JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA MTAJI. SEHEMU YA 3

JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA MTAJI.

SEHEMU YA 3.

Habari yako ndugu msomaji wa makala hii.  Tuko katika mwendelezo wa mada yetu ya, kuanza biashara bila mtaji.  Na leo tunaendelea na sehemu ya tatu ya mada hii, leo tutaangalia mambo mawili ambayo unaweza kuyatumia na yakakusaidia katika kuanza biashara.  Karibu tujumuike sote.

TUMIA UWEZO BINAFSI.

Katika hali ya kawaida kila mwanadamu kajaliwa uwezo fulani wa ziada ambao mbali na elimu au kipaji cha kuzaliwa nacho ila anaweza kuwa kajaliwa uwezo fulani binafsi ambao unaweza kuupata kwa kufanyia mazoezi kila mala na ukaweza kubobea katika jambo hilo.

Sasa basi kama wewe ni mbobevu katika jambo fulani basi waweza kutumia nafasi hiyo nakuweza kujitengenezea mfereji wa pesa.  Mfano: yawezekana wewe ni mbunifu wa mitindo mbalimbali ya mavazi, basi fungua office au kampuni kisha anza kuonyesha umahili wako katika kubuni mavazi na mitindo mbalimbali.

Au yawezekana wewe ni mchoraji mzuri, kiasi kwamba ukiamua kuchora basi kitu kinatokea kama kilivyo, basi anzisha kituo cha uchoraji na anza kujitengenezea pesa, ebu angalia katika maeneo unayoishi ni watu wangapi wanaitaji kuchorewa katika vibanda na frem zao za biashara, au ni watu wangapi wanahitaji michoro mbalimbali kwaajili ya matumizi yao binafsi, basi anza kuitumia nafasi hii.

Kuna dada mmoja ni rafiki yangu tokea tuko chuoni, siku moja alinifuata na kuniuliza jambo, Frank hivi nikiamua kubuni mikoba ya akina mama na viatu vya chini chini kwa kutumia vitenge siwezi kutengeneza kipato kweli?  Swali nililomuuliza ni, Je unauwezo wa kutengeneza hivyo vitu?  Alinijibu, ndio naweza kufanya hivyo maana naweza kushona na nimewai kujifunza kwa mama yangu.  Basi baada ya kuwa ameniambia hivyo, nikamwambia basi fanya hicho kitu. Huwezi amini mpaka Sasa anaduka kubwa tu la vifaa vya urembo kwa akina dada ambavyo anatengeneza mwenyewe kwa mikono yake. 

Tatizo linalotukumba tulio wengi hatujiamini na kile tulichonacho ndio maana tunatanguliza kushindwa badala ya kutanguliza ushindi na kama kushindwa kubaki kuwa bahati mbaya.

TUMIA MWONEKANO WAKO.

Muonekano wako waweza kuwa chanzo kikubwa cha mapato ukashangaa, ndio maana wale wote wanao bahatika kutambua hili ufanikiwa sana.

Ebu jiulize swali hili, Je mimi ninamwonekano gani?  Je muonekano wangu unafaa kuniingizia pesa?

Juzi nikiwa ofsini kwangu, alikuja binti mmoja akiwa na shida ya kiofisi, baada ya mazungumzo nilimuuliza swali, Hivi dada Angel, mwonekano wako huo unaonaje ukifanya shughuli za modeling maana wembamba, urembo na urefu wako vimekaa sawa?  kwanza hakuamini kama ninaweza kumwambia kitu hicho.  Alichonijibu ni kuwa, ata yeye anapenda sana hicho kitu sema uwezo hana.

Ninachotaka kukwambia ni kuwa, unaweza kuutumia mwonekano wako ukatoka kimaisha, mfano, mwangalie mtu kama kingwendu, Hashim Thabit, na wote wenye mili mikubwa kama Mac Organ, Rend Guard na wengine wameweza kutengeneza pesa za kutosha.  Sasa na wewe anza kujiuliza je mwonekano wako unafit sehemu gani, ambayo unahisi unaweza kutengeneza pesa?

Basi nikutakie mchanganuo mwema wa jinsi ya kuanzisha biashara bila mtaji, waweza pia kuwashilikisha na wengine kwa kushare hili na wao waweze kujifunza, kuwa tayali kuwapatia elimu hii bure kama mimi nilivyo kupatia bure kabisa.

Ni mimi Mkufunzi na Mshauri wako wa maswala ya biashara,  Frank A. Ndyanabo.  +255 785 494 456

www.fancompany.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG