ata mama nyumbani ujisikia amani pale ampapo mwanae kitu nakupokea Asante.
Basi chukua hiyo itakusaidia maishani.
Frank A. Ndyanabo
Whatsapp/imo +255785494456
www.fancompany.blogspot.com
frankalfred2814@gmail.com
Comments
Post a Comment