JIFUNZE JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA. SEHEMU YA 2.
JIFUNZE JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA. SEHEMU YA 2
Baada ya kuwa tumeona zile njia tatu za awali, basi apa tutaona njia zingine ambazo zitakusaidia kupata wazo la biashara kama una ndoto za kuanzisha biashara.
Kwa dondoo tu kwa zile tulizokwisha jifunza, tuliona jinsi ya kukitumia kipaji chako kama wazo la biashara, kwa kutumia shida zilizopo katika jamii yako na kuwa wazo la biashara na mwisho tukaona jinsi ya kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali waliokwisha kutangulia.
Basi tutazame mbinu zingine unazoweza kutumia na kupata wazo la biashara.
KUPITIA MAZUNGUMZO YA MARAFIKI ZAKO.
Kila mtu anamarafiki wa aina mbalimbali ivyo kupitia wao unaweza pata wazo la biashara. Chamsingi angalia ni mambo gani wanapendelea kuzungumza na wanapendelea nini. Ukiona wanapendelea mambo fulani na ili wayapate uwalazimu kutumia gharama na muda MWINGI kuyapata.
Basi wewe kuwa suluhisho la tatizo lao, kisha utaona utakavyo pata pesa mpaka ushangae. Mfano kwa akina dada yawezekana kuna kitu fulani wanapendelea hasa katika mambo yao ya kiurembo, Maana wanawake ndio wanaosifika kwa kuzijua fasheni, basi wewe waletee vitu wanavyopenda, ukifanya ivyo Utakuwa umewateka akili zao na mwisho wa siku utashangaa utakavyoanzisha biashara na kuwa na wazo juma kwao.
KUPITIA KUSAFIRI KATIKA MAENEO MBALI MBALI.
Kupitia kusafiri katika maeneo mbalimbali unaweza kupata wazo la biashara na ukalitumia likakuingizia kipato.
Mfano wewe unaishi Dar es salaam kisha ukaamua kutembelea mikoani na unaweza kugundua aina ya biashara inayofanyika uko mikoani na Dar es salaam hakuna, ivyo ukiamua kuchukua wazo hilo na kuliingiza Dar es salaam utaona jinsi utakavyo jipatia pesa za kutosha maana Utakuwa ni wewe tu na hakuna mwingine maeneo hayo. Ivyo anza kusafiri kwa Malengo.
SOMA VITABU NA MAJARIDA MBALIMBALI.
Kupitia kusoma tunajifunza mambo mbali mbali na kutuongezea ujuzi mbalimbali. Ivyo pindi upatapo nafasi ya kusoma makala, majarida na vitabu soma kwa Malengo.
Kuna majarida mbali mbali ya ujasiliamali, kuna makala mbalimbali zinazozungumzia mambo ya biashara, ivyo usiyapuuze ndugu yangu soma unaweza kujiajili na kutengeneza wazo ZURI la biashara.
Mimi mwenyewe ni sahidi wa swala hili maana kabla ya kuachana na Ajira na kutengeneza ajira binafsi nilikuwa najisomea sana makala na vitabu mbali mbali kisha mwisho wa siku nikaja na wazo la biashara yangu ya uuzaji na usambazaji bidhaa mbalimbali na sasa nina project mpya ya NYUMBANI BUSINESS PLAN. Ivyo nakushauri ndugu yangu anza sasa kujisomea.
SHIRIKI SEMINA NA MAKONGAMANO YA KIBIASHARA.
Unapopata nafasi ya kushiliki katika semina mbali mbali za ujasiriamali usipuuze. Kule unaweza kujifunza jinsi ya kuanzisha biashara ambayo ata ukuwai kuwazia.
Mfano kuna wakati uwa kunakuwa na maonyesho ya kibiashara, kama Saba saba na nane nane kwa Tanzania, maonyesho haya sio ya kwenda na kununua bidhaa na kuondoka, ebu jiulize wewe hatamani kuwa miongoni mwa wanaohusika katika kuuza bidhaa mbalimbali mahali apo. Basi siku nyingine nenda ukidhamilia kujifunza na kupata wazo jipya la biashara.
KUPITIA ELIMU ULIYONAYO.
Wakati mwingine watu usahau kuwa elimu zao zaweza kutengeneza wazo la biashara, na mwisho wa siku uishia kuwaza kuwa elimu ni kwaajili ya kuajiriwa tu.
Hivi ulijiuliza ni kwanini unaajiliwa, Je umeajiliwa kwa sababu gani? Unajua kuwa apo ulipo ajiliwa unatimiza wazo la biashara la mtu fulani na unatimiza ndoto yake.
Sasa basi kupitia elimu yako unaweza kuanzisha biashara yako na ukajipatia kipato. Mfano. Kama wewe ni ubunifu wa majengo, basi anzisha kampuni yako, kama wewe ni mwalimu anzisha shule, kama wewe ni mtaalamu wa maswala ya biashara anzisha taasisi yako ya biashara kama mimi nilivyofanya.
Kila kitu kinawezekana kaa chini tafakari kisha njoo na wazo litakalo tokana na elimu yako na kwakuwa umesomea mambo ayo basi usimamizi wake Utakuwa mzuri na wa kitaalamu zaidi kuliko kujiingiza katika biashara ambayo huna ujuzi nayo mwisho wa siku utaishia kufirisika.
Basi mpaka apo naamini umeweza kupata kitu fulani ambacho kwa namna moja au nyingine kitakusaidia katika safari yako ya kimafanikio.
Basi nikualike katika blog yangu ambapo utaweza kujifunza mambo mengi yatakayokufaa kibiashara na kimaisha www.fancompany.blogspot.com
Pia unaweza kulike ukurasa wangu facebook wa FRANK A. NDYANABO - FAN na unaweza kushare makala hii na mafanikio zako nao wakajifunza zaidi.
Ni mimi, Frank A Ndyanabo 0785494456
Comments
Post a Comment