HILI NDILO TATIZO LINALOMFANYA MWANAMKE AKOSE HAMU YA TENDO LA NDOA (LOBIDO IN WOMEN)

HILI NDILO TATIZO LINALOMFANYA MWANAMKE AKOSE HAMU YA TENDO LA NDOA (LOBIDO IN WOMEN):

Karibu ndugu msomaji wa makala yangu ya afya ninayoandika kila wakati ili kuelimisha jamii, japokua wengine wanadhani natangaza huduma yangu ila cha msingi ninachokusudia ni jamii inayonizunguka iweze kufaidi na kuelewa afya zao kwa ufasaa .
Leo hii ningependa kuelezea tatizo hili la upungufu wa hamu ama ashki ya kushiriki tendo la ndoa kwa kinamama, niwazi kua imezoeleka katika masikio ya wengi kusikia wanaume wakilalamika kupungukiwa na nguvu za kiume lakini, nimarachache sana kusikia malalamiko haya kutoka kwa wanawake. sio kwamba wanawake hawana tatizo hili,hapana, hata wao wanasumbuka sana na hii hali lakini ni wagumu sana kujitokeza na kutafuta tiba lakini takwimu zinaonesha wanawake ndio wanatatizo hili kubwa sana hata kuliko wanaume ila niwachache wanaojitokeza ,mara nyingi wenzi wao (bwana zao), ndio wanaopokea malalamiko haya, utasikia mwanamke akiomba UDHURU kila siku kua HAJISIKII kushiriki tendo hilo ama kila siku utasikia akilalamika kua ANAUMWA hivyo basi hawezi kushiriki tendo hilo na hata inapotokea mwanaume akamlazimisha kushiriki tendo hilo basi hulalamika kua ANAUMIA wakati mwingine mwanaume anaweza ona mwanamke akitokwa na damu sehemu zake za siri mara baada ya kushiriki tendo hilo hali inayompelekea mpaka kumeza vidonge vya kutuliza maumivu.
Hali hii huwapata sana wanawake walio na umri wa kuanzia miaka 35 na kuendelea lakini kwasasa hata watoto wadogo wa umri wa miaka 25 utaona wanalalamika kua hawana kabisa hisia za kushiriki tendo hili (sex), hali hii inaweza sababishwa na mambo ya fuatayo.
chanzo cha tatizo hili zinaweza kugawanywa katika makundi mawili;
1).Tatizo la kimaumbile na tabia (Physical cause),
2). Tatizo la kifikra (Psychological cause)
TATIZO LA KIMAUMBILE & NATABIA.
visababishi hivyo vinaweza kua;
~ Kupungukiwa kwa madini chuma (Anaemia) ,hii ni kutokana na ukweli kua mwanamke hupoteza madini mengi sana akiwa kwenye siku zake (Hedhi).
~ Ugonjwa wa kisukari (Diabetic patients), ugonjwa huu wa kisukari husababisha upungufu wa kushiriki tendo la ndoa kwa njinsia zote mbili,(wanaume na wanawake).
~Mabadiliko ya vichocheo vya mwili (hormonal changes), mabadiliko haya yanaweza kusababishwa na mabadiliko ya maisha ya mwanamke kama vile lishe, kazi n.k lakini pia, hali hii hujitokeza kwa wanawake wengi mara baada ya kujifungua (Kuzaa), mwanamke hukosa kabisa hamu ya kushiriki tendo hilo na hujikuta mkavu katika sehemu zake za siri na hivyo basi hupata maumivu makali sana anapokua kwenye tendo hili.
~Matumizi ya madawa, mara nyingi matumizi ya dawa za uzazi wa mpango imelalamikiwa na wanawake wengi kua zinawafanya kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wengine hudai kua wanakua wakavu sana ama wengine hudai wanakua na hali ya kutokwa na maji (ute), mwingi sana anaposhiriki katika tendo hili hali ambayo huwachukiza wapenzi wao na hivyo basi hali hii huwaharibu ushiriki katika tendo hili kwa kuogopa lawama kutoka kwa wapenzi wao.
~ Unywaji wa pombe kupita kiasi, huharibu vipokeo (receptors) ambavyo huwa ni muhimu katika kuuweka mwili katika mudi nzuri tayari kwa kushiriki tendo hilo.
~ Matumizi ya madawa ya kulevya.
Ukomo wa hedhi (menopausal syndrome), hii ni kwa wale wanawake waliofikia umri wa kuanzia miaka arobaini, japokua siku hizi hata maika 35 unakuta mwanamke anasumbuka na hili tatizo la kukoma kwa hedhi ambapo sio kawaida,mara nyingi humfanya mwanamke kua na ndoto nyevu hali inayomfanya akose hamu ya kua na mumewe na kushiriki tendo hili.
TATIZO LA KIFIKRA ( Psychological cause );
hii inaweza kua;
~Msongo wa mawazo (Depression),
~Utendaji wa kazi kupita kiasi,
~Hofu ama wasiwasi (anxiety),kutokana na jambo flani linalo mkabili basi mwanamke anakua katika hofu flani hivi ambayo inamfanya asiwe na furaha ama hamasa ya kushiriki tendo la ndoa.
~Kumbukumbu ya kitendo cha kikatili cha kijinsia,hii mara nyingi inawakuta wanawake waliowahi kubakwa ama kushuhudia kitendo chochote kiovu cha unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake. hali hii hujijenga katika akili na hatima yake huharibu kabisa msisimko wa kushiriki tendo hili la ndoa.
~Athari zinazotokana na kitendo cha USAGAJI ( latent lesbianism), hii ni kwa wanaume wanaita kufanya PUNYETO, sasa kwa wanawake ni USAGAJI, mwanamke anajiridhisha mwenyewe kwa kujichokonoa kwa vifaa maalumu kwaajili ya tendo hilo. hii humfanya awe na msisimko mdogo sana hata anapokutana kimaumbile na mwanaume kwani hujihisi kama vile hawezi kuendana na kasi anavyofanya yeye kwa kutumia mikono pamoja na kifaa chake.
~Matatizo ya kimahusiano, hapa utakutana na wanawake wanaoishi katika mahusiano kwa ugonvi, yaani kila siku tuhuma na malalamiko kibao, matusi na wakati mwingine ngumi mkononi.
~Mazingira ya kushiriki tendo la ndoa,unakuta mnaishi kwenye nyumba ya wazazi wa mume au mke sasa mwanamke anashindwa kujiachia na kujipa raha badala yake anapoteza ule msisimko wenyewe.
TIBA;
upatikanaji wa tiba wa tatizo hili linalo wakabili wanawake umekua ni mgumu sana,hata hivyo kuna baadhi ya dawa zilizowahi kutumika na hata wakati mwingine bado zinaendelea kutumika kwa kiasi kidogo sana ili kuongeza hamu ya tendo hili ni kama;
TESTOSTERONE
hivi ni virutubisho vinavyotumika kuamsha ashki kwa mwanamke ili aweze kushiriki tendo la ndoa japokua madhara yake ni kama
* kupoteza nywele,
*Sauti kua kama ya kiume,
*Kua na tabia za kiume.
* kuongezeka kwa ukubwa wa kisimi ( clitoris enlargment) n.k
wengine wanatumia kifaa kimoja kinaitwa,
SUNCTION VIBRATOR,
kifaa hiki hutikisa kisimi na kumfanya mwanamke ajihisi kua na hamu ya kuhitaji mwanaume sasa lakini,hata hivyo kinapatikana kwa bei kubwa sana hasa vinatumiwa sana na Watu wanaoishi nchi zilizoendelea.
wengine wanatumia mafuta flani hivi yanaitwa ,
DESIRE CREAM,
Haya ni mafuta ambayo mawanamke anajipakaa sehemu zake za siri basi yanamfanya kusisimka na kuhitaji mwanaume.
NB; ili uweze kutibu tatizo hili basi ni vizuri ukatambua kwa kina chanzo chake ni nini??
japokua tatizo hili kwa kiasi kikubwa linambatanishwa na kubadilika kwa homoni za uzazi ndipo tatizo linapojitokeza,hasa wanawake waliofikia ukomo wa hedhi ndio huongezeka zaidi hali hii.
DAWA NILIZONAZO KWA WATU WA TATIZO HILI NI WALE TU AMBAO TATIZO HILI LINAAMBATANA NA;
~kuvurugika kwa homoni (vichocheo vya mwili),
~tatizo la kisukari,
~ Tatizo la moyo,
~ msongo wa mawazo (Depression).
ikiwa tatizo linambatana na hizo sababu hapo juu na unahitaji tiba basai waweza kuwasiliana na mimi kwa simu namba +255 785 494 456.

KARIBU SANA.

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG