JIFUNZE JAMBO HILI KILA SIKU.
Mzee mmoja alianza hofia kuwa yawezekana
mkewe kaanza matatizo ya kutosikia vizuri.Hivyo
ikambidi amtafute daktari wa familia na
kumsimulia mkasa mzima.
Baada ya daktari kumsikiliza yule mme vizuri,
akamwambia kuwa sasa atahitaji akirudi
nyumbani amfanyie jaribio moja mkewe ili
majibu yake yaweze kumpa dokta mwanga wa
kumsaidia kulitambua tatatizo na yule mama
apone.
Daktari akamwambia, “ ukirudi nyumbani
simama futi 40 kutoka kwa mkeo na kwa sauti
ya mazungumzo ya kawaida ongea neno ili uone
kama atasikia na kama hatasikia simama karibu
futi 30 ukimsogela , kama hatishoshi ongeza zaidi
futi 20 mpaka atakapo kusikia”
Jioni yake mzee akiwa sebuleni na mama akiwa
jikoni anaandaa chakula cha jioni, baba akiwa
sebuleni akamwita mkewe na kuuliza, “Mpenzi
tuna kula nini leo jioni?” lakini mke hakujibu.
Mzee akazidi kusogea futi 30 karibu akamuuliza
tena, “Mpenzi tuna kula nini leo jioni?” lakini pia
mke hakujibu, mzee akasogea tena futi 20 karibu
na jikoni na kumuuliza tena, “Mpenzi tuna kula
nini leo jioni?” mara hii mke hakujibu tena.
Basi ikambidi yule mzee amsogelee mpaka
karibu yake na kumkumbatia mgongoni huku
akimuuliza tena “Mpenzi tuna kula nini leo jioni?”
mkewe akamjibu,” mme wangu nimepika kuku”
mbona nimekujibu tangu uko sebuleni ina
maana hukunisikia?
Mzee yeye alidhani mkewe ndio mwenye tatizo la
kutomsikia mtu akiwa mbali yake kumbe yeye
mzee ndio mwenye tatizo la kutosikia mtu akiwa
mbali.
Ndio ilivyo katika Maisha yetu ya kila siku,
tunaweza tukafikiri kuwa wenzetu ndio wenye
matatizo zaidi lakini kumbe sisi ndio wenye
matatizo zaidi.
Pia ni vyema kutokuwa wepesi wa kuhukumu au
kueneza jambo lolote tunaloliona kuwa ni baya
bila ya kuangalia sisi tupo upande gani katika
uvumi huo~Frank A. Ndyanabo - FAN
Comments
Post a Comment