UNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA BINTI GETRUDE CLEMENTI?
UNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA BINTI GETRUDE CLEMENTI?
Getrude Clement ni binti kutoka Jijini Mwanza, nchini Tanzania. Na anasoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Mnarani, ilioko nje kidogo ya mji takribani km 10 au zaidi kutoka mjini. Shule iyo ni ya serikali ni moja kati ya shule za kata zilizoanzishwa kipindi hicho.
Getrude ana umri wa miaka 16. Alipata fursa ya kipekee kuongea kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa, akikaribishwa na Mhe. Ban Ki Moon, katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kama muwakilishi wa watoto na vijana wote duniani kwa ajili ya kuzungumzia maswala ya mazingira na uchafuzi wake.
Baba yake ni Kinyozi na mama yake ni mfanya biashara mdogo mdogo wa nyanya na vitunguu.
Getruda Clement, aliweza kuushangaza ulimwengu jinsi alivyo simama mbele ya viongozi mbali mbali nakuweza kuhutubia bila wasi wasi na kwa kujiamini kupita kiasi.
Ujasiri alio nao binti huyu ndio umenifanya niandike maneno haya ili uweze kujifunza kitu fulani. Wewe kama mfuatiliaji mzuri wa makala zangu Utakuwa unakumbuka makala niliowai kuiandika hapa yenye kichwa cha habari, "UMRI WAKO SIO KIKWAZO "
https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1317959224900692&substory_index=0&id=1241654279197854 bonyeza link hiyo apo juu uitazame na kuisoma zaidi tena.
Baada ya kuisoma hiyo basi utagundua kuwa wengi tunashindwa kufanya mambo kwa kuhofia umri wetu.
Binti huyu bila kujali umri wake na watu walio mbele yake alisimama kidete na kutimiza azma yake. Utagundu kuwa tunashindwa kufanya mambo makubwa kwa sababu ya woga,niliandika pia juu ya tiba ya woga, ebu soma hapa chini kwa kubofya link hii https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1328090020554279&substory_index=0&id=1241654279197854
Mwisho nakwambia kuwa, malengo na matarajio yako yatatimia endapo tu, utaamua kuacha kisingizio cha umri wako na utaondoa woga rohoni mwako.
By, Frank A. Ndyanabo - FAN
Comments
Post a Comment