KIPI UNAKIHUSUDU?

KIPI UNAKIHUSUDU?

Katika maisha kila mtu anakitu fulani ambacho anatamani kuwanacho au angependa kufikia mahali fulani.

Mahitaji ayo utofautiana kati ya mtu na mtu, na pia utofautiana kulingana na mazingira ya mtu husika.

Sasa ebu jiulize, unahusudu nini katika maisha yako?  Mfano mimi Frank Ndyanabo, natamani kuwa mfanyabiashara mkubwa kimataifa na natamani kuwa mmiliki wa makampuni makubwa duniani.

Je wewe unatamani kuwa nani? Mwanamziki mkubwa, mfanya biashara kama mimi, unataka kuwa na salon nzuri, unatamani kuwa na mke au mume mzuri, unatamani kuwa na gari nzuri, nyumba nzuri, kumiliki kiwanda, kumiliki hotel, kupata elimu ya juu, kuwa na duka kubwa, kumiliki kalakana ya fenicha, au nini?

Kwa kuwa mambo ni mengi, Je unafikili kile unachokihusudu ni rahisi kukipata? Ukweli ni kuwa sio rahisi na ndio maana watu wengi tumekuwa tukiishia njiani katika safari zetu maana kila tukianza safari uhisi kuwa tunakoenda ni karibu na mwisho wa siku tunachoka na kuhailisha maana mwendo uwa ni mrefu.

Sasa leo nataka nikupe siri ya kutimiza kile unachokitamani au unacho kihusudu.  Ukisha tambua kuwa unapenda kufanikisha jambo fulani ambalo ndio ndoto yako, unapaswa kuipenda ndoto yako na kuzipenda njia unazo zipitia, 
"To be successful, the first thing to do is to fall in love with your work "
Maneno hayo ni mazito sana, huwezi kufanikiwa katika ndoto yako kama hukipendi kile unachokifanya. 

Kama wewe unapenda kuwa mwalimu bora na mzuri, unapaswa kwanza kuipenda kazi yako, kisha chukua muda wa kujifunza kila siku kwa kusoma vitabu na majarida mbalimbali yahusuyo maswala ya elimu bora.
Na kama wewe ungependa kuwa mfanya biashara mkubwa na bora, basi jambo la kwanza ni kuipenda ndoto yako hiyo na kwa mapenzi yako hayo chukua jukumu la kujifunza mbinu mbalimbali za kukuza biashara yako kupitia kusoma vitabu, kuudhulia matamasha na makongamano mbalimbali ya biashara, pia jifunze kutoka kwa marafiki au ndugu waliofanikiwa.

Ukiipenda ndoto yako basi kwa moyo mmoja utawajibika katika kuakikisha inatimia, ebu kuanzia leo ipende kazi yako, ipende biashara yako, utaona matunda yake.

Pia jambo lingine la kuzingatia apa, na jambo hili limeniongoza sana na mimi Frank Ndyanabo, hili ni kutokuwa na mawazo ya kufanikiwa kwa muda mfupi, hiki kimekuwa ni kikwazo kikubwa maana watu hawafiki safari zao kutokana na kutaka kufanikiwa kwa muda mfupi, mimi kufikia apa nilipo imenichukua mwaka mzima na zaidi sasa, na bado naendelea kufanya kile kinachozidi kuboresha biashara zangu, kila siku najifunza, naboresha mbinu zangu, mpaka pale nitakapo kuwa nimefanikiwa, wataalamu wanakwambia ili ufanikiwe unapaswa uchukue walau miaka kuanzia kumi uku ukifanya kitu kile kile. Ebu waone matajiri wakubwa kama Dangote, Mengi, Barlesa, Muhamed Dewj(MO). MO anakwambia imemchukua zaidi ya miaka 30 mpaka kufikia apo alipo na mpaka Sasa ndio tajiri mkubwa na anayeongoza kwa kutoa ajira kwa kuliko mtu yeyote apa Tanzania kwa taasisi binafsi, Maana ameweza kuajili watu zaidi ya 25000 na ndoto yake ni kuajili watu zaidi ya laki tano.  Sasa unafikili ni kazi rahisi kama haipendi kazi yake na ndoto yake.

Kuanzia leo husudu ndoto yako na ifanye kwa moyo mmoja, hakika utabarikiwa, na kwa kila ulifanyalo kumbuka kumtanguliza Mungu wa mbinguni akika utafanikiwa.  Nikutakie siku njema.

By, Frank A Ndyanabo
0785494456

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG