UKUBWA WA ELIMU YAKO SIO KIGEZO CHA WEWE KUFANIKIWA.
UKUBWA WA ELIMU YAKO SIO KIGEZO CHA WEWE KUFANIKIWA.
Tumekuwa tukiwaza kuwa ukiwa na elimu kubwa kama kuanzia degree,masters,PhD au Profesor basi ndio unaweza fanikiwa katika maisha.
Nahili limekuwa likijengeka siku adi siku miongoni mwetu. Na nikutokana na uridhi wa fikra tuliopata kutoka kwa walio tutangulia.
Utakuta ata mzazi anamsisitizia mwanae kuwa ukitaka kuishi maisha mazuri lazima usome sana. Sipingani na hilo,ila chakuzingatia apa ni kuwa kusoma sana au kuwa na elimu kubwa sio kigezo cha mtu kufanikiwa kimaisha.
Kama huna mtazamo chanya maishani mwako basi ata usome mpaka vyuo vyote duniani bado utaendelea kuwa na maisha duni.
Nataka nikwambie ukiwa na mtazamo chanya wakujiletea mafanikio ata uwe hujaenda shule au umeishia darasa la saba.
Hujawai kujiuliza kwanini watu watu waliosoma sana wanamaisha ya kawaida ukilinganisha na walioishia shule za chini? Si unawaona wamekuzunguka? Ebu mtazame tajiri mkubwa apo jirani yako au mtaani kwako kaishia darasa la ngapi?
Je mnalingana kielimu au unamzidi?
Kitu cha msingi apa nikuwa na mtazamo imara mbele ya majukumu yako,pasipo kuangalia ni mambo mangapi unakumbana nayo na unauwezo gani kimtazamo katika kukabiliana nayo.
Pambana sasa husifikili kwakuwa hunaelimu basi maisha mazuri ni kwa wenye elimu, utakuwa unajidanganya ndugu yangu.
Matajiri wakubwa duniani hawana elimu za kutisha,na ndio wanao ongoza kwa kuajili watu wenye elimu zao,na ndio wanao ongoza uchumi wa dunia na nchi zake na watu wanaongoza kwa kuwa na maisha duni ni watu wenye elimu kubwa duniani,na huo ndio ukweli.
Niwakati wako sasa,kujipambanua kimtazamo na kuchukua atua kwaajili ya maisha yako.
By,
Frank Ndyanabo
0785 494 456
www.fancompany.blogspot.com
Comments
Post a Comment