JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA MTAJI. SEHEMU YA 2
JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA MTAJI.
SEHEMU YA 2 :
Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu, natumaini ni mazima wa afya. Nikukaribishe katika mwendelezo wa darasa hili ambalo leo tunaingia sehemu ya pili, ili kuweza kutazama mambo gani yanaweza kutusaidia ili kuweza kuanza biashara zetu bila mtaji. Utakuwa nami Mkufunzi na Mshauri wako wa maswala ya biashara, Frank A Ndyanabo. Karibu twende pamoja:
TUMIA ELIMU YAKO (USE YOUR KNOWLEDGE)
Hili limekuwa ni tatizo kubwa kwa tulio wengi. Tunapomaliza shule tunawaza kuajiriwa, ulisha jiuliza kiwango cha wahitimu na idadi ya ajira zilizopo?
Takwimu zinaonyesha kuwa ajira ni chache ukilinganisha na idadi ya wahitimu wa vyuo nchini hasa apa Tanzania. Nakumbuka mwaka juzi zilitangazwa nafasi za kazi uhamiaji, walioshiliki katika interview ya hawali walikuwa ni maelufu ya watu mpaka mamlaka husika wakakosa mahali pakuwaweka wakawapeleka uwanjani wa taifa. Sasa jiulize kama interview inafanywa na watu zaidi ya 25000 unafikiri nani atakuwa na muda wa kusahihisha makalatasi yote hayo?
Bado Juzi tu TRA walitangaza nafasi watu wakajaa tena vilevile. Hii ikupe picha kuwa lazima tufikirie nje ya ajira. Sio kila ukimaliza tu shule unawaza kuajiriwa. Tusiwe kama wanafunzi wawili wanao soma kazi moja lakini kila mmoja anawazo lake baada ya kuhitimu, mmoja anawaza baada ya apo akaajiliwe na mwingine anawaza akafungue kampuni yake. Unafikiri hawa wako sawa kimtazamo? Maana yake mmoja yuko mbele kifikra kwa miaka 50 na mwingine anawaza kesho tu apo.
Chakufanya sasa wewe kama una elimu yako fikiria kuiweka katika matendo, usiwaze kwenda kuiweka rehani elimu yako. Kumbuka apo unapoenda kufanya kazi unatimiza ndoto ya mtu. Sasa basi ebu buni mradi ambao unatokana na elimu yako.
Ebu tuangalie katika jamii zetu tunamoishi unafikiri elimu yako haiwezi kuwa suruhisho la matatizo yalio katika jamii yako? Nina marafiki wengi ambao wamefanikiwa katika hili kwa kutumia elimu zao na sasa maisha yao ni mazuri. Mfano mzuri, kuna rafiki yangu mmoja ni Mwanasheria kafungua office yake ya kutoa ushauri wa kisheria, mwingine ni Daktari kuanzisha taasisi yake inayohusika na maswala ya afya. Haya mambo yanawezekana kama una mtazamo chanya wakutimiza ndoto yako.
Yawezekana wewe ni Mwalimu, fungua kituo cha elimu kwa watoto, kama wewe ni Mtaaramu wa maswala ya biashara kama mimi Frank anzisha taasisi yako ya ushauri au mradi utakao endana na elimu yako. Na haya mambo yanawezekana kabisa, ukiwa mbunifu mzuri au ukipata washauri wazuri basi utaona maajabu ya point hii.
Najua Utakuwa unajiuliza haya yanawezekanaje bila pesa, nakuhakikishia hili linawezekana ndugu yangu, bila kuwa na pesa. Katika masomo yangu yanyofuata nitakufundisha jinsi ya kuwekeza au kuanza biashara kwa kutumia pesa za watu na watu kufanya biashara.
TUMIA UZOEFU WAKO (USE YOUR EXPERIENCE)
Hii ni njia nyingine inayoweza kukusaidia katika kuanzisha biashara. Unajua unapokuwa na uzoefu na jambo fulani ni rahisi kuliendesha pasipo kuitaji msaada wowote kutoka kwa mtu. Mfano wewe ni Fundi magari, yani gari likiletwa kwako hupati shida, lakini huna office bali uko kwenye garage ya jamaa au rafiki yako. Anzisha garage yako na uanze kutengeneza pesa.
Wiki iliyopita nilikodi gari ya jamaa mmoja kwaajili ya kunibebea mzigo kutoka stand na kunipelekea ofsin kwangu, katika maongezi akanipa story moja ya Fundi gari mmoja ambaye ni mtaaramu wa BMW akasema yule Bwana anajulikana balaa anatafuta kama pesa, tatizo sasa hana office, kwaiyo yeye gari ikiletwa garage yoyote anapigiwa simu anakuja kutengeneza na pale anapotengenezea razima alipe ushuru sasa vip angekuwa na garage yake? Kilichonishangaza ni kuwa elimu yake ni kidato cha nne ila kwa sababu ya uzoefu unaweza sema labda anamasters ya engineering.
Kwaiyo basi na sisi katika idara au mazingira yetu tuliomo ebu tuutumie vizuri uzoefu wetu vizuri naamini tutafanikiwa, kama wewe ni mwalimu Anzisha shule(napenda kutumia walimu maana nawapenda sana watu hawa na ndio walionifikisha apa nilipo), kama wewe ni pharmasia anzisha dispensary. Kisha utaona majibu yake.
Basi kwa leo niishie apo, nakukaribisha katika sehemu ya tatu ya darasa hili.
Ni mimi Mkufunzi na Mshauri wako wa maswala ya biashara, Frank A Ndyanabo
+255785494456
www.fancompany.blogspot.com
Comments
Post a Comment