KWANINI HATUFANIKIWI KATIKA MIPANGO YETU AU KWA NINI NDOTO NYINGI HAZITIMII.

KWANINI HATUFANIKIWI KATIKA MIPANGO YETU AU KWA NINI  NDOTO NYINGI HAZITIMII.

SEHEMU YA 2:

Katika somo lililopita tuliweza kuziangazia sababu mbalimbali zinazo sababisha watu wengi kushindwa kuzitimiza ndoto zao. Tuliweza kuona kuwa kuna sababu kuu mbili;
▶ Sababu za ndani ya nafsi ya mtu
▶ Sababu za nje ya nafsi ya mtu.

Natuliweza kuzichambua kwa kina sababu zilizo ndani ya mtu. Na leo tutaangalia kiundani sababu ya pili, ya sababu zilizo nje ya nafsi ya mtu.

2⃣ Sababu za nje ya nafsi ya Mtu.

Hizi ni sababu ambazo zimeweza angamiza ndoto za watu wengi maana ni sumu ya mafanikio ya mwanadamu kuliko kitu chochote.

Ebu tuziangalie sababu hizo maana zipo za aina mbali mbali kulingana na mazingira na wakati.

1. Kuofia kuchekwa.

Kuna baadhi ya watu uzionea haya ndoto zao kwa watu wengine. Mtu unakuta anawazo zuri tu ila kwakuwa anaogopa jamii inayomzunguka kumcheka basi ukuta wazo lake linatokomea na kufa. Ivyo basi ukitaka ufanikiwe upaswi kujijengea wazo hilo,bali fanya wewe kama wewe.

2. Kukosa mtaji.

Huu sasa ni wimbo wataifa hasa kwa vijana tulio wengi. Hii inatokana na wazo lakuwa wengi kuwa na fikra potofu kuwa ili uanze biashara lazima uanze na mamilioni ya pesa ndio uweze kuanzisha mradi. Nataka nikupe suluhu moja mtaji mkubwa wa mradi wako ni WAZO LAKO. ukisha pata wazo huo ndio mtaji mkubwa na usifikilie kuanza na milioni kumi au miamoja. Tambua kuwa ata elfu hamsini au elfu ishirini inaweza kuanza biashara.

Hivi unafahamu madhara ya kuanza biashara na mtaji mkubwa?

Fikilia leo hii uanze biashara na mtaji wa milioni 10 niambie apo utakuwa unatarajia milioni ngapi kila mwezi kama faida? Bila shaka unawaza kupata milioni tano au  tatu kama faida kwa mwezi. Ikitokea ukapata laki tano au tatu utaona hii biashara kichaa na hautakaa muda mrefu utaifunga.

Sasa ebu mtazame mtu alianza biashara ndogo kwa mtaji wa laki moja au elfu hamsini akipata faida ya elfu 30'000/= au 20'000/= basi atafarijika maana ata mtaji wenyewe mdogo ivyo haumpi presha kuwa.

Hii inamaana gani? Ni kuwa unapo anza biashara kwa mtaji mkubwa ata akili yako inategemea mapato makubwa sana ivyo ukiteleza kidogo tu biashara inakufa na  mtaji kidogo hana presha na ni rahisi kukuza biashara yake.

3. Kutokutengeneza mazingira ya kibiashara.

Wajasiliamali waliowengi wanafanya biashara zao ilimradi tu, hawako tiali kuwa smart katika biashara zao. Lazima uwe na mpangilio mzuri na kujenga mazingira mazuri ya kuwavutia wateja wao. Hii ikiwa na kauli nzuri, kuakikisha uduma inamfikia mteja kwa wakati muafaka, kuwa na vitendeakazi vizuri pamoja na usafi kwa ujumla.
Haya ni mambo muhimu san na usipo yatimiza ndoto zako zitaishia kwenye makaratasi.

4. Kutokujua jinsi ya kulisoma soko kabla ya kuanza biashara au mradi fulani.

Hili ni tatizo kubwa mno na limekuwa likiwakwamisha walio wengi.  Hii ni pale mtu anapoanzisha mradi bila kujua uitaji wa watu wale katika eneo husika. Ukifanya ivyo bila kufanya tafiti ktk mazingira hayo utaishia kupoteza ndoto zako na kupoteza muda wako bure.

5. Kuhofia upinzani katika biashara.

Katika ulimwengu wa leo upinzani hauzuiliki ata kidogo. Hivyo hupaswi kuhofia bali unachopaswa kufanya ni wewe kuwa mbunifu ktk  biashara yako au mradi wako,akikisha unafanya tofauti na wenzako ataka kama mnafanya kitu cha aina moja ukiongeza ubora basi utaliteka soko,sio unashindwa kufanya kile ulichopanga kwa kuwaogopa wapinzani wako.

6. Kuogopa hasara katika biashara.

Hili ni swala lisiloepukika. Lazima utambue kuwa katika biashara uwa kuna mambo matatu
👉Faida.
👉Hasara.
👉 Faida sifuri.
Katika biasha la ichokitu hakiepukiki ivyo ukijijengea wazo la kuogopa ivyovitu basi huwezi songa mbele.

7. Kukatishwa tamaa.

Biashara zilizo nyingi lazima ukutane na changamoto za kukataliwa ivyo waliowengi uhofia icho kitu. Nataka nikwambie kuwa harakati za kutimiza ndoto ilo jambo lazima ujue kuwa ni la kawaida ivyo lazima ulitegemee maana sio wote wanaokutakia mema. Ivyo jipange kukabiliana nalo kwa kuwa na msimamo wa biashara yako.

8. Kupolomoka kwa uchumi.

Hili uhusisha maswala ya masoko na kushuka kwa dhamani ya pesa katika soko la kimataifa.

Biashara nyingi utegemea sana soko kuwa zuri ikiambatana na pesa kuwa na dhamani dhidi ya pesa ya kigeni ivyo kama ikitokea ilo swala hupaswi kukata tamaa bali vumilia na uzidi kusonga mbele.

9. Kurudisha shukrani katika jamii.

Watu wengi tunapofanya biashara tunajisahau kuwa tumezungukwa na watu wanaoishi katika mazingira magumu, ivyo ni wajibu wetu kutoa sadaka kwa kuwasaidia watu hao kwa kuyagusa maisha yao. Hili utaona niswala la ajabu ila ni swala muhimu sana katika kuzielekea ndoto zako,amini usiamini ukitaka kuona muujiza wa mafanikio jaribu kutenga fungu fulani kwaajili ya jamii iyo kisha utaniambia matokeo yake. Usione wakina Mengi wanatoa misaada ukafikili wamekosa matumizi ya hizo pesa. Kunausemi kuwa, ukitaka kupokea basi nawe toa.

10. Mtangulize Mungu katika shughuli zako zote.

Hili ndio swala la msingi kuliko ayo yote tuliojadili toka mwanzo. Unaweza kujiuliza kwanini nimeiweka point hii mwishoni,ni kwakuwa nataka nikuonyeshe ukuu wa Mungu kuwa ata ayoyote nilioandika ni kutokana na uwezo wake maana naamini bila yeye alie juu nisingeweza kuyafikilia ayo yote.

Hivyo basi ili uzitimize ndoto zako lazima umtangulize, utaona neema ya mafanikio itakavyo kumiminikia.

Nashukuru sana kwa kuwa nami kwa makala zote mbili ya kwanza na hii. Na apa ndio tamati ya somo langu la mafanikio. Nina ujumbe mmoja kwako;

"Badili fikra, timiza ndoto zako"

By,
Frank A. Ndyanabo
0785 494 456

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG