UMUHIMU WA BUSINESS PLAN
*UMUHIMU WA BUSINESS PLAN.*
Business Plan (mpango biashara) ni nini?
Business Plan ni taarifa iliyo andikwa ambayo huonyesha lengo la biashara husika kwa kuonyesha hatua muhimu za kupitia ili kufikia lengo.
Hapa unapata picha kuwa, ni wapi ulipo, unaenda wapi na jinsi gani utafika ulipo kusudia kufika.
*Umuhimu wa business plan*
i) Mpango huo unaelezea njia ambayo mfanya biashara au mjasiriamali anayopaswa kupitia kipindi chote cha uendeshaji wa biashara yake. Katika biashara lazima kuwepo na kanuni na taratibu, hivyo basi ili biashara yako ikue lazima kuwe na njia unazopaswa kupitia, na kupitia business plan kila kitu kitakuwa kimejipambanua humo.
ii) Husaidia wawekezaji, watu wa mabenki na wafadhili wengine kuelewa na kumkubali mfanya biashara kwa ajili ya uwekezaji wao katika biashara yake. Lazima utambue kuwa popote utakapo hitaji kwenda kupata msaada wa kuongeza mtaji (mkopo) kwa ajili ya kukuza biashara yako lazima uwe na mpango kazi huu ili kumuwezesha huyo anayetaka kuwekeza kwako au kukupatia mkopo kuona ni kwa kiasi gani unaweza kunufaika na huo mkopo.
iii) Mpango kazi mzuri utakusaidia kukuza biashara yako kirahisi maana inasaidia kuwaonyesha wafadhili wako kuwa soko la bidhaa zako lipo, na usimamizi wa biashara yako upo imara kwa ajili ya kutoa huduma nzuri.
iv) Business Plan nzuri humsaidia mfanya biashara kupunguza gharama zisizo za lazima na kuepusha uwezekano wa biashara yake kushindwa kuendelea.
v) Humsaidia mfanyabiashara kujiendeleza kiutawala na kiujuzi.
vi) Hutumika kama kiunganishi kati ya mfanya biashara na wadau mbali mbali. Mpango biashara huchukua nafasi kubwa katika kujipambanua kwa watu mbali mbali maana hutoa ufafanuzi wa kina juu ya biashara yako.
"Kufanya biashara bila mpango kazi ni sawa na kuendesha gari isiyo na taa gizani"
Kwa Mawasiliano zaidi juu ya uandishi wa BUSINESS PLAN zenye ubora wasiliana na Nyumbani Business Plan LTD kupitia mawasiliano yaliyotolewa hapo chini.
fb: Nyumbani Business Plan LTD
Instagram : @nyumbanibusinessplanltd
Email: nyumbanibusinessplan@gmail.com
Comments
Post a Comment