THAMINI KILE KILICHO MKONONI MWAKO.
THAMINI KILE KILICHO MKONONI MWAKO.
Nimekuwa nikishangaa wajasiliamali wenzangu ambao mala zote utamani mambo makubwa uku wakidharau yale madogo.
Mtu utakuta anakwambia kuwa anatamani kumiliki kiwanda ila cha kushangaa anadharau duka dogo alilokuwa nalo.
Wakati mimi naanza ujasiliamali wangu kitu cha msingi nilichokiweka akilini Mwangu ni kuwa sikuzote kama nataka kuwa mfanya biashara mkubwa lazima niipende hii ndogo nilionayo, ndio maana kuna usemi kuwa 1000 uanza na 1.
Hali iyo imekuwa ikiniongoza mpaka apa nilipofikia siri ni kukithamini kile nilicho nacho, ukikidharau basi ata wenzako watakidharau.
Najua una ndoto kubwa ila tambua ndoto kubwa utokana na ndoto ndogo.
Kuna watu mwanzo walikuwa wakizani nacheza vile na mpaka Sasa kuna ambao hawaamini kama ni mimi, ila nataka nikwambie ndugu yangu Ukiweza kujua jinsi ya kukipenda na kukiboresha kile ulicho nacho basi utapata mafanikio makubwa.
Kumbuka kile unachotamani kuwa nacho kuna watu wamekithamini na kukijali ndio maana kina kuvutia.
Anza sasa kuipenda biashara yako ata kama ni ndogo kiasi gani ipende tu ipo siku utashangaa.
Matokeo makubwa utokana na juhudi, uwezi kuwekea juhudi kitu kama hukipendi, mfano wale akina mama wanaoshinda barabarani wakiwa na beseni la ndizi, unafikili wangekuwa hawapedi biashara yao ungewakuta?
Leo hii biashara yako unaweza ukahisi ina taswira mbaya kwa watu na unafanya kwakuwa huna jinsi, ndugu yangu ata wakina Barlesa, Muhamed, Mengi na wengine walianzia uko ila kwakuwa waliipenda na kuithamini biashara yao ndio maana leo hii kila mtu anawajua mpaka mtoto mdogo anawafahamu.
Hujachelewa anza leo kuipenda biashara yako, kukipenda chochote kile unachokifanya utaona matunda yake.
Usiwe kama mtu asiye na busara anayetamani vya jirani nakudharau vya nyumbani kwake. Anza sasa.
Frank A Ndyanabo
0785494456
Comments
Post a Comment