KUWA KIOO KWA WENGINE.
KUWA KIO KWA WENGINE.
Kioo siku zote utoataswila sahihi ya kile kilichoko mbele yake. Kama mwanamke akisimama mbele ya Kioo haiwezi kuonekana taswira ya mwanaume kwenye kio. Hii inakupa picha kuwa siku zote utabaki kuwa wewe kama wewe tu. Vyovyote utakavyo jiweka ndivyo utakavyo onekana. Swali la kujiuliza, Je unataka uonekaneje katika Kioo ?
Ukitaka maisha yako kuwa mazuri basi kuwa Kioo kwa wengine. Chochote utakacho panda kwao ndio utakacho vuna. Kama wewe unaishi na watu vizuri basi na watu watakupenda na kinyume chake inawezekana. Ukitaka kupokea zaidi basi na wewe toa zaidi. Kuna msemo mmoja zamani kutokana na akili za katoto sikuuelewa vizuri nilikuwa nikiutafsiri kitoto, msemo huo unasema hivi "Ukitaka kula shariti nawe uliwe kidogo" hii kauli inamaana kubwa sana.
Ata maandiko yanasema, huwezi kukusanya husipo Tapanya, yaani kwa lugha nyingine huwezi vuna usipo panda. Ivyo basi kama unaitaji mambo mazuri nawe wekeza katika hayo mazuri, kama unaitaji mapenzi mazuri nawe onyesha upendo zaidi, kama unatamani kuwa maisha mazuri basi wekeza katika maisha hayo unayoyataka kwa kufanya kazi kwa bidii, kama unaitaji kuwa na mauzo mazuri katika biashara yako basi na wewe boresha uduma zako kwa kuuza vitu vizuri vyenye ubora na uwe na kauli nzuri kwa wateja wako, kama unaitaji mpenzi wako azidi kukupenda basi na wewe onyesha mapenzi ya dhati kwake.
Be a refletor of what u want.
Nikutakie siku njema ndugu yangu uliesoma ujumbe huu naamini umebarikiwa.
By, Frank A. Ndyanabo - FAN
Www.fancompany.blogspot.com
0785494456
Comments
Post a Comment