ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO.
ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO. SEHEMU YA 2. Karibu katika mwendelezo wa mada yetu iliyotangulia ikiwa na sehemu ya kwanza na leo tuko katika sehemu ya pili. Kila mtu anatamani maisha yake yabadilike kutoka alipo na kusonga mbele zaidi. Ila maisha hubadilika pale tu unapotaka yabadilike. Na ili yaweze kubadilika lazima ukubali kupigika kwa ajili ya kuyafanya yabadilike. Huwezi kulala na kuamka ukakuta yamebadilika. Kwa leo hebu tujifunze njia zingine : 6. Achana na mahusiano yenye kukuumiza. Watu wengi naweza sema ni ving'ang'anizi kwa mambo yasiyo na tija. Haimaanishi kuwa, kwakuwa umekuwa na mtu au umekuwa ukifanya jambo fulani kipindi cha nyuma basi ni lazima uwe nae au uendelee na mambo hayo maishani mwako. Kukosa jambo fulani ulilolizoea haimaanishi kuwa lazima ulipate. Au kumkosa mwenzako aliye kuumiza hapo awali haimaanishi kuwa lazima uwe nae maishani mwako. Kukikosa kitu cha awali ni nafasi nzuri kwako kupata muda wa kusonga mbele k...