ZINGATIA HAYA KABLA YA KUANZA BIASHARA YA MTANDAO.
Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu za kila siku, ni siku nyingine tena tunakutana hapa nami Mkufunzi wako Frank A. Ndyanabo-FAN
Nimekuwa nikikutana na watu mbali mbali, kwa sms, simu, na inbox ya hapa facebook na kwenye mitandao mingine kama kwenye blog yangu ya www.fancompany.blogspot.com, instagram, whatsapp, telegram na LinkedIn wakiniuliza juu ya biashara hii ya mtandao, ila nilikuwa nikiwaambia mambo mbali mbali juu ya biashara hii na mambo ya kufanya ili biashara zao ziweze kunawili na kuwaletea matunda walio yatarajia.
Leo napenda nikushilikishe kitu muhimu sana wewe ndugu yangu mfuatiliaji wa makala zangu hizi, ninaamini kati yenu wapo wanaofanya biashara hii na wengine wako mbioni kuingia na wengine wanatamani kuingia ila hawajuhi waanzie wapi.
Kwanza hebu kwa ufupi tufahama biashara ya mtandao ni nini:
Biashara ya mtandao au kwa lugha nyingine wanaita biashara ya karne ya 21, ni mfumo wa biashara ambao unamuwezesha mtu kufanya biashara huria kwa kununua bidhaa au kutoa huduma ndani ya Kampuni husika na kuwa sehemu ya mmiliki ndani ya Kampuni hiyo. Mfumo huu umpatia mtu fursa ya kujitengenezea kipato cha kumwezesha kuwa mwekezaji mkubwa kupitia kampuni hiyo alio jiunga nayo.
Mfumo huu wa kibiasha ni rahisi mno maana hutakiwa kujiunga au kuingia ubia na kampuni husika kwa gharama kidogo na utendaji kazi wake huwa ni mwepesi maana hutumii nguvu nyingi bali utumia raslimali watu kutengeneza pesa, na ndio maana walio wengi utumia muda wao wa ziada na kujipatia pesa nyingi bila jasho.
Na biashara hii inafanyika katika mifumo ya aina mbili, yaani kuna kampuni zinazo toa huduma na zingine zinahusika na usambazaji wa bidhaa.
Kampuni zinazofanya biashara hizi zipo nyingi sana duniani na kampuni maarufu kwa hapa Tanzania ni kama Nepstar, Forever Living, oriflame, Edmark, Rifaro,Trevo n. k
MAMBO GANI UZINGATIE KABLA YA KUANZA BIASHARA HIYO?
Juzi kuna rafiki yangu mmoja mfuatiliaji mzuri wa makala hizi anaitwa James Kiambo, yuko Morogoro alinipigia simu na kuniuliza, "Mr. Frank A Ndyanabo, nimekutana na watu wananipa habari juu ya biashara fulani ya mtandao sasa shida ni kuwa sijuhi nifanyeje maana mimi sio mzoefu wa mambo haya, naomba unisaidie"
Majibu yangu juu ya swali Lake yalikuwa kama yafuatayo:
1. Angalia kwanza hiyo kampuni kama inafursa za kutosha.
Maana yake nini, ni kuwa ukitaka kufanikiwa katika biashara hii ya karne ya 21, kabla ya kujiunga unapaswa kujua kwanza hiyo kampuni ina bidhaa za kutosha na zipo za haina gani? Hii itakusaidia sana kibiashara. Kuna kampuni zingine zinafanya biashara hii zikiwa na bidhaa moja tu, na zingine zina bidhaa zaidi ya kumi. Ushauri wangu kwako ndugu yangu bwana James, kampuni iliyo na bidhaa zaidi ya moja Inakupa uhuru wa kufanya biashara kirahisi, yaani una uwezo wa kufanya kwa kila idara, idara moja ikikwama basi unaingia nyingine. Mfano kuna kampuni zinasambaza bidhaa za urembo, Kilimo, tiba, usafi, umeme, nk. Ukikuta kampuni kama hiyo unakuwa huru kuchagua wapi ujikite na wakati gani, hii ni tofauti na mtu alie na bidhaa moja tu.
2. Tafuta kampuni iliofanikiwa katika biashara hiyo ya mtandao.
Hii itakusaidia kujua kuwa unafanya biashara na kampuni imara yenye kukupeleka katika mafanikio na kutimiza ndoto yako. Sehemu hii ni muhimu sana na ya kuzingatia mno, ukizubaa unaingia mkenge. Lazima huisome kampuni vizuri ujue imejitanua kiasi gani, na inakubalika kiasi gani.
3. Angalia kampuni iliyo na bidhaa zenye bei inayoendana na kipato cha watu wako.
Hakuna kitu kibaya kama kuwa na bidhaa yenye bei kubwa kiasi kwamba hata mtu mwenye kipato cha chini kushindwa kupata huduma yako. Kumbuka zaidi ya 85% ya watu ni wenye kipato cha chini na chini 15% ni matajiri, Je kwa kuangalia hapo ni kundi gani kubwa sana? Sasa ukijichanganya ukaingia ubia na kampuni ambayo bei za bidhaa zao hazizingatii kipato cha walio wengi na kulenga wenye kipato kikubwa na ambao ni wachache, basi Utakuwa unajifunga kitanzi mwenyewe.
4. Tafuta kampuni yenye mfumo mzuri wa ulipaji gawio(bonus).
Hapa ndipo walio wengi huangalia tu lakini pasipo kufikiria ni mfumo nzuri au lah. Swala la kulipwa gawio lazima kuwa makini nalo, sio linatolewa kwa kificho kificho, pasipo kujua ni asilimia ngapi, na formula ya mahesabu hazijulikani.
Na katika ulipaji wa gawio au mimi Frank napenda kuita shukrani, kampuni zingine zinakuwa na masharti magumu sana kiasi kwamba mtu mwenye mtaji mdogo hawezi kuimudu mwishowe wanaishia kujuta na kujirahumu.
Pia muda muafaka wa ulipaji unaweza husijulikane, Ukiweza kuyafahamu haya mapema basi Utakuwa katika nafasi nzuri ya kufanya maamuzi.
5. Tafuta kampuni yenye viongozi wazuri wa biashara na sio washauri tu.
Kuna jamaa yangu siku moja katika mazungumzo yetu aliwai kunipa story ya jamaa mmoja ambae alimuunganisha katika kampuni kisha akamtelekeza, inamaana yeye ndio achakalike kufanya kila kitu. Hii inakupa picha kuwa huyu bwana hakuwa kiongozi bali ni mshauri tu. Ndiomaana leo hii kuna watu wanafanya biashara hii pasipo kuwa na miongozo sahihi badala yake wanaishia kusambaza habari zile zile. Mfano kuna watu ukikutana nao wanakusalimia tu kisha wana kutumia video ya kuelezea fursa hiyo ya biashara, na ukiziangalia video hizo ni zile zile kila mtu anayo. Sasa huwanajiuliza, hivi mtu akijiunga anapewa video kama kitendea kazi au inakuwaje? Ukitaka kufanikiwa katika biashara hii tafuta sehemu yenye kukusaidia kibiashara sio sehemu yenye kukukaririsha, mimi mtu akinishilikisha biashara alafu akanitumia video namtoa baruti. Nataka nisikie kutoka kwako wewe kama wewe umeiva kiasi gani,unawezaje kujieleza kibiashara maana ile ni biashara yako. Sio wewe ni Samson alafu unanipa video ya Ashura.
6. Angalia kampuni yenye bidhaa bora.
Kama umeamua kuingia ubia na kampuni iliyo katika mfumo wa usambazaji bidhaa basi angalia ubora wa bidhaa hizo. Na kila nchi ina vyombo vyake vya kudhibitisha ubora huo. Mfano Tanzania kuna TBS na TFDA kwa upande wa vyakula na dawa, pia kimataifa kuna ISO hii itakupa uhakika wa kufanya biashara maana Utakuwa na uhuru wa kuingia kokote na kufanya biashara.
7. Ijue historia ya Kampuni vizuri na mapana yake kwa ujumla.
Kufahamu kampuni kiundani sio swala la ihari bali ni razima maana hii ni biashara yako hili ikitokea la kutokea ujue wapi pakuanzia. Hapa nakushauri utambue kuwa kampuni hiyo ilianzishwa na nani, wapi, mwaka gani, imesambaa kiasi gani na kama ni ya nje iliingia lini nchini mwako na imesajiliwa lini na je vibari vya usajili vipo? Ukiweza kuyajua hayo basi unakuwa katika kipindi kizuri cha ufanyaji wa biashara.
8. Mfumo wa upandaji ngazi/vyeo.
Katika biashara ya mtandao kuna vyeo ambavyo utolewa kwa kuzingatia vigezo fulani fulani vya utendaji kazi. Sasa basi nakushauri kabla hujajiunga na kampuni yoyote akikisha unafahamu ni jinsi gani utapanda cheo, kumbuka unavyo panda cheo ndivyo jinsi na gawio lako linaongezeka, hivyo lazima uwe makini usije ukakurupuka mwishowe ukaja kujuta.
Mwisho napenda nikwambie kuwa biashara ya mtandao ni nzuri sana kuliko biashara yoyote ile apa duniani kwa sasa ila usipozingatia hayo mambo nane niliokueleza hapo juu basi utajikuta unapoteza pesa, muda na mwisho wa siku unajuta. Na mimi sipendi mwanafunzi wangu ajute nataka kila mtu awe mshindi daima.
Napenda nikukaribishe katika mada zinazokuja mbeleni, hivyo endelea kufuatilia ukurasa huu ili ujifunze mengi, nitakuletea mada juu ya MAKOSA WANAYOYAFANYA WAFANYA BIASHARA YA MTANDAO. Hivyo endelea kufuatilia na nakushauri uwashilikishe na wengine kwa kushare hili na wao waweze kujifunza mbinu hizi.
Ni mimi Mkufunzi na Mshauri wako wa maswala ya biashara, Frank A. Ndyanabo
Waweza kuwasiliana nami kupitia namba +255 785 494 456 au ukatembelea www.fancompany.blogspot.com.
Comments
Post a Comment