KWANINI HATUFANIKIWI KATIKA MIPANGO YETU AU KWANINI NDOTO NYINGI HAZITIMII?

KWANINI HATUFANIKIWI KATIKA MIPANGO YETU AU KWANINI NDOTO NYINGI HAZITIMII?

SEHEMU YA 1:

Mafanikio ni nini? Hili ni swali ambalo linaweza kuwa jepesi kwa baadhi ya watu ila niswali gumu sana kwetu wana damu. Lazima ujiulize nini maana ya mafanikio.

Mafanikio nikitendo cha kutimiza kile ulicho jipangia kutimiza kwa muda fulani. Neno mafanikio linajieleza kuwa ni kupiga atua kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Watu tumekuwa tukishindwa kuchanganua jambo hili kiundani na ndio maana tunalichukulia kawaida sana kwakuwa tumelizoea. Ila kiualisia ni neno moja zito na pana sana katika maisha ya kila siku na maisha ya mwandamu

Watu wengi tumekuwa tukishinda kutimiza yale tulio jiwekea/kufanikiwa kutokana na sababu mbalimbali zinazo tukabili hasa vijana wa leo.
Kutokana na jinsi nilivyokaa na kutafakari jambo hili nimegundua kuwa sababu hizi zimegawanyika katika makundi makuu mawili;
▶ Sababu za ndani ya nafsi ya mtu.
▶ Sababu za nje ya nafsi ya mtu.

1⃣. Sababu za ndani.
Hizi ni sababu  ambazo zimeweza angamiza ndoto za watu wengi maana ni sumu ya mafanikio ya mwanadamu kuliko kitu chochote.

Nimejaribu kuwaza na kuwazua lakini sikupata majibu papo kwa papo, ila baada ya kuamua kujiuliza kwa muda mrefu ndio nikaja na majibu ya swali hilo, ambalo limenisukuma mpaka kuamua kuandika makala hii ili niweze kukuelimisha wewe kijana na mtanzania mwenzangu.

Sababu hizi za ndani ukianza kuzichanganua unaweza kumaliza ata mwaka mzima ukiandika. Sasa basi ebu tuzitazame sababu hizo za ndani zinazo kwamisha ndoto za watu walio wengi.

1. Kutofanyia kazi mawazo yetu.

Watu wengi tumekuwa na mawazo mengi sana juu ya maisha yetu ya kimaendeleo,ila tumekuwa tukikumbwa na mdudu huyu anaetutafuna kila kukuchapo. Ninachotaka nikwambie ni kuwa ukitaka fanikiwa katika  ulimwengu wa leo fanyia kazi wazo lako ulilo nalo sasa, husiwaze kisha ukaliacha kwenye ubongo.

Ebu jiulize unapo umwa njaa kuna mtu ukufuata na kukwambia nenda ukale? Kwanini usihisi njaa kisha mtu mwingine aje akwambie nenda ukale. Basi kwakuwa hakuna wakufahamu kile kilichoko akilini mwako ndio maana una nyanyuka na kukitafuta chakula kilipo na kula.

Hivyo basi pindi upatapo wazo la kimaendeleo usilikalie bali liweke katika vitendo. Ndio maana kuna msemo kuwa matajiri wengi wako makaburini, maana yake nn? Maana yake ni kuwa wengi wanakufa na mawazo mazuri.

2. Kutokuushughulisha ubongo.

Watu tulio wengi bongo zetu tumezifunga na makufuri ya solex, kiasi kwamba haturuhusu kuyafungua ili vitu vingine viweze kuingia.

Kuna msemo mmoja unasema, ili upate maji ya kunywa lazima glasi yako iwe tupu. Mwanzoni niliuchukulia kawaida sana msemo huu, ila sasa ndio naona maana yake

Tumekuwa hatutaki kufungua bongo zetu ili ziweze kuingiza mawazo na mbinu mpya za kutuwezesha kupiga atua mbele.

Sasa basi ukitaka ufanikiwe ktk malengo yako lazima ukubali kuishughulisha akili yako kikamilifu.

Unaishughulishaje ili ufanikiwe?

Jisomee vitabu na makal mbalimbali, sikiliza audio na tizama video mbalimbali za watu waliofanikiwa na mbinu mbalimbali za kimaendekeo. Lakini pia udhulia semina na mikutano mbalimbali ya kimaendeleo ili uweze kujifunza wenzako wanafanya nn ili kupiga atua za kimaendeleo.

3. Tumejaa woga ndani ya mioyo yetu.

Watu wengi hasa vijana tumejaza woga ndani yetu ndio maana wengi tunashindwa kutekeleza mipango yetu kuwa na woga.

Nawoga wa walio wengi ni kuofia kuibiwa,kutapeliwa,kuofia kupata hasara.

4. Kutokujiamini.

Watu wengi hatujiamini na kile tukifanyacho.

Hili ni tatizo kubwa sana kwa walio wengi,mala nyingi hatujiamini ndio maana watu ndoto zao zinashindwa kutimia kwa sababu hii

Utakuta kijana au mtu yeyote ana mawazo mazuri ya kimaendeleo ila anazongwa na mdudu kutokujiamini. Kutokujiamini huku kunajengwa na hofu inayoweza kupelekea kuwaza kuchekwa.

Ukitaka ufanikiwe kimaisha jijengee ujasiri ndani yako, jiamini kuwa unaweza kufika pale ulipopanga kufika bila shida yoyote.

Amini kuwa kuwa unauwezo kufanya lolote na likakubalika, amini kuwa unauwezo wa kusimama ata mbele ya watu wasio pungua 1000 na ukalitetea wazo lako

Amimi kuwa wewe ni wewe na hakuna mwingine.

5. Kutokuzitambua ndoto zetu.

Hili sasa ndio tatizo, kama ni magonjwa tungesema ni kansa au ukimwi

Watu tulio wengi hatuzijui ndoto zetu, ata wale wanao zitambua hawajaziandika ivyo ni sawa na hakuna

Utakuta mtu mwanzo wa mwaka anakwambia mimi mwaka huu nataka ninunue Gari, ila kabla mwaka kuisha ana nunua pikipiki, ukimuuliza anakwambia nimeamua nianze na hii. Sasa jiulize je iyo pikpik ilikuwa katika malengo yake?

Pia katika upande huu watu hatuko makini na ndoto zetu, yani ni za kubadilikabadilika bila mpangilio pasipo kutekelezwa

Ukitaka ufanikiwe zitambue ndoto zako, kisha zieshimu. Utaona matunda yake

6. Tumejawa na tamaa.

Waswahili usema,"tamaa mbele........mauti nyuma" hii kauli inamaana kubwa sana kuliko jinsi ufikiliavyo

Watu wengi utamani vitu tusivyo na uwezo navyo. Apa naomba tuelewane vizuri katika hili. Maana unaweza hisi nakuchanganya maana wakati mwingine lazima tutamani ili tupate hamasa ya kufikia katika mafanikio.

Ninachokimaanisha apa ni kuwa watu tunakuwa washika mbili, "mshika mbili moja umponyoka" utakuta mtu anaanzisha project kabla haijafanikiwa kaishaanzisha nyingine na hiyo kabla haijaisha kaanzisha nyingine

Hatusemi kuwa projects nyingi ni kosa lahasha bali ukitaka ufanikiwe fanikisha projet moja kabla ya nyingine.

7. Kupangilia mambo yako.

Tunashindwa kufanikiwa kwakuwa hatuna mipangilio katika mambo yetu. Kwa lugha nyingine tunasema, hatuko smart ktk mambo yetu

Umakini ktk mambo yetu ya kimaendeleo ni muhimu sana.

Ebu jiwekee utaratibu wakujipangia ratiba yako ya kila siku ili usiingize mambo yasistahili katika mambo yako

Ratiba ya siku itakusaidia kujua kipi kifanyike na wakati gani. Sasa apo wengine watakwambia we unataka kutufanya tuwe kama wanafunzi

Si hivyo, hivi ulisha wai kujiuliza kwanini diary nyingi zimeandaliwa kwa mfumo wa siku,wiki,mwezi na mwaka uku ikiambatana na tarehe usika.

Zile hazikuandaliwa kama mapambo, bali lengohasa ni kukuwezesha kupangilia mambo yako ya kila siku. Ili usichanganye mambo, yani jambo la wiki ijayo ulifanye leo na jambo la leo ulifanye mwezi ujao

Ukifanyabmambo yako smart ata mafanikio yatakujia smart. Smartness brings smart life.

8. Kutokuwa tiali kusaidia watu.

Hili pia ni tatizo kwetu, wengi wetu hatuko tiali kujitoa kwaajili ya watu wengine.

Hivi ulisha wai kujiuliza hivi kama wazazi wako na jamii yako kama isingejitoa kukujali wewe pindi ukiwa mdogo ungekuwa apo ulipo?

Sasa kwanini na wewe usijitoe kwaajili ya watu wengine?

Ipende jamii inayokuzunguka, ndugu jamaa na marafiki.

Tambua kuwa kwa kufanya ivyo utajijengea dhamani katka jamii hiyo na kuikuza kimaendeleo

Watu tunawaza kuwa kumjali mtu au kumsaidia mtu ni mpaka kuwa na pesa,la hasha. Kumjali mtu ata kwa ushauli au kumfariji kwa maneno ni msaada tosha kuliko mali au pesa.

9. Tunajikweza au tunajivika ushindi kabla ya mashindano.

Mala nyingi ukiwa katika mashindano ya mpila wa miguu kisha ukafanikiwa kumfunga mshindani wako magori matatu kipindi cha kwanza kisha ukarelux kwa kuhisi umeisha shinda,wakati bado kuna dakika zingine 45 basi unajidanganya.

Utakuta mtu kaanzisha mradi fulani basi pindi matunda yanapoanza kuchomoza basi muhusika ujiona kuwa sasa maisha yamemnyookea,nakujisahau kuwa bado safari ndefu sana mbele yake.
Ukitaka kufanikiwa basi epuka tabia hii na jenga tabia ya kutoridhika, pale unapoona mafanikio yanaanza kuja basi ndio ongeza speed kama vile ndio unaanza mapambano upya

10. Changamkia fursa zinazojitokeza.

Katika maisha ya leo yamejaa fursa zakutosha kiasi kwamba unaweza shangaa ata jambo ambalo unahisi haliwezekani linawezekana

Kunawakati mwingine unaweza kukutana na fursa ya biashara mpaka ukabaki unashangaa na kuiacha ikupite, alafu ukisikia fulani kafanikiwa kutikana na fursa hile basi unaanza kutoa macho.

Hakuna kitu kibaya kama majuto katika maisha.

Usije ukadhubutu kuzalau fursa yoyote, maana hatujui kesho kutapambazukaje.

Hapo ndio mwisho wa sehemu yetu ya kwanza. Husikose mwendelezo wa makala hii katika sehemu ya pili.

By,
Frank Ndyanabo
0785494456

Comments

  1. Kaka makala makini sana hii nasubir mwendelezo na kiukwel umenifundisha viti vizuri sana hapo kaka be blessed

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG