HACHA KUIHUKUMU NAFSI YAKO

HACHA KUIHUKUMU NAFSI YAKO.

Kila mtu analo jambo la kufanya na tunayo malengo ya kutimiza, ila tatizo ni kuwa mioyo yetu imejaa hukumu zisizo za msingi ndio maana tunashindwa kutimiza malengo yetu.  Tunatanguliza kushindwa, aliekwambia kuwa huwezi kumiliki biashara yako nani, nani alikwambia kuwa huwezi kumiliki kampuni?  Nani alikwambia huwezi kuwa kiongozi bora, unafikiri mafanikio watu wanazaliwa nayo?  Yote yanatafutwa hapa hapa duniani.  Hacha kujihukumu bure kuwa huwezi jambo fulani,kwani wewe ni nani usiweze, wanaoweza wana nini cha ajabu?

Biashara zetu zinashindwa kustawi kutokana na minyororo iliopo ndani yetu maana tumeifunga kisawa sawa.  Mtu wazo la kufanya biashara au jambo fulani unalo ila hutaki kufanya unategemea nani akufanyie sasa, au unataka jirani yako aje afanye badala yako?  Hachana  na mawazo hayo ya kuifunga nafsi yako, punguza hiyo hukumu na upe mwili wako nafasi ya kufanikiwa, ni kuamini kwamba unaweza, kuondoa mambo yasiyo kufaa, amini kwamba unaweza, na fanya kazi kwa bidii, bonyeza link hiyo apo upate undani zaidi juu ya njia hizo http://fancompany.blogspot.com/2015/01/njia-za-kukutoa-katika-kifungo-cha.html?m=1

Mbinu hizo zitakufungua akili na kukufanya huru, Maana ata mimi zimenifunza jambo ambalo mpaka leo sijutii kuzitumia, ndio maana nazidi kusonga mbele, sasa je wewe hutaki kutoka kifungoni,au unataka kuendelea kuihukumu nafsi yako na kujiongezea minyororo?  Bonyeza link hiyo utaona ni jinsi gani baada ya mimi kuamua kuondoa makufuli kipi kimetokea http://fancompany.blogspot.co.ke/2016/01/toka-kifungoni.html?m=1

Ukiweza kufanikiwa katika hili basi kuwa tayali kuyatengeneza maisha yako kwa kutumia muda, pesa na elimu yako vizuri ili ufanikishe kile ulicho lenga http://fancompany.blogspot.co.ke/2016/02/jitoe-muhanga-sacrifice.html?m=1  hapo ndipo utakapokuwa umefanikiwa kuacha hukumu zisizo na msingi katika maisha yako.  Tusiipe mioyo yetu hukumu zisizo na maana.  Amini unaweza na amini katika ushindi tu, hachana na mawazo ya kushindwa.

~Frank A. Ndyanabo ~

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG