UMRI WAKO SIO KIKWAZO.

Watu wengi tumekuwa tukipata kigugumizi juu ya maamuzi yetu katika kuzielekea ndoto zetu.  Wapo tunaofikiria umri wetu kutujengea vikwazo mbele yetu. 

Umri wako kuwa mkubwa sio sababu ya kukuzuia kutimiza ndoto yako.  Nimekuwa nikikutana na watu mbali mbali na kuwashirikisha juu ya fursa za kuwaletea maendeleo lakini hutanguliza swala la umri mbele.  Utasikia mtu anakwambia, "mimi umri umekwenda nimeisha jichokea na karibia nitakufa"  Aliyekwambia utakufa kesho au baada ya mwaka mmoja ni nani?  Umri wa uzalishaji kwa mwanadamu hasa Tanzania ni miaka 60.  Sasa utakuta mtu ana miaka 40 anakwambia umri wake umeenda na hawezi kufanya jambo lolote kwa sababu ya umri.  Sasa kama una miaka 40, hujui kuwa bado una miaka 20 mbele?  Kwa maana hiyo umeisha tumia 50% ya maisha yako katika utafutaji hapa duniani. Toka ulivyo timiza miaka 20 nakuanza kujitengenezea maisha, ulikuwa na jukumu la miaka 40 mbele, hivyo bado unadaiwa asilimia 50 mbele yako.  Sasa ili uweze kutimiza hiyo asilimia 50 unahitaji kujituma nakujiona bado kijana kabisa mwenye matarajio makubwa ya kusonga mbele zaidi.  Amka leo acha kufikiria kuwa umri wako huo ni kikwazo.

Umri wako kuwa mdogo sio sababu ya kukuzuia kutimiza ndoto yako.  Vijana wengi wa kileo utakuta anakwambia mimi bado kijana nakula ujana.  Unakulaje ujana huku ukiwa hujui kesho yako itakuwaje.  Mbali na hao wapo ambao wanajiona bado wadogo kabisa kuanzisha biashara kubwa kwa kigezo cha umri.  Aliyekwambia makampuni yanamilikiwa na wazee ni nani?  Umri mdogo ndio nafasi pekee uliyonayo leo kuhakikisha maisha yako yananyooka baadae, usikae na kubweteka na kuridhika na maisha uliyonayo kisa unajiona mtoto.  Kuna wenzako wamekuwa mabilionea wakiwa na umri mdogo kabisa, mbali na hapo kuna watu wanamiliki makampuni na biashara kubwa ila ukiangalia umri wao ni chini ya miaka 25. 

Kitu cha msingi ni kujipima uko wapi kiumri na kisha toa katika miaka 60 alafu tazama imebaki mingapi.  Ukisha pata jibu jiulize ni umri mkubwa mbele au mdogo.  Na baada ya hapo  tafakari kwanini usitie juhudi na nguvu badala ya kukaa na kulalamika kuwa maisha magumu na mwisho wa siku umri ukiisha unaanza kujuta!

Chukua hatua stahiki kwa manufaa yako ya baadae.
By. Frank A Ndyanabo - FAN
+255 785 494 456

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG