MAMBO MATANO (5) AMBAYO HUPASWI KUFANYA KAMA UNAHITAJI MAFANIKIO.
MAMBO MATANO (5) AMBAYO HUPASWI KUFANYA KAMA UNAITAJI MAFANIKIO.
Habari yako ndugu msomaji wa makala hii. Leo nakuletea mambo ambayo yatakuwa chachu kwako wewe ambae kila siku unandoto za kuwa bilionea au mjasiriamali mwenye mafanikio.
Najua una mambo mengi unayoyafahamu juu ya ujasiriamali ambayo mengi unatoa kwangu Frank A Ndyanabo, na mengine umeyapata kutoka kwa wengine au kupitia makala na vitabu mbali mbali.
Leo nataka nikupe kitu muhimu sana ambacho sijawai kukupatia, mbali na mambo ambayo unapaswa kuyafanyia katika harakati zako lakini leo nakupa mambo hupaswi kuyafanya kama una ndoto za kufanikiwa katika maisha yako. Na mambo haya mimi Frank nimejaribu kuyafanyia tafiti na kugundua kuwa ni mambo mazuri ivyo nikaona ni bora nikushilikishe na wewe rafiki yangu mpendwa.
Mambo hayo ni mengi sana ila kwa leo nimeona nikushilikishe aya matano maana ndio yameshiba zaidi.
1. KUTOKURUDIA KOSA.
Kurudia jambo ambalo awali lilishindika ni kosa kubwa maana huwezi kufanikiwa atakidogo. Mfano chukulia mtu ambae Ulikuwa nae katika mahusiano kisha mkaachana, ikitokea leo mkarudiana mtafanikiwa katika safari yenu?
Ni jambo gumu sana kutegemea mafanikio makubwa katika jambo lilelile ambalo haijabadilika. Ata katika biashara yako ambayo uliwai kuifanya kisha ikakushinda, huwezi kuirudia itafanikiwa ikiwa bado ni ileile, unachopaswa kufanya ni kuachana nayo kisha kujikita katika mambo mengine mapya.
2. KUTOKUJIULIZA KWANINI UNAFANYA JAMBO FULANI.
Hii kitu ndio utofautisha kati ya matajiri na masikini. Sasa basi na wewe kama unataka kuondoka katika mtego huu basi husifanye kosa hili. Kila jambo unayoyafanya lazima ulitathimini lina manufaa gani kwako.
Usikubali kuwa kila kitu kinachotokea maishani mwako basi unafanya tu, jaribu kuwa mtu wa kuuliza na kutafakari. Wale wote waliofanikiwa hawafanyi kosa hili maana hawataki kupoteza ndoto zao.
Usiwe kama bendela fuata upepo wewe kila upepo ukipuliza mashariki, magharibi au kusini basi na wewe unafuata. Jiulize mala mbilimbili kwa kila kinachotokea usije ukajikuta ndoto zako zinaishia hewani.
3. KUJISAHAULISHA KUWA FIKRA ZAO ZA NDANI HUTOA TASWIRA YA NJE.
Hivi ulisha jiuliza kwanini unaishi maisha hayo na si maisha ya Bakari wala Amina? Kila mtu anaishi kulingana na mtazamo wake wa ndani.
Kama unataka kufanikiwa basi husizibe masikio na kuifunga akili yako kuwa kila kitu kinatokea kwa bahati nasibu tu. Utakuwa unajidanganya.
Tambua kuwa mafanikio yako yanatokana na mtazamo wako wa ndani. Kama akilini mwako hufikilia wala kutamani kufanikiwa basi huwezi kuyapata mafanikio kama ajali, wale wote unaowaona wamefanikiwa ni kutokana na msukumo walionao ndani yao na kile unachokiona kwao ni tafsiri ya kilichoko ndani yao.
4. KUTOKUSAIDIA WATU.
Hili limekuwa ni tatizo kubwa mno baina yetu wajasiriamali, na hii nadhani ni kwa kutojua na ndio maana leo Frank niko apa nakuelimisha.
Katika mafanikio yoyote yale apa duniani yanatokana na watu, Maana ndio raslimali kubwa kibiashara. Na ndio maana ukitaka kufanikiwa kimaisha na kibiashara wekeza katika watu.
Tunawekezaje katika watu? Najua hili nalo ni swali la kujiuliza. Watu tunawekeza kwao kwa kuwapatia elimu ya bure kama hii, tunawekeza kwao kwa kutatua matatizo yanayowakabili, tunawekeza kwao kwa kutumia kauli nzuri kwao na mambo mengine kama hayo.
Sasa utakuta mtu kwakuwa akajiona yeye anauwezo kifedha zaidi ya wengine basi unakuta ndio hutaki kajichanganya nao na kuwadharau na kutaka kajichanganya na watu wenye uwezo kama yeye. Kumbuka ukiwa mbinafsi ata mafanikio kwako itakuwa ndoto au ukiyapata basi hayatadumu muda mrefu maana watu ambao ndio soko lako watakuwa hakuzungumzii vizuri na hawataisapot biashara yako.
5. KUTOKUWA NA MTAZAMO MKUBWA.
Watu wengi tunakuwa na Woga wa ajabu sana juu ya jambo hili. Watu wanawaza mambo madogo.
Nakumbuka wakati niko secondary niliwai kukutana na mwalimu mmoja kutoka nchi jirani, aliniambia jambo moja ambalo toka miaka hiyo uwa halinitoki kichwani. Nanukuu, "if you want to succeed in your life you have to think big and think beyond the boundaries" Yaani kama unataka kufanikiwa kimaisha basi wewe siku zote fikilia mambo makubwa, waza mbali zaidi ya ukomo. Kauli hii haitanitoka. Bado siku nyingine nikamsikiliza Mchungaji mmoja anaitwa, Pastor Chris Oyakhilome, nae anakwambia, Kuwa wa tofauti, fikilia mambo ambayo wengine wanahisi hayawezekani kabisa kufanyika.
Ukitaka kufanikiwa basi tembea katika kauli hizo. Maana unapofikiria mambo makubwa ndivyo jinsi unavyo jiweka katika mazingira ya kufanikiwa.
Sasa basi ili hacha kufanya mambo hayo matano, naamini utafanikiwa mpaka ushangae.
Kwa ushauri na elimu ya ujasiriamali ungana nasi katika project yangu ya NYUMBANI BUSINESS PLAN, au waweze tembelea www.fancompany.blogspot.com ili ujifunze mengi.
Ni mimi, Frank A. Ndyanabo
0785494456
Comments
Post a Comment