ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

Nanasi ni mojawapo ya matunda niyapendayo sana. Ni matamu, yana maji mengi, na ladha iliyo kamili. Nimeona ni vizuri kuweza kuchangia mawazo yangu juu ya faida kubwa za kula nanasi kwa wingi ili kuweza kuboresha afya yako. Cha msingi zaidi, nanasi hutumika kama dawa ya kuulinda mwili mwako.

Tuangalie faida moja moja za nanasi kwa mwili wako:

1.Kuondoa Uvimbe.

Nanasi ina kimeng’enya kinachoitwa
bromelain, kinachosaidia kutibu vitu mbalimbali mwilini lakini ni madhubuti kwa kupunguza uvimbe wa ngozi kutokana na maambukizi au vidonda. Bromelain ni madhubuti pia katika kupunguza mauvimu ya viungo au uvimbe sugu. Kimeng’enyo hiki pia kina kemikali zinazosaidia kuangamiza seli za uvimbe mwilini.

2.Kuongeza kinga ya mwili.

Nanasi lina vitamin C kwa wingi pamoja na vitamin A, B1, B6, nyuzinyuzi (fiber), calcium, phosphorous na potasiam.
Nanasi husaidia kuimarisha mifupa kutokana kuwa na madini ya manganese, ambayo hutumika mwilini kujenga tishu (connective tissues) na mifupa.
Kuboresha mmeng’enyo wa chakula
Kimeng’enya cha bromelain pia hutumika katika kuvunja (breakdown) molekuli za protini, ndio maana juisi ya nanasi hutumika kwenye marinade kulainisha nyama. Faida za kulainisha nyama na juisi ya nanasi ni kuwa kiwango cha sukari kilichopo kwenye nanasi kinafanya mwili kupunguza kiwacho cha sukari kwenye damu. Hii inasaidia katika kuongeza nguvu na kusaidia mmeng’enyo mzuri wa chakula.

3.Kuimarisha macho

Nanasi lina kemikami inayoitwa beta-carotene ambayo ni muhimu kwa macho yenye afya. Ukiwa na nanasi kama tunda katika mlo wako kila siku unaongeza ufanisi wa macho na kuepuka kupata matatizo ya upofu umri unavyozidi kwenda.

4.Kupunguza uzito.

Nanasi limejaa virutubisho muhimu ambavyo vinahitajika mwilini. Uzuri wa vyakula vilivyojaa virutubishi ni kuwa vinakufanya unajisikia umeshiba bila kula karoli nyingi. Hii nni njia mbadala ya kuhakikisha uzito wa mwili wako unabaki wa afya wakati unaendelea kula vizuri.

Baadhi ya faida zingine za nanasi:

i.Tunda hili husaidia kutengeneza damu
ii.Nanasi husaidia kuimarisha mifupa , meno, neva na misuli (muscles).
iii.Tunda la nanasi hutibu matatizo ya tumbo.
iv.Hutibu matatizo ya Bandama
v.Hutibu matatizo ya Ini
vi.Husaidia kusafisha Utumbo mwembamba
vii.Husaidia kutibu Homa
Viii.Husaidia kutibu Vidonda mdomoni
ix. Husaidia kutibu Magonjwa ya koo
x. Husaidia kutibu tatizo la Kupoteza kumbukumbu
xi.Husaidia kutibu maradhi ya akili Kukosa mori (low spirit)
xii.Husaidia kutibu Kikohozi.
xiii.Husaidia kutibu tatizo la Kutetemeka
xiv. Husaidia kutibu tatizo la Woga ( Anxiety )

NB:
Nanasi lina sukari nyingi sana, na ni vizuri kula vyakula kama hivi kabla ya kufanya zoezi ili kuupa mwili nguvu sababu inapunguza kiwango cha sukari kwenye damu. Inabidi uwe makini tu kama una matatizo ya kisukari au unadhurika na sukari nyingi, sababu nanasi linaweza kukuletea madhara zaidi ya faida.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG