UMUHIMU WA BUSINESS PLAN KWA MFANYABIASHARA

UMUHIMU WA BUSINESS PLAN KWA MFANYABIASHARA.

Business Plan (mpango biashara) ni nini?

Business Plan ni taarifa iliyoandikwa ambayo huonyesha lengo la biashara husika kwa kuonyesha hatua muhimu za kupitia ili kufikia lengo.

Hapa unapata picha kuwa, ni wapi ulipo, unaenda wapi na jinsi gani utafika ulipo kusudia kufika.

*Umuhimu wa business plan kwa mfanya biashara.*

Tuangalie umuhimu wa mpango biashara kwa mfanya biashara.

Mpango biashara ina umuhimu mkubwa sana kwa mfanya biashara /mjasiriamali yeyote ambapo faida zake ni kama ambavyo tutazitazama hapa chini.

i) Humsaidia mfanya biashara kuepukana na uwezekano wa kuingia katika biashara yenye uwezekano wa kufa.

Kama tulivyo ona katika makala zetu zilizo tangulia, business plan inakuwa kama ramani ya kukuonyesha njia sahihi ya kupitia. Hivyo ukiitumia kwa usahihi utakuwa na biashara au mradi endelevu.

ii) Humsukuma mfanyabiashara kuongeza umakini katika usimamizi wa biashara yake.
Muda, juhudi, utafiti na nidhamu hutumika hapa kwa ajili ya kumuongoza mfanya biashara afike mahala sahihi alipokuwa anahitaji kufika.

iii) Uchunguzi na usimamizi wa mikakati ya biashara husika ni muhimu sana na husaidia kutoa taswira njema kwa watu wa nje.  Mikakati yote hii huonyeshwa kwenye business Plan.

iv) Husimama kama kipimo cha mafanikio katika biashara yake, hii ni kutokana na kuwa, dira na malengo huonyeshwa kwenye business Plan.

v) Business Plan hutumika kama njia ya mawasiliano kati ya mfanyabiashara na wadau mbalimbali wa nje.

vi)  Hutumika kama nguzo ya utawala katika kuelekea mafanikio.Huo ndio ukamilifu wa business plan.

vii)  Humsaidia mfanya biashara kujua changamoto za kiuchumi, tafiti za kifedha na ushindani wa kiuchumi kwa ajili ya kusaidia kukua kwa biashara.  Haya yote huainishwa katika business Plan.

"Kufanya biashara bila mpango kazi (business Plan) ni sawa na kuendesha gari isiyo na taa gizani)

Facebook : Nyumbani Business Plan LTD

Instagram: @nyumbanibusinessplanltd

Email : nyumbanibusinessplan@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

ZIFAHAMU FAIDA ZA NANASI KAMA DAWA MWILINI

FAIDA KUMI ZA MAPERA MWILINI.

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG