TAFAKARI YA LEO, UMEDHIBITISHA?

TAFAKARI YA LEO; UMEDHIBITISHA?

Mtoto mdogo, ambaye ndio anakua kama akikaa kwenye kiti vibaya na hivyo akaanguka, huwa anahusisha kiti na kuanguka kwake. Hivyo anaweza kukiogopa kiti moja kwa moja, kwa kukihusisha na maumivu aliyoyapata.Ila ukweli ni kwamba, hatari sio kiti, hatari ni jinsi alivyokuwa amekaa kwenye kiti kile. Labda alikaa kwenye kona sana ikawa rahisi sana kuanguka.

  Tabia hii tumekwenda nayo mpaka ukubwani, tunapokutana na hatari yoyote, au maumivu yoyote, tunakimbilia kukwepa kabisa hali ile. Bila ya kukaa na kuhoji ni kipi hasa ambacho hakikwenda vizuri.
Umeingia kwenye biashara na ukapata hasara, halafu unaishia kusema biashara mbaya sana, sifanyi tena. Lakini huo sio ukweli, ukweli ni kwamba kuna mambo uliyofanya kwenye biashara ambayo yalisababisha upate hasara. Labda hukuwa makini, labda hukuajiri watu waaminifu, labda hukuweka ubora na mengine mengi.

  Au kwenye mahusiano, unaingia katika mgogoro na kujikubalia mwenyewe kwamba mahusiano ni hatari kabisa, hayafai. Kumbe kuna mambo ambayo ulifanya, au hukuwa makini na yamepelekea wewe kuingia kwenye matatizo.
Muhimu ni kudhibitisha ni kipi kweli kimepelekea wewe kuishia kwenye hali ambayo hukuitaka, na baada ya hapo ndio uchukue hatua.

Siku ya leo tafakari ni mara ngapi umekuwa unakwepa mambo kwa ujumla kwa sababu ya changamoto ulizokutana nayo awali. Tafakari ni kwa  kiasi gani umekosa fursa nzuri kwa kuepuka moja kwa moja.
Amua leo kuhakikisha uhukumu jambo lolote mpaka udhibitishe ukweli uko wapi na umehusikaje nao.
NAKUTAKIA SIKU NJEMA SANA RAFIKI.

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG