UNAUJUA MGUU WAKO WA KUSHOTO?
Kila mtu aliyeko duniani,amepewa na Mungu kitu cha kipekee ili aweze kufanikiwa katika mazingira aliyopo,hakuna mtu asiye na kitu cha kipekee.Inawezekana haukijui ila hiyo haimaanishi hauna.Ukichunguza kwa kila aliyefanikiwa utagundua kuwa waligundua uwezo,kipaji ama nguvu ya kipekee waliyonayo wakaitumia kikamilifu kubadilisha maisha yao.
Jana kabla ya kutoa tuzo ya Mchezaji bora wa dunia(Ballon d'Or) Christiano Ronaldo na Lionel Messi Kila mmoja aliulizwa ni kitu kipi anacho mwenzake na yeye anagetamani kuwa nacho.Nilipenda sana jibu la Ronaldo,alisema.."Mguu wa kushoto wa Messi"Huo ndio Ukweli kila beki duniani anajua athari za mguu huu na ukweli ni kuwa mguu huu ndio umekuwa chachu ya mafanikio ya Messi katika uchezaji.
Habari njema ni kuwa kila mtu ana "Mguu wake wa Kushoto"{Uwezo maalumu} ambao ukiugundua na kuanza kuutumia utashangaa matokeo yake.
WANAOFANIKIWA SANA SI WALE WANAOFANYA MAMBO MENGI;BALI WALE WALIOGUNDUA NGUVU YAO NA WAKAAMUA KUWEKEZA KATIKA ENEO HILO.
Leo Jiulize na ujijibu kwa uaminifu;Ni kitu gani kwako sawa na mguu wa kushoto wa Messi?Mara uttakapogundua siri hii dunia nayo itakujua.
DISCOVERING OF YOUR UNIQUE GIFT IS THE BEGINNING OF YOUR GREATNESS.
Comments
Post a Comment