THERE IS NO FUTURE IN THE PAST. Ukitaka kufanikiwa usiangalie nyuma yako kunanini na ulishindwa mara ngapi. Siku zote kukaa Chini nakuanza kujuta kwa makosa uliofanya uko nyuma nikupoteza muda, huo muda Utumie kwa kupanga ya kesho. Bahati nzuri Mungu alitujalia kusahau, ivyo siku zote sahau ya nyuma na waza yale ya mbele yako. Maisha bora ya mbele hayawezi kuja kama akili yako imebeba kushindwa kwa nyuma. Binadamu yeyote anayeweza kupoteza muda wake wa leo kwa kulaumu mabaya ya jana, kesho atapoteza muda akilaumu mabaya ya leo. Tambua ya kuwa, "hakuna awezaye kurudi nyuma na kuanza upya, bali waweza kuanza leo na kutengeneza maisha yako ya kesho" Kadri unavyofikiria ya nyuma ndivyo unavyochelewa kufika mbele zaidi. Penda zaidi ndoto yako ya kesho kuliko historia yako ya jana,maana hatima yako siku zote iko mbele na sio nyuma. Siku zote utashindwa kwa kuendekeza mambo yaliopitwa na wakati maana utakuwa unatumia ujuzi uliopitwa na wakati. "Habari njema ya siku ni ...