JIFUNZE KUTUMIA PESA
JIFUNZE KUTUMIA PESA.
Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu za kila siku. Natumai ni mzima wa afya tele. Leo nakuletea mada ambayo nimeona ni tatizo kwa watu wengi, hivyo karibu uweze kujipatia somo hili makini na lenye Mwanga wa maisha yetu.
Ulisha jiuliza kwa nini maskini wanazidi kuwa maskini zaidi na matajiri wanazidi kuwa matajiri? Kuna msemo mmoja nimekuwa nikiusikia toka nikiwa mtoto mdogo, kuwa ukizaliwa maskini basi utakufa maskini na tajiri atazidi kuwa tajiri. Bado wakaenda mbele zaidi kuwa mwenye nacho atazidi kuongezeawa, hapa tunasema maji ufuata mkondo, haipo siku maji yakapanda mlima. Kauli hizi zinaweza kuwa kweli au si kweli, Je wewe kutokana na mtazamo wako unaonaje?
Kwangu mimi Frank, nasema sio kweli kabisa matajiri wanaendelea kuwa matajiri kwa maana wanajua mbinu sahihi za kutumia pesa hili kutengeneza pesa ndio maana pesa kwao hazikatiki. Lakini kumbuka watu hao hawakuzaliwa wakiwa matajiri bali nao walikuwa maskini kama wengine waivyo. Lakini kwakuwa waliukataa umaskini ndio maana wakajifunza mbinu hizi za kutumia pesa vizuri ili kuwa mabilionea.
Sasa hebu tutazame ni jinsi gani wewe waweza kutimiza ndoto yako, kwa kutumia pesa kidogo ulionayo na unatengeneza mabilioni ya pesa.
Kwa kuanza hebu tumuangalie maskini anatumiaje pesa. Tunaposema maskini tunamaanisha watu wenye vipato vya chini, kama waajiriwa na wafanya biashara wadogo. Kundi hili mara nyingi uhishi kwa kutegemea mshahara na mapato kidogo yanayo patikana katika biashara zao. Hivyo kipato hicho huishia kununua maitaji ya kila siku kama chakula, nguo, matibabu na baadhi ya vitu vya ndani visivyo ingiza pesakama TV(flat screen), Radio(home theater), sofa, AC, makabati n.k. Hivyo pesa yote inapoingia huishia katika maitaji hayo. Mwisho wa siku hujikuta wanajaza makolokolo kibao ndani pasipo na sababu za msingi, hii wakati mwingine ni kujifanya tunaenda na fasheni. Na hii ni kutokana na sababu kuwa pesa tunayopata haizalishi pesa nyingine badala yake ujikuta tunatumia yote mpaka inaisha.
Kundi hili la maskini pia ujitahidi kumiliki vitu ambavyo huwalazimu kutumia pesa kila kukicha. Mfano : kununua magari ya kutembelea, kukodi nyumba za kifahari za kuhishi, hivyo basi kila pesa inapoingia (mshahara na mapato mengine) huishia kulipia kodi ya pango na service za magari na vitu vingine kama umeme n. k, kwa kufanya hivyo hujikuta wakati mwingine matumizi yao huzidi kipato Chao. Kwa maana hiyo hulazimika kuwa watumwa katika ajira, Maana bila kufanya kazi maisha hayaendi sawa,maana mahitaji ni makubwa, na hili kukidhi razima kufanya kazi kwa nguvu ili kupata pesa ya kujikimu.
Kwa maana hiyo maskini kipato chake utegemea zake. Hapo ndio nakumbuka usemi mmoja kuwa, "mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe" na maandiko yanachagiza kuwa, hasiye fanya kazi hasile. Maana yake ni kuwa, maskini analazimika kusoma kwa bidii ili aweze kupata ujuzi atakao badilishana na mtu mwenye pesa zake, na wakati mwingine unaweza kuta mwenye pesa zake ata shule hajaenda, na bado pesa unayoipata inapigwa kodi ya kutosha, apo haipo siku kipato kitatosha maitaji yako.
Hebu tumuangalie tajiri anatumiaje pesa au ni jinsi gani utaweza kubadilisha maisha yako kutoka umaskini na kuwa tajiri mkubwa. Siri kubwa ilioko hapa ni kuwa ukitaka kuwa tajiri nunua ASSETS. Assets ni kitu chochote chenye uwezo wa kukuingizia pesa. Matajiri siku zote ununua vitu vyenye kuwaingizia pesa. Mfano :wananunua magari ya biashara, wanajenga majumba ya kukodisha, wananunua mashamba kwaajili ya kufanya kilimo cha biashara.
Pia ukitaka kuwa tajiri juhusishe na fursa mbalimbali zitakazo kuingizia kipato endelevu. Fursa hizi zipo nyingi mno na zimetuzunguka. Kuna biashara katika karne hii ya 21 ambazo unaweza kufanya na zikakulipa maisha yako yote kwa kila mwezi mpaka mwaka bila ukomo. Na unaweza kuendelea kupokea pesa uku ukiendelea kuijenga biashara yako na ukakua kwa urahisi na kwa muda mfupi. Katika makala zinazofuata nitakuja kukuelezea fursa hizo kiundani zaidi na maajabu yake kiuchumi katika ulimwengu huu tuliomo. Hivyo husikose.
Mwisho napenda nikwambie kuwa kama una ndoto ya kuwa bilionea anza kubadilika sasa na hacha kununua vitu hovyo visivyo kuingizia pesa, bali anza kununua vitu vyenye kukuingizia kipato. Ila kama unavyo tayari anza kuvibadilishia matumizi yake na vifanye vitega uchumi utaona maajabu yake baada ya muda mfupi. Kumbuka, "Maskini siku zote ununua vitu vya kujikimu kimaisha, na tajiri ununua vyanzo vya mapato"
Ulikuwa nami Mkufunzi na Mshauri wako wa maswala ya biashara.
Frank A. Ndyanabo
+255 785 494 456
NB: ELIMU HII NIMEKUPA BURE HIVYO NA WEWE TOA BURE KWA KUSHARE NA WENZAKO ILI NAO WAIPATE.
Comments
Post a Comment