- Get link
- X
- Other Apps
ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI
Nanasi ni mojawapo ya matunda niyapendayo sana. Ni matamu, yana maji mengi, na ladha iliyo kamili. Nimeona ni vizuri kuweza kuchangia mawazo yangu juu ya faida kubwa za kula nanasi kwa wingi ili kuweza kuboresha afya yako. Cha msingi zaidi, nanasi hutumika kama dawa ya kuulinda mwili mwako. Tuangalie faida moja moja za nanasi kwa mwili wako: 1.Kuondoa Uvimbe . Nanasi ina kimeng’enya kinachoitwa bromelain, kinachosaidia kutibu vitu mbalimbali mwilini lakini ni madhubuti kwa kupunguza uvimbe wa ngozi kutokana na maambukizi au vidonda. Bromelain ni madhubuti pia katika kupunguza mauvimu ya viungo au uvimbe sugu. Kimeng’enyo hiki pia kina kemikali zinazosaidia kuangamiza seli za uvimbe mwilini. 2.Kuongeza kinga ya mwili . Nanasi lina vitamin C kwa wingi pamoja na vitamin A, B1, B6, nyuzinyuzi (fiber), calcium, phosphorous na potasiam. Nanasi husaidia kuimarisha mifupa kutokana kuwa na madini ya manganese, ambayo hutumika mwilini kujenga tishu (connective tissues) na mifu...
Comments
Post a Comment