ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO.
ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO.
SEHEMU YA 2.
Karibu katika mwendelezo wa mada yetu iliyotangulia ikiwa na sehemu ya kwanza na leo tuko katika sehemu ya pili.
Kila mtu anatamani maisha yake yabadilike kutoka alipo na kusonga mbele zaidi. Ila maisha hubadilika pale tu unapotaka yabadilike. Na ili yaweze kubadilika lazima ukubali kupigika kwa ajili ya kuyafanya yabadilike. Huwezi kulala na kuamka ukakuta yamebadilika.
Kwa leo hebu tujifunze njia zingine :
6. Achana na mahusiano yenye kukuumiza.
Watu wengi naweza sema ni ving'ang'anizi kwa mambo yasiyo na tija. Haimaanishi kuwa, kwakuwa umekuwa na mtu au umekuwa ukifanya jambo fulani kipindi cha nyuma basi ni lazima uwe nae au uendelee na mambo hayo maishani mwako.
Kukosa jambo fulani ulilolizoea haimaanishi kuwa lazima ulipate. Au kumkosa mwenzako aliye kuumiza hapo awali haimaanishi kuwa lazima uwe nae maishani mwako.
Kukikosa kitu cha awali ni nafasi nzuri kwako kupata muda wa kusonga mbele kwa mikakati mipya. Hupaswi kusononeka kwa kukosa kazi au kushindwa kwa mikakati yako. Cha msingi yasahau na anza maisha upya.
7. Mshukuru Mungu kwa kile ulichonacho.
Hii inaitwa, shukuru kwa kila jambo,hili ni jambo ambalo yawezekana ulikuwa hulifahamu au unalifahamu ila hujui umuhimu wake. Hebu bonyeza link hiyo hapo chini uone, thamani ya shukrani https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1242857949077487&id=1241654279197854
Hata wakati ambapo mambo ni magumu huna budi kumshukuru Mungu na tambua ya kuwa mazuri yote bado ni yako. Mtangulize Mungu kwa kila jambo.
8. Tenga muda maalumu kila siku kwa ajili yako.
Najua unajiuliza swali, kivipi? Tambua kuwa kila siku unahitaji muda wa kukaa peke yako bila bugudha yoyote na kuanza kutafakari juu ya maisha yako. Huku ukijiuliza ni wapi unashindwa na wapi umekwama katika maisha na mbinu gani uzitumie kujinasua katika makwamo hayo. Wakati huu ndio wakati wa kujionyesha upendo mwenyewe maana utakuwa ukizungumza na nafsi yako mwenyewe na kujishauri na kujipatia muongozo sahihi wewe mwenyewe. Utajionyesha upendo wa dhati maana hautakuwa tayari kuacha nafsi yako iteketee Kizembe.
9. Endelea kujifunza.
Msingi wa mafanikio yako unatokana na kushindwa kwako hapo nyuma. Maisha yako mazuri yatatokana na juhudi zako binafsi kwa kupambana na vikwazo vyote vilivyo mbele yako.
Utukufu wako unatokana na kupondeka kwa nafsi yako. Simama imara na songa mbele, jifunze kila kukicha. Hata kiangazi hugeuka kuwa masika, majira siku zote hubadilika.
10. Furahia pale ulipo.
Hili nalo ni tatizo, kuna watu hawafurahii maisha waliyonayo na badala yake hupoteza muda wakiwaza mambo yaliyopo mbele yao kiasi kwamba hukosa muda wa kukaa na kufurahia maisha waliyonayo.
Kule unakowaza kwenda una uhakika gani kama utafika? Na itakuwaje kama hautafika? Sasa basi furahi kuwa hapo ulipo. Waswahili usema, "raha jipe mwenyewe " Furahia maisha yako sasa, na huo ndio wakati wako, na sio kesho.
MWISHO:
Baada ya kuyaona hayo nina imani umejifunza mengi kutoka kwangu, na ili kushare furaha yangu, nakualika uweze kushare makala hii ili na wengine waweze kujifunza zaidi.
https://m.facebook.com/Frank.A.Ndyanabo/
By. Frank A. Ndyanabo - FAN
Comments
Post a Comment