JITOE MUHANGA (SACRIFICE)
JITOE MUHANGA(Sacrifice)
Mafanikio yako yatategemea na kiwango cha uwekezaji wako. Ili ufanikiwe na upate matunda mazuri lazima ujitoe vya kutosha.
Kujitoa muhanga sio jambo jepesi bali inakupasa ujipange hasa. Watu tumekuwa tukishindwa kwa kushindwa kufahamu jambo hilo.
Kuna watu wamekuwa wakiitaji mafanikio makubwa ila kiwango cha uwekezaji wao hakiendani na kile wanachokiwekeza.
Ebu jiulize apo ulipo ni vitu gani unatamani kuwa nayo, ukisha pata jibu basi jiulize tena umejitoa kiasi gani kwaajili ya kuyapata yale uyatakayo?
Kujitoa muhanga kupo kwa aina nyingi, na apa nataka tuelewane jambo moja, apa sizungumzii Kujitoa muhanga kwa kufanya kafala, la hasha. Jambo la msingi apa ni jinsi gani utajitoa kwaajili ya maisha yako pasipo kuhusisha habari za kafala za kumwaga damu wala nini.
Kujitoa muhanga, ni jinsi gani unatumia muda wako mwingi katika kuakikisha unafanikiwa, kuna usemi mmoja kuwa, "kadri unavyojitoa kwa muda mrefu ndivyo jinsi unavyo yakaribisha mafanikio"
"Sacrifice in the short - term is the price you pay for security in the long-term"
Unapoamua kujitoa kwaajili ya maisha yako lazima uzingatie mambo ya msingi yafuatayo
1⃣ Muda.
2⃣ Pesa.
3⃣ Elimu
MUDA :
Tukiwa tiali kujitoa kwaajili ya maisha yetu, swala la Muda ni muhimu sana. Usije ukakaa ukafikilia kuwa maisha mazuri yanatokea kama muujiza.
Toka nilipoamua kujiingiza katika ujasiriamali, swala hili limeniongoza sana mimi Frank Ndyanabo, Maana kipindi cha nyuma niliona kama vile maisha ni kubaatisha ila baada ya kuamua kuyabadili maisha yangu, swala la Muda imekuwa ni nguzo kubwa sana. Katika maisha yangu sikubali muda wangu upotee bila sababu ya msingi, Maana naamini kuwa kila sekunde inayo pita na kupotea bure inaondoka na kitu muhimu maishani Mwangu, na kitu hicho siwezi kukipata tena maana muda haurudi nyuma tena.
Kila siku naakikisha kuwa nina mpangilio maalumu kwaajili ya kazi zangu za kila siku. Haipo dakika inapotea bure. Ndio maana ninaakikisha ninakuwa na muda maalumu wa kufanya shughuli zangu za kiofisi, muda kwaajili ya kuelimisha watu mbalimbali juu ya ujasiriamali na muda maalumu wa kufanya shughuli za kifamilia. Haipo siku utakuta ninamuda wa kukaa kijiweni na kusogoa.
Kwa maana hiyo sina muda wa kupoteza kabisa, na wewe akikisha huna muda wa kupoteza maana muda ukiisha pita umepita.
Ulimwengu wa sasa unakutaka wewe kuwa mjanja sio wakati wa kukaa kijiweni na kujadili yasiyo ya maana, bali akikisha vijiwe vyako viwe ni vyenye kujadili mambo ya msingi mfano, kujadili juu ya uanzishwaji wa biashara, kutafuta masoko mapya na kuboresha biashara yako ili ikuletee mafanikio.
PESA:
Ukiamua kujitoa kwaajili ya maisha yako swala la pesa halipingiki ndugu yangu. Uwa nakaa najiuliza hivi mimi Frank, kama sio kuingiza kiwango fulani cha pesa katika biashara ningekuwa wapi. Maana katika biashara kuna mambo hayazuiliki, mfano vitu kama safari hazizuiliki, gharama za mawasiliano, gharama za mitandao kama simu na Internet, ni mambo ambayo hayapingiki
Kuna kipindi mimi mwenyewe nililazimika kusafiri katika mikoa mbalimbali lengo ni kwaajili ya kujenga biashara zangu, sasa kama wewe unafikilia kuwa mafanikio yatakukuta ukiwa umekaa tu sehemu moja ujue unajidanganya.
Kuna wakati unatakiwa kuwa na vitendea kazi kama simu, laptop, office na vitu vingine kam hivyo. Kuna watu waliwai kuniuliza kuwa office lazima kuwa na laptop au komputa?
Ulimwengu wa sasa vitu kama hivyo havipingiki lazima tutambue kuwa ulimwengu umebadilika ni ulimwengu wa karne ya 21, ni mwendo ya digital mambo mengi yanafanyika katika mitandao ivyo hupaswi kujenga visingizio vitakavyo kukwamisha kusonga mbele.
Jua kujitoa kugharamikia hivyo ni lazima sio hiari tena kwa ulimwengu huu.Kuna usemi mmoja unasema "Tumia pesa kupata pesa" ivyo tumia pesa katika uwekezaji wako kama unaitaji kupiga atua.
ELIMU:
Hili ni swala jingine la muhimu sana ambalo tunapaswa kujitoa muhanga ili kufanikisha ndoto zetu. Husifikilie kuwa nakwambia urudi darasani.
Wakati naanza ujasiriamali imenichukua muda sana katika kujifunza mambo haya, elimu hii kutokana na mfumo wa Elimu yetu hayafundishwi darasani. Hivyo unatakiwa kujitoa muhanga ili uweze kuvuna mafanikio yako.
Matajiri wote duniani siri ya mafanikio ni kutokana na elimu wanayoipata kutoka katika vyanzo mbali mbali. Mfano kuna wakati unasikia kuna makongamano ya biashara, husisite kushiliki.
Amua kujitoa kwa kuitafuta elimu kwa kununua vitabu na majarida mbalimbali ya kibiashara.Tafuta watu waliofanikiwa katika nyanja hizo ili wakupe muongozo wao walifanyaje mpaka kufikia apo walipo.
Kama una ndoto za kuwa bilionea katika ulimwengu huu, na ukae meza moja na mabilionea wengine, basi kuwa tayali kujitoa muhanga kwaajili ya maisha yako.
By, Frank A Ndyanabo
0785494456
Comments
Post a Comment