TOKA KIFUNGONI
TOKA KIFUNGONI.
Tuliowengi tuko gerezani ila hatujijui kama tuko gerezani.
Na gerezani tulilopo limefungwa makufuli makubwa na yamelindwa na kwa mitutu na makombola.
Kwa sababu hiyo ni ngumu sana kuchomoka umo au kutoloka. Kwa taarifa yako makombola na makufuli ayo alieyaweka ni wewe mwenyewe.
Ebu yaondoe haraka sana, inashangaza kuona mtu unajiwekea ulinzi mkali wa kushindwa kusonga mbele.
Wanadamu wengi akili zetu ziko gerezani na hatutaki kuzitoa uko ili tuwe huru.
Nakumbuka mwaka mmoja uliopita nikiwa maeneo ya Maeneo ya kimara Dar es salaam nilikuwa kwenye mgahawa mmoja nikiwa na rafiki yangu Benson Kailuki. Basi tukiwa tunapanga mikakati ya kuanzisha biashara yetu binafsi na kuacha na mbio za ajira.
Tuliweza kukumbana na changamoto ya kitu gani tuanzishe ili kuweza kutuingizia kipato kwa haraka. Huwezi amini ilituchukua kama masaa manne kuweza kupata wazo la biashara.
Toka siku iyo nikagundua kumbe akilizetu tumeziteka wenyewe na kuzifunga kwa minyororo mizito.
Ndio maana leo hii ukiulizwa ghafla apo ulipo ni biashara gani unaweza kuanzisha utashindwa kutoa jibu maana akili umeifunga kwa makufuli mazito.
Au ikitokea ukapewa shilingi laki moja apo ukaambiwa anza biashara utashindwa maana akili yako umeifunga kwa minyororo kama mimi Frank nilivyo kuwa nimeifunga bila kujua.
Katika maisha nimejifunza mambo mengi maana sikuizi sio Frank wa miaka mitatu nyuma, na hii ni kwakuwa nimeamua kuitoa akili yangu kifungoni nakuweza kuzipambanua ndoto zangu.
Kuna watu walioniona miaka mitatu nyuma kwa sasa hawaamini maana tushatofautiana kimtazamo.
Sasa na wewe bado unaitaji kuendelea kubaki katika mtazamo ule ule kama niliokuwa nao mimi kipindi hicho ambapo niliwaza kuwa maisha yangu hayawezi kusonga mbele bila ajira, niliwaza kuwa biashara kuianza lazima niwe na mtaji mkubwa wa kuanzia milioni tano na kuendelea, niliwaza kuwa biashara nikianzisha basi nitapata hasara maana sikuwa mzoefu.
Mawazo hayo yalitokana na minyororo niliokuwa nimeiweka katika akili yangu, Je na wewe unawaza kama mimi au unatamani kutoka ila hujui jinsi ya kutoka?
Ebu jiulize umeishakutana na fursa ngapi ukazipuuza au ni biashara ngapi umewahi kuzifanya ila zikafa kabla ya kufikia lengo lako?
Mambo mengi tunayo yapanga na kufanya yanashindwa kutumia kutokana na akili zetu kuziruhusu kuendelea kubaki gerezani uku sisi tukiwa mataan tunazurura tu na kulalamika maisha magumu.
Akili ndio injini ya maisha yako ukiitumia vizuri basi maisha yako yatakunyookea, kwakuwa utafanya maamuzi ya busara juu ya maisha yako na kuweka mikakati madhubuti kwaajili ya kutimiza ndoto zako.
Toa akili yako kifungoni.
"Do not let what you cannot do interfere with what you can do "
Comments
Post a Comment