MATENDO NI TIBA YA WOGA.

MATENDO NI TIBA YA WOGA.

Hii ndio dawa pekee ya kutibu ugonjwa wa woga ndani yako.  Pindi tunapotaka kufanya jambo fulani utakuta tunakabiliwa na woga. Woga ni kitu kibaya sana katika maisha yetu ya kila siku. Jiulize ni mambo gani umeshindwa kuyafanya kwa sababu ya woga.

Siku zote ukitaka kushinda jambo kwanza ondoa woga ndani yako.  Na ili kufanikisha jambo lako jiulize ni kitu gani ufanye ili kukabiliana na woga uliopo ndani yako. Jibu utakalolipata litumie kukabiliana na adui huyo woga.  Utakuwa umepata muarobaini wa mafanikio yako.

Weka mfumo mpya sasa wa maisha yako, utakaokupa mwanga sahihi katika maisha yako.  Utakuwa umekutana na fursa nyingi katika maisha yako ila woga umekufunika na kuiteka akili yako.  Sasa ni wakati wa kukataa hali hiyo na kuamua kutenda. Nyanyuka tutembee pamoja sasa.

By: Frank A. Ndyanabo - FAN

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG