Posts

Showing posts from April, 2016

MATENDO NI TIBA YA WOGA.

Image
MATENDO NI TIBA YA WOGA. Hii ndio dawa pekee ya kutibu ugonjwa wa woga ndani yako.  Pindi tunapotaka kufanya jambo fulani utakuta tunakabiliwa na woga. Woga ni kitu kibaya sana katika maisha yetu ya kila siku. Jiulize ni mambo gani umeshindwa kuyafanya kwa sababu ya woga. Siku zote ukitaka kushinda jambo kwanza ondoa woga ndani yako.  Na ili kufanikisha jambo lako jiulize ni kitu gani ufanye ili kukabiliana na woga uliopo ndani yako. Jibu utakalolipata litumie kukabiliana na adui huyo woga.  Utakuwa umepata muarobaini wa mafanikio yako. Weka mfumo mpya sasa wa maisha yako, utakaokupa mwanga sahihi katika maisha yako.  Utakuwa umekutana na fursa nyingi katika maisha yako ila woga umekufunika na kuiteka akili yako.  Sasa ni wakati wa kukataa hali hiyo na kuamua kutenda. Nyanyuka tutembee pamoja sasa. By: Frank A. Ndyanabo - FAN

VYAKULA HIVI VITAKUSAIDIA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANYO NA KUKUA KWA TEZI DUME.

Image
VYAKULA HIVI VITAKUSAIDIA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME. Kichocheo cha testosterone au kwa Kiswahili , japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme, pia kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone upungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA, KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzi...

UMRI WAKO SIO KIKWAZO.

Image
Watu wengi tumekuwa tukipata kigugumizi juu ya maamuzi yetu katika kuzielekea ndoto zetu.  Wapo tunaofikiria umri wetu kutujengea vikwazo mbele yetu.  Umri wako kuwa mkubwa sio sababu ya kukuzuia kutimiza ndoto yako.  Nimekuwa nikikutana na watu mbali mbali na kuwashirikisha juu ya fursa za kuwaletea maendeleo lakini hutanguliza swala la umri mbele.  Utasikia mtu anakwambia, "mimi umri umekwenda nimeisha jichokea na karibia nitakufa"  Aliyekwambia utakufa kesho au baada ya mwaka mmoja ni nani?  Umri wa uzalishaji kwa mwanadamu hasa Tanzania ni miaka 60.  Sasa utakuta mtu ana miaka 40 anakwambia umri wake umeenda na hawezi kufanya jambo lolote kwa sababu ya umri.  Sasa kama una miaka 40, hujui kuwa bado una miaka 20 mbele?  Kwa maana hiyo umeisha tumia 50% ya maisha yako katika utafutaji hapa duniani. Toka ulivyo timiza miaka 20 nakuanza kujitengenezea maisha, ulikuwa na jukumu la miaka 40 mbele, hivyo bado unadaiwa asilimia 50 mbele yako....