UMUHIMU WA BUSINESS PLAN KWA MFANYABIASHARA
UMUHIMU WA BUSINESS PLAN KWA MFANYABIASHARA. Business Plan (mpango biashara) ni nini? Business Plan ni taarifa iliyoandikwa ambayo huonyesha lengo la biashara husika kwa kuonyesha hatua muhimu za kupitia ili kufikia lengo. Hapa unapata picha kuwa, ni wapi ulipo, unaenda wapi na jinsi gani utafika ulipo kusudia kufika. *Umuhimu wa business plan kwa mfanya biashara.* Tuangalie umuhimu wa mpango biashara kwa mfanya biashara. Mpango biashara ina umuhimu mkubwa sana kwa mfanya biashara /mjasiriamali yeyote ambapo faida zake ni kama ambavyo tutazitazama hapa chini. i) Humsaidia mfanya biashara kuepukana na uwezekano wa kuingia katika biashara yenye uwezekano wa kufa. Kama tulivyo ona katika makala zetu zilizo tangulia, business plan inakuwa kama ramani ya kukuonyesha njia sahihi ya kupitia. Hivyo ukiitumia kwa usahihi utakuwa na biashara au mradi endelevu. ii) Humsukuma mfanyabiashara kuongeza umakini katika usimamizi wa biashara yake. Muda, juhudi, utafiti na nidhamu hutumika ha...