JE WEWE UNAWAZA KUFANIKIWA BAADA YA MUDA GANI?
Najua huu umekuwa ni ugonjwa kwa tulio wengi hasa pale tunapo anzisha miradi mbalimbali. Kwa kuwaza kufanikiwa kwa kutumia muda mfupi.
Jana katika semina yangu na wajasiriamali wa mwanza niliweza kulizungumzia hili swala kwa mapana zaidi, naamini wale walioshiliki kwa siku ya jana naamini walijifunza kitu.
Mafanikio hayaji kirahisi bali yanakuitaji uvumilivu na jitihada zaidi na hatupaswi kukata tamaa.
Jambo hilo analizungumzia tena hapa bilionea wa kiafrika bwana Dangote,mafanikio sio ndoto ya muda mfupi, ikiwa yeye imemchukua miaka 30 mpaka apo alipo,iweje wewe utake kufanikiwa kwa miezi kadhaa.
Futa mawazo hayo na anza kujituma na husikate tamaa.
Comments
Post a Comment