Posts

Showing posts from August, 2015

DALILI ZA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO. (2)

Image
DALILI ZA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO. (2)  Karibu sana ndugmsomaji wa makala zangu za afya,nisiku nyingine tena Mwenyezi Mungu ananikutanisha na wewe ktk ukurasa huu kwaajili ya kuhabarishana mambo mbalimbali yahusuyo afya yetu. Leo tunaendelea na somo letu la ulcers(vidonda ya tumbo). Somo lililopita tuliweza kuona madhara yake na leo tutaangalia dalili zake. Katika ugonjwa huu kunaweza kusiwe na dalili za moja kwa moja lakini mara nyingi ishara zifuatazo zimekuwa zikijitokeza ivyo ni vyema kumuona daktari au mtaalamu wa waswala ya afya alieko karibu yako kwaajili ya vipimo na ushauli zaidi. Dalili hizo nikama zifuatazo: 1⃣ Maumivu makali ya tumbo kwa muda mrefu hususani nyakati ambazo muhusika hajapata chakula. 2⃣ Kutapika mala kwa mala. Hii ujitokeza mala nyingi pale vinapoanza kukomaa 3⃣ Uchovu wa mwili. Mala nyingi muhusika huanza kujihisi uchovu usio na msingi ata bila kufanya kazi yoyote mwili uhisi uchovu. 4⃣ Kukosa hamu ya chakula 5⃣ Kupungua kwa uzito. Marany...

SHINIKIZO LA DAMU HUSABABISHWA NA NINI?

Image
SHINIKIZO LA DAMU HUSABABISHWA NA NINI? AINA YA KWANZA: Asilimia 90-95 sababu huwa hazijulikani na kitaalamu huitwa primary or essential hypertension. Ingawa vitu vifuatavyo vimehusishwa kupelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu. Navyo ni: -Uvutaji sigara -Unene (visceral obesity) -Unywaji wa pombe -Upungufu wa madini ya potassium -Upungufu wa vitamin D -Umri mkubwa -Chumvi na madini ya sodium kwa ujumla -Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin) -Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin AINA YA PILI: Asilimia 5 huwa na sababu dhahiri zinazopelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu na huitwa kitaalamu secondary hypertension. Na sababu hizi ni: -Hali ya kukosa hewa usingizini (sleep Apnea) -Kasoro ya kuzaliwa nayo katika mshipa mkubwa wa damu (Coarctation of Aorta) -Saratani za figo (wilm’s tumor, renal cell carcinoma) -Saratani ya tezi iliyo juu ya figo (pheochromocytoma) Ujauzito – wapo wakina mama wajawazito ambao hupata shinikizo la damu na huwa...

MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO

Image
MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO. Karibu sana ndugu msomaji wa makala zangu za afya, nisiku nyingine tena Mwenyezi mungu ananikutanisha na wewe katika ukurasa huu kwaajili ya kukuhabarisha mambo mbalimbali yahusuyo afya yetu. Kama kawaida Naitw Frank A. Ndyanabo,leo tutaangalia zaidi madhala ya ugonjwa ulcers(vidonda vya tumbo). Niugonjwa unaoshika kasi Tanzania na duniani kwa ujumla ambayo unatokana na mifumo ya maisha yetu. VIDONDA VYA TUMBO: Huibuka baada ya kutokea vidonda kwenye kuta za utumbo mwanadamu ambavyo utokana na kuzidi kwa kiwango cha tindikali yenye kazi ya kuyeyusha chakula kiingiacho mwilini. Endapo mgonjwa hata patiwa tiba mapema uweza kusambaa zaidi adi kufikia mishipa ya damu na kupelekea madhara makubwa zaidi katika mwili. Ugonjwa huu usababishwa na mambo mbalimbali yanayotokana na tabia zetu za kila siku ikiwa ni vyakula tunavyokula,lakini kitaalamu ujonjwa huu usababishwa na bakteria ajulikanae kwa jina la Helicobacter pylori. MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBA...

UNATAKA KUBADILI MAISHA YAKO KWA KUONGEZA KIPATO CHAKO?

Image
UNATAKA KUBADILI MAISHA YAKO KWA KUONGEZA KIPATO CHAKO? Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu. Leo uko na mimi apa Frank A. Ndyanabo, mkufunzi wako wa kila siku katika ujasiliamali wenye tija katika maisha yako ya kila siku. Najua wengi wetu tumekuwa na maisha magumu kwa kuwa na vipato visivyo tosheleza maitaji yetu ya kila siku. Leo nitakupatia njia rahisi itakayo weza kubadili maisha yako kutoka chini kwenda juu endapo utazingatia mambo ayo nakuyafanyia kazi. Kwanza tuangalie mambo aya ambayo ndio kiini cha mada yetu leo: 1⃣ Employment(ajira) 2⃣ Self employed(ajira binafsi) 3⃣ Business owners(wamiliki wa biashara) 4⃣ Investors(wawekezaji) Wengi wetu tuko katika kundi number 1 na 2 na tunatamani kuwa kwenye number 3 na 4 Sasa basi jiulize ni shida gani unakumbana nazo katika ajira yako kila siku. Apa kila mtu anaujua uchungu wake kulingana na ajira alio nayo. Katika ajira kuna mambo mengi ambayo yanapelekea watu wengi tunashindwa kutimiza ndoto zetu. Maana waajili w...

WACHINI HAWEZI KUMSAIDIA WA JUU.

Image
Katika maisha ya kawaida hii inaweza kukushangaza kuona kuwa alieko chini ataendelea kuwa chini daima kama hatapata msaada wa kumtoa alipo. Kuna msemo wawenzetu kuwa kuwa,"down people can't help the down people,but  up people can help the down people" Kauli hii inauzito sana ndani yake,yaani haipo ata siku moja alieko chini aweze kumnyanyua mwenzake aloeko chini bali mtu alieko juu ndiopekee awezae kumnyanyua alieko chini. Sasa basi ukitaka kufanikiwa katika jambo fulani lazima utafute yule aliekwisha fanikiwa katika jambo lile ndio utaweza pata muongozo maana ukimtafuta mtu hasie faamu jambo lile atakupoteza. Yawezekana umekuwa ukitaka kufanya biashara fulani ila sasa hujui uanzie wapi,chakufanya tafuta watu waliokwisha kutangulia na waliofanikiwa katika biashara iyo watakupa muongozo sahii. Kwa mafunzo mengi zaidi juu ya mafanikio nitafute whatsapp au piga/text +255785494456 Waweza pia tuma email address yako ili nikutumie masomo ayo moja kwa moja

KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA BIASHARA YA MTANDAO

Image
KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA BIASHARA YA MTANDAO. Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu za kila siku,natumai ukosalama kabisa. Leo nataka nikupe siri kwanini watu wengi wanashindwa kufanya biashara hii ya mtandao. Biashara ya mtandao mala nyingi huusidha bidhaa kwa makampuni yalio mengi na machache uhusisha uduma. Sasa leo tujikite katika aya yanayohusika na usambazaji wa bidhaa. Walio wengi wanapoingia ubia na makampuni ukosa kuzingatia ile dhana ya msingi ya mtandao, WATU UANZA KUWAZA KUUZA BIDHAA ILI KUPATA FAIDA YA REJAREJA,BADALA YA KUWAZA KUTENGENEZA MSULULU WA WATU KATIKA MTANDAO. Unapo ingia tu katika biashara ya mtandao na kuanza kuwa muuzaji badala ya kutengeneza network basi wewe utofautiani na mtu anaefanya biashara ya kizamani ya uchuuzi. Biashara ya mtandao sio uchuuzi wa bidhaa bali ni utengenezaji wa mtandao. Unapokuwa ume waunganisha watu ni kazi yako sasa kuwafundisha na kuwaelekeza kuwa wao katika biashara ya mtandao ni watumiaji wa mwisho wa bidh...

MUUJIZA WA BIASHA YA KISASA BILA MTAJI

Image
Biashara nyingi zinafanyika ila biashara ya kisasa inamuujiza wake ambao watu wengi hawaugundua. Biashara ya kisasa ni ipi? Biashara hii ndio wengine wanaita biashara ya mtandao au network marketing kwa lugha ya wenzetu. Biashara hii ni mfumo wa ufikishaji uduma kutoka kiwandani na kwenda kwa mtumiaji wa mwisho moja kwa moja kupitia kwa mtu tunaemuitata msambazaji(distributor). Msambazaji uyu anakuwa ameingia ubia na kampuni husika kwa gharama Kidogo. Pia anaruhusiwa kuwashilikisha watu wengine katika mfumo huu. Ivyo basi biashara hii muujiza wake uko Katika mambo aya yafuatayo: 1. OPT-Other People's Time Hii Maana yake msambazaji anatumia muda wa watu wengine kujitengenezea pesa. Akisha unganisha watu nakuwafundisha jinsi ya ufanya biashara basi anawaacha na  wao waweze kujiendesha kwa kutumia muda wao. kwakufanya ivyo watakapokuwa wanatumia muda wao kufanya kazi basi yule msambazaji aliewafundisha atakuwa analipwa kutokana na utendaji kazi wao. 2. OPM-Other People...

KWANINI HUNA FURAHA?

Image
KWANINI HUNA FURAHA? Ulishawai jiuliza kwanini watu wengine wanaamka  saa nne asubuhi wakiwa na furaha moyoni mwao na wewe unaamka saa 11 alfajili kuwai kazini ukuukiwa umenuna na kusononeka rohoni mwako? Sasa basi wakati ndio huu wakurudisha furaha yako kwa kuungana na mimi ili nikuonyeshe fursa itakayokufanya uwe na furaha ya kudumu moyoni mwako. Nitakufundisha BURE mbinu za kuongeza kipato chako na jinsi ya kubadili maisha yako. Pia nitakuonyesha fursa mbalimbali unazoweza kutumia ndani ya karne hii na kubadili maisha yako kwa mtaji mdogo kabisa. Hupaswi kuwaza wasiliana nasi kupitia number hii apa chini,tupigie muda wote au tuma text au kama unatumia whatsapp unaweza pia kutupata kupitia namba hiyo. TAMBUA MSTAKABALI WA MAISHA YAKO UKO NDANI YAKO MWENYEWE SIO KWA NDUGU AU RAFIKI. NA KUMBUKA USIPO BADILIKA NA KUFANYA MAAMUZI LEO HAKUNA ATAKAEKUBADILISHIA KESHO. NI ZAMU YAKO SASA. Number ni 0785 494 456