JIFUNZE JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA.
JIFUNZE JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA.
Habari yako ndugu msomaji wangu, natumai umejaariwa afya tele na Mwenyezi Mungu. Vivyo hivyo na mimi anazidi kunijalia pumzi ili niendelee kutimiza lengo lake la kuniletea duniani. Najua moja ya lengo lake ni kunifanya nikuelimishe juu ya mambo mbali mbali ya maisha hasa yale yanayolenga kukuza uchumi wako wa kila siku.
Leo nakuletea mada nzito iliosheheni utamu na ufumbuzi wa matatizo mengi hasa kwetu sisi wenye ndoto ya kuwa wajasiriamali na wawekezaji wakubwa hasa katika ulimwengu huu wenye utandawazi wa technologia kubwa.
Katika ulimwengu huu, kiujasiriama umegawanyika katika makundi makuu matatu.
▶ Watu wenye pesa lakini hawana muda na hawana wazo la biashara.
▶Watu wenye muda lakini hawana pesa wala wazo La biashara.
▶Watu wenye wazo la biashara lakini hawana muda wala pesa.
Basi leo nitajikita hasa katika swala la kujua jinsi gani mtu unaweza kupata wazo la biashara. Kuna njia nyingi sana za kuweza kugundua wazo la biashara, Hapa nitakupa njia tatu tu na zile zingine unaweza weka namba yako ya Telegram, whatsapp, imo au ukaweka email address yako kwenye comment apo chini kisha nitakutumia.
UNAKIPAJI GANI. (WHAT IS YOUR TALENT?)
Hii ni njia ya kwanza ambayo ni wachache sana wanaitumia. Kipaji ni talanta ambayo mtu uzaliwa nayo, hii ni zawadi ambayo Mungu umjalia mwanadamu bure zako Ukiweza kuitambua inaweza kuwa ni chanzo cha wewe kupata wazo la biashara na ukatengeneza pesa za kutosha, ebu anza kujiuliza sasa ivi ni kitu gani cha pekee ambacho Umejaliwa na Mungu.
Kama unaweza kuimba mpaka ukakonga nyoyo za watu basi imba sana. Si unaona waimbaji wa mziki duniani na nchini mwako wanavyo tengeneza pesa kwanini usitumie nafasi iyo kutengeneza maisha.
Je unakipaji cha kucheza mpira? Basi jinoe iyo ndio talanta yako na itumie vizuri. Si unaona wachezaji mpira wakubwa duniani, si unaona jinsi walivyo mabilionea, sasa kwa nini na wewe unitumie kipaji chako kutengeneza maisha.
Tambua kipaji chako leo na kitumie vizuri hilo ndio wazo lako la biashara na hautajuta.
NI SHIDA GANI ILIOKO KATIKA JAMII YAKO. (WHAT IS THE PROBLEM IN YOUR SOCIETY)
Hii ni siri kubwa sana ambayo Ukiweza kutumia naamini itakuletea matunda makubwa katika maisha.
Huna aja ya kuangaika kujua ni biashara gani uanzishe, cha msingi angalia jamii yako inasumbuliwa na matatizo gani kisha tatua tatizo hilo uone jinsi utakavyo nufaika.
Tatizo letu tunapenda biashara za kuigana, ukisikia masawe kufungua genge la kuuza nyama ya kuchoma na anapata faida kubwa basi na wewe unakurupuka nayo unafungua na wewe genge mwisho wa siku mnaanza kugombania wateja mwisho wa siku kile ulichokitarajia unakikosa na unaanza kutafuta dawa ili uvute wateja. Katika biashara hakuna uchawi mchawi ni wewe mwenyewe.
Mfano katika mtaa wako, kuna uduma ya maji? kuna uduma ya matibabu kama pharmacy? kuna duka la nyama la kisasa? Kuna uduma za machine za kusaga? Je, kuna uduma za uzoaji taka? Sasa utashangaa mtu anakwambia mimi siwezi kuzoa taka taka na elimu yangu hii ya chuo kikuu. Ndugu yangu ebu hesabu kijiji au mtaa wako una kaya ngapi? Chukulia kijiji kiwe na kaya 1000 na wewe ukiamua kuchukua tenda ya kukusanya uchafu huo na kila kaya ilipe 1000 kwa wiki, ni shilingi ngapi Utakuwa umekusanya kwa wiki moja? Utapata Tsh 1,000,000/= kwa mwezi ni milioni 4. Je ikitokea ukapata tenda Mitaa 4 utakusanya shilingi ngapi kwa mwezi? Ni milioni 16. Ebu tuzisome jamii zetu zina matatizo gani tutazjikosesha utajiri bure na kuishia kulalamika maisha magumu kumbe sisi ndio wagumu.
JIFUNZE KUTOKA KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI. (LEAN FROM YOUR NEIGHBORS)
Mala nyingi tunashauriwa kujifunza kwa walio tutangulia. Maana wao ndio wanauzoefu wa biashara na ni wao wanajua masoko yanapatikanaje, ni wapi kuna changamoto na wanazikabili vip.
Mfano chukulia shangazi yako au baba ako mdogo anamiliki biashara fulani na amefanikiwa basi ni nafasi nzuri kukaa nae na kujifunza yeye amefanya nini mpaka kufika pale alipo. Ukisha jifunza kwao unanafasi kubwa ya kuifanya kiubora zaidi maana Utakuwa umeishajifunza mbinu zao na jinsi ya kuwasiliana na changamoto. Mfano mzuri ni Bilionea MO Dewji wa Tanzania, ukimsikiliza yeye mwenyewe anakili kuwa biashara kujifunza kutoka kwa baba yake, na kutokana na hilo alifanya kuendeleza biashara ya baba ake na akaamua kuifanya kwa ubora zaidi.
Mbinu hizi ni nzuri na ninaimani ukiitumia zitakusaidia sana. Mbinu zipo nyingi, kuzipata hizo zingine weka namba yako ya whatsapp, telegram, imo au email address nitakutumia bure kabisa.
Unaweza kutembelea www.fancompany.blogspot.com ili ujifunze mengi zaidi, karibu sana Tujifunze pamoja na tuutokomeze umaskini.
Comments
Post a Comment