KWANINI BIASHARA YAKO HAIKUI
KWANINI BIASHARA YAKO HAIKUI?
Dunia hii imejaa biashara za aina nyingi sana kiasi kwamba watu tumeamua kujichagulia kile tunachoona tunakimudu.
Kwasababu hiyo tumekuwa na mwanya wa kuamaama ovyo pale tunapogundua biashara fulani hailipi kama tulivyo tarajia.
Sasa jiulize ukiamua kila biashara inayokushinda unaiacha utaacha biashara ngapi apa duniani?
Nakumbuka kipindi cha nyuma Ulikuwa ukiona biashara fulani hailipi basi unaamua kubadili mazingira tu nakwenda kuweka biashara iyo iyo sehemu nyingine. Ila mwisho wa siku inakufa.
Ila ulimwengu wa leo sio kama zamani, sasaivi unaweza fanya biashara ukiwa sehemu yoyote bila Kujali mazingira.
Tambua kuwa hakuna biashara mbaya apa duniani kila biashara inaweza kukupeleka katika ndoto yako, sema shida inayotukabili hatujui mbinu za kuifanya iweze kukua na kukutimizia ndoto.
Siku moja nikiwa mtaani nikikutana na vijana fulani ambao nilisoma nao katika chuo cha SAUT miaka hiyo,basi katika mazungumzo wakanieleza changamoto wanazo kutaka nazo katika ajila mpaka wanatamani kuamia katika ajila binafsi.
Ila rafiki yangu mmoja ambae nae amejaribu kuanzisha biashara yake ya ufugaji wa kuku nae akaniambia kuwa katika biashara nako hakufai maana kila siku ni mawazo maana asara huzikomi ila anaendelea nayo biashara yake kwa kulazimisha tu ili mladi apate pesa ya kula ila hana ndoto ya kutimiza kutokana na biashara hiyo.
Kitu ambacho nilikigundua kwa rafiki zangu hawa wawili wa SAUT ni kuwa kila mmoja hajui jinsi ya kukabiliana na kile kilicho mbele yake, na kwa taswira hiyo basi haipo siku watafanikiwa bali kila mmoja anaijutia nafsi yake.
Ninachotaka ukifahamu ni kuwa biashara katika ulimwengu huu ni rahisi mno kuliko unavyo fikilia, tatizo la rafiki zangu wa SAUT wanatumia nguvu nyingi sana katika kuendesha biashara zao,wakati kuna watu wanafanya biashara iyo iyo kama yao na wamekuwa mamilionea
Kwa sababu hiyo ndio maana nikaamua kuanza kutoa elimu juu ya maswala haya ili watu wajikwamue kiuchumi na wao watimize ndoto za umilionea kama wengine.
Napenda kila mtu afanikiwe kupitia njia nilizopitia mimi mpaka kufikia apa nilipo.
Basi ungana na mimi katika project hii ya NYUMBANI BUSINESS PLAN (NBP) Ili uweze kuvuna matunda ndani ya ulimwengu huu.
Hakuna njia ngumu katika biashara kama kumfanya mteja aweze kununua bidhaa zako ila ukizifahamu basi ni kazi nyepesi sana maana watu watakuja wenyewe tu.
Unasubili nini sasa shiliki sasa ili tutembee pamoja, Timiza ndoto zako kwa kujifunza kwa walio kutangulia.
Comments
Post a Comment