UMEWAHI KUJIULIZA JAMBO HILI?

UMEWAHI KUJIULIZA JAMBO HILI?

Unaweza ona kama upuuzi ila ndio ukweli. Umewahi kujiuliza kwa nini vijana wengi wanaohitimu vyuo kwa kozi mbalimbali akilizao uwaza kuajiliwa tu?

Mala nyingi watu wanao waza hivyo tunasema ni wenye akili mgando na akili zao zimefungwa.

Umewai kujiuliza kuwa mwenye hiyo ajila alikaa chini na kuwaza kisha akaja na wazo la kufungua hiyo kampuni ambayo wewe unawaza ukaajiliwe nayo.

Hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao unamjenga mtu kuajiriwa na sio kujiajili. Lakini kisiwe kisingizio, wewe unauwezo kujiongeza, usifikili ukibadili fikra zako utaonekana mjinga.

Ebu fikilia vijana wawili Juma na Bakari,wanaosoma  chuo kimoja cha biashara CBE. Hawa vijana wanasoma kozi moja na darasa moja na mwaka mmoja. Ila kila mmoja ana mawazo tofauti na mwenzake. Juma anawaza akimaliza chuo akaajiliwe kwenye makampuni mbalimbali uku akiwa na ndoto ya kulipwa ujira mkubwa na maisha mazuri.
Bakari nae anawaza baada ya kumaliza chuo akafungue kampuni kisha awaajili vijana wakuweza kumsaidia uzalishaji na kuwa mfanya biashara mkubwa.

Swali la kujiuliza ni, je Juma na Bakari wako sawa kifikra ikiwa wanasoma kozi moja na darasa moja?

Tafsiri yake ni kuwa Bakari yuko mbele ya Mwenzake kimawazo zaidi ya miaka 50 ila Juma yeye anawaza kesho.

Nataka nikwambie kijana wa leo hasa uliehitimu juzi, elimu yako husiiweke lehani, maana ukiamua kutafuta ajira ujue umeshindwa kuitumia elimu yako vizuri na badala yake umeamua kuikabidhi kwa watu waitumie vilivyo na kukutumikisha kwa kukupangia muda wa kuamka,kula,nguo za kuvaa,muda wa kupumzika uku ukiamuliwa kiwango cha kulipwa ujira kutokana na elimu yako.

AMKA SASA.

Frank A.Ndyanabo
0785494456
www.fancompany.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG