ZINGATIA HAYA KILA SIKU.
ZINGATIA HAYA KILA SIKU.
Yaweza kuwa unayafahamu ila hujui umuhimu wake, au unajua ila unayachukulia kawaida sana. Lazima ufikie mahali ujiulize ni kwa kiasi gani unazitumia mbinu hizi kimaendeleo. Hizi ndio waswahili usema "nondo nzito" ila mimi nasema ni "funguo tatu muhimu katika maisha yako" funguo hizi ukipoteza moja wapo basi usitegemee muujiza, Maana mafanikio hayamfuati mtu kama muujiza bali mtu mwenye ndio uyafanya yamtokee kama muujiza kwake. Na funguo hizi ndio za kutumia ili ufikie pale ulipopalenga.
MTANGULIZE MUNGU KILA SIKU:
Najua kila mtu ananjia yake ya kuabudu, uwe Mwislam au mkristu unamuabudu Mungu alie juu, basi tambua kuwa ata uwe mjanja namna gani Mungu ndio kilakitu. Huwezi kufanikiwa bila kumuweka mbele. Nakumbuka wakati nikiwa shuleni, na nikiwa kiongozi wa dini kwa wanafunzi kimkoa tulikuwa na usemi wetu kuwa "God.... first, education..... Second" hii inamaana kuwa katika mambo yote utakayoyafanya lazima Mungu umtangulize.
Ni wakati gani wa kumtanguliza Mungu. Hakikisha kuwa kila asubuhi kabla ujatoka kitandani Mshukuru kwa ulinzi wake wa Usiku huo na Muombe akupatie tena neema na riziki katika siku hiyo mpya. Pia ukiingia kazini kabla ya kuanza kutenda kazi, Muombe tena Mungu wako anyooshe mkono juu ya kazi yako unayoenda kutenda kwa siku hiyo, na ukiimaliza Mshukuru pia. Usiku kabla ya kwenda kulala akikisha unamshukuru na kumuomba ulinzi wake juu yako na familia yako.
Pia akikisha unamuonyesha Mungu uwepo wake kwako kwa vitendo, kwa kushiliki katika nyumba za ibada kwa kwenda msikitini au kanisani. Na hakikisha unatoa sadaka yako kwa kuwasaidia wasio na uwezo. Kwa kufanya hayo yote utaona jinsi Mungu atakavyo shusha Neema maishani mwako.
PITIA NDOTO ZAKO KILA SIKU:
Huu ni ufunguo mwingine wa kutumia kila siku. Watu wengi hatufanyi hiki kitu maana tunaishi kwa mazoea. Kumbuka Ukiweza kupitia ndoto zako kila siku utapata picha kuwa umeweza kufanikiwa au umepiga atua kiasi gani mpaka Sasa katika kutekeleza ndoto yako hiyo na uongeze nguvu kiasi gani.
Na watu tunashindwa kutekeleza hili kutokana na kuwa wengi hatuna ndoto, bali tunaishi tu bola liende, ata kama una ndoto lakini hujaziandika, kwaiyo ata nikikwambia uzipitie utapitia nini, maana apo tu nikikwambia nitajie ndoto zako za mwaka huu, unamambo miamoja kidogo na yako kichwani, na yanabadilika kila kukicha.
Ukitaka ufanikiwe kimaisha akikisha unaandika ndoto zako katika diary yako na kila siku zisome, husiwe kama ndege au wanyama ambao wanaishi tu bila kujua kesho kutatokea nini, ila wewe ni mwanadamu mwenye utashi kesho yako unaweza kuitengeneza leo na ukajua nini kitatokea. Sasa basi utumie ufunguo huu wa kuzisoma ndoto zako kila siku. Au ukiona ni ngumu, ziandike katika karatasi kisha zibandike nyuma ya mlango, ili kila ukitoka ndani kwenda kazini unaziona na ukirudi unaziona. Hii itakusaidia kukupa molali ya kufanya Kazi ili uzitimize na itakusaidia kukuzuia Kutofanya mambo bila mpangilio.
TEKELEZA WAJIBU WAKO KILA SIKU:
Najua unamajukumu mengi ya kufanya kila siku,na moja kati ya hayo ni jukumu la kufanya kazi na kutimiza ndoto yako. Sasa hivi kauli mbiu ya Tanzania ni "Hapa kazi tu" hii kauli naipenda sana maana Inakupa picha kuwa kila siku lazima uwajibike, na sio kukaa tu kulalamika kuwa maisha magumu uku umekaa tu. Serikali haiwezi kukuletea pesa nyumbani kwako bali yakupasa utoke na uyatafute maisha kwa kufanya kazi.
Na maandiko yanatwambia, "hasiyefanya kazi hasile, na tafuta utapata " hii maana yake Ukiweza kutimiza wajibu wako basi lazima ufanikiwe, haiposehemu inayosema kaa tu nyumbani mafanikio yatakukuta. Kama unaitaji ufunguo huu ukuletee maendeleo basi timiza wajibu wako wa kila siku. Kama ni kazi fanya kwa bidii zote, kama ni biashara fanya kwa nguvu zako zote, kama ni mwanafunzi basi soma kwa bidii. Sipendi mtu aje kujuta kwa sababu alishindwa kutumia nafasi yake kikamilifu na wakati uwezekano ulikuwepo wa kufanya hivyo.
Tumia funguo hizi kwa makini ninahakika utafanikiwa bila shaka.
~Frank A. Ndyanabo
+255 785 494 456
Comments
Post a Comment