USIMDHARAU USIYE MJUA.

Siku moja nchini marekani mzungu mmoja
aliingia kwenye mgahawa na kukuta kuna kijana
mmoja mweusi amekaa kwenye Kona ya
mgahawa huo.
Akaingia ndani na kumwagiza muhudumu awape
watu wote chakula kasoro yule kijana mweusi na
pesa atatoa yeye.
Muhudumu akagawa chakula kwa watu wote
kasoro yule mweusi na kisha akaenda kwa yule
mzungu kuchukua malipo.
Yule mzungu akalipa pesa huku akimtizama yule
mweusi.
Yule akamtizama kwa sura ya bashasha na
tabasamu kisha akamwambia Yule mzungu
asante.
Yule mzungu akachukia inakuwaje yule mweusi
anafurahi baadala ya kukasirika..!
Akamuita muhudumu na kumwambia wape
vinywaji BURE Mimi ndio nitalipa kasoro yule
mweusi.
Muhudumu akawapa vinywaji wote kasoro yule
mweusi.
Yule jamaa akalipa pesa ya vinywaji huku
akimtizama yule kijana mweusi,cha ajabu yule
kijana mweusi akaonyesha tabasamu kubwa zaidi
kuliko mwanzo na kusema ahsante sana....
Yule mzungu akamfuata muhudumu na kumuuliza
vipi huyu kijana mweusi ni mwendawazimu? mbona nafanya yenye kumkera lakini yeye anafurahi
na kusema ahsante,muhudumu akamwambia
huyo ndio mwenye mgahawa HUU..
Mafunzo:Tujifunze kuondoa chuki mioyoni mwetu
kwani Ubaya umfanyiao MTU huenda ikawa
sababu ya kunufaika kwake na ikawa njia ya
kuanguka kwako

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG