Posts

HABARI NJEMA KWAKO MWANA DAR ES SALAAM

Image
HABARI NJEMA KWAKO MWANA DAR ES SALAAM. Najua kila mtu anatamani kuniona na kujifunza mengi kutoka kwangu.  Sasa fursa ni hii.  NJOO UBUNGO PLAZA, GHOROFA YA PILI, OFFICE NAMBA 202. Nitakuwepo kukufunza juu ya uanzishaji biashara kwa mitaji midogo.  Najua kila mtu anatamani kuwa na biashara yake ila tatizo kubwa limekuwa ni mitaji. Sasa basi, njoo siku ya Ijumaa, Tarehe 24/06/2016 Kuanzia saa 12:00 Mchana mpaka saa 05:00 Jioni. Ili nikupe mbinu hizi adimu kabisa. Njoo, kiingilio ni bure na nitakufundisha bure. Unaruhusiwa pia kuja na mwenzako. By,  Frank A. Ndyanabo - FAN

TANGAZO LA AJIRA

Image
TANGAZO LA AJIRA. NYUMBANI BUSINESS PLAN ENTERPRISES Inakutangazia nafasi ya kazi katika idara ya afisa mauzo kwa watu wote waishio MWANZA. SIFA ZA MUOMBAJI. ••Awe ni muhitimu wa kidato cha nne Au sita. ••Awe na shahada,stashahada au cheti cha Masoko(marketing), Sayansi ya jamii(sociology), usimamizi wa biashara(business administration), fedha (finance), kibenki(banking) KAZI ZA AFISA MAUZO. 1.Kutafuta na kutengeneza masoko mapya ya bidhaa. 2.Kuandaa taarifa ya mauzo kila siku, kwa wiki na mwezi. 3.Kufuatilia na kukusanya mauzo ya kila siku. 4.Kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa msimamizi(supervisor) wake kila siku. MSHAHARA MNONO UTATOLEWA TUMA MAOMBI: Tuma maombi yako kwenda kwa Afisa Utumishi wa Nyumbani Business Plan. Email: nyumbanibusinessplan@gmail.com Kwa Mawasiliano zaidi. • +255 753 183 583 • +255 684 459 947 MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 30/06/2016

ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO.

Image
ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO. SEHEMU YA 2. Karibu katika mwendelezo wa mada yetu iliyotangulia ikiwa na sehemu ya kwanza na leo tuko katika sehemu ya pili. Kila mtu anatamani maisha yake yabadilike kutoka alipo na kusonga mbele zaidi. Ila maisha hubadilika pale tu unapotaka yabadilike. Na ili yaweze kubadilika lazima ukubali kupigika kwa ajili ya kuyafanya yabadilike.  Huwezi kulala na kuamka ukakuta yamebadilika. Kwa leo hebu tujifunze njia zingine : 6. Achana na mahusiano yenye kukuumiza. Watu wengi naweza sema ni ving'ang'anizi kwa mambo yasiyo na tija.  Haimaanishi kuwa, kwakuwa umekuwa na mtu au umekuwa ukifanya jambo fulani kipindi cha nyuma basi ni lazima uwe nae au uendelee na mambo hayo maishani mwako. Kukosa jambo fulani ulilolizoea haimaanishi kuwa lazima ulipate.  Au kumkosa mwenzako aliye kuumiza hapo awali haimaanishi kuwa lazima uwe nae maishani mwako.  Kukikosa kitu cha awali ni nafasi nzuri kwako kupata muda wa kusonga mbele k...

UNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA BINTI GETRUDE CLEMENTI?

Image
UNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA BINTI GETRUDE CLEMENTI? Getrude Clement ni binti kutoka Jijini Mwanza, nchini Tanzania.  Na anasoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Mnarani, ilioko nje kidogo ya mji takribani km 10 au zaidi kutoka mjini. Shule iyo ni ya serikali ni moja kati ya shule za kata zilizoanzishwa kipindi hicho. Getrude ana umri wa miaka 16. Alipata fursa ya kipekee kuongea kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa, akikaribishwa na Mhe. Ban Ki Moon, katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kama muwakilishi wa watoto na vijana wote duniani kwa ajili ya kuzungumzia maswala ya mazingira na uchafuzi wake. Baba yake ni Kinyozi na mama yake ni mfanya biashara mdogo mdogo wa nyanya na vitunguu. Getruda Clement, aliweza kuushangaza ulimwengu jinsi alivyo simama mbele ya viongozi mbali mbali nakuweza kuhutubia bila wasi wasi na kwa kujiamini kupita kiasi.  Ujasiri alio nao binti huyu ndio umenifanya niandike maneno haya ili uweze kujifunza kitu fulani. Wewe kama mfuatiliaji mzuri wa...

ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO.

Image
ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO. SEHEMU YA 1: Kila mtu anatamani maisha yake yabadilike kutoka alipo na kusonga mbele zaidi.  Ila maisha hubadilika pale tu unapotaka yabadilike. Na ili yaweze kubadilika lazima ukubali kupigika kwa ajili ya kuyafanya yabadilike.  Huwezi kulala na kuamka ukakuta yamebadilika. Leo nimeamua kukuletea njia zitakazo fanya maisha yako yabadilike kikamilifu endapo utayazingatia.  Siku zote ndoto yangu mimi Frank A. Ndyanabo - FAN ni kuona kila ninacho kifanya kinaleta matunda chanya kwa watu hasa wewe unayesoma na kufuatilia makala zangu hapa kila siku.  Ila ndoto hii na furaha yangu haiwezi kukamilika kama hautawashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako ili na wao wapate ujumbe huu. Sasa hebu njoo tutembee pamoja tujifunze mambo haya. 1. Ondoa mambo mabaya maishani mwako. Ukiona kitu fulani hakikuongezei thamani au hakina manufaa maishani mwako huna budi kukiacha.  Huwezi kupata maisha mapya bila kukubali kuachana na ...

MATENDO NI TIBA YA WOGA.

Image
MATENDO NI TIBA YA WOGA. Hii ndio dawa pekee ya kutibu ugonjwa wa woga ndani yako.  Pindi tunapotaka kufanya jambo fulani utakuta tunakabiliwa na woga. Woga ni kitu kibaya sana katika maisha yetu ya kila siku. Jiulize ni mambo gani umeshindwa kuyafanya kwa sababu ya woga. Siku zote ukitaka kushinda jambo kwanza ondoa woga ndani yako.  Na ili kufanikisha jambo lako jiulize ni kitu gani ufanye ili kukabiliana na woga uliopo ndani yako. Jibu utakalolipata litumie kukabiliana na adui huyo woga.  Utakuwa umepata muarobaini wa mafanikio yako. Weka mfumo mpya sasa wa maisha yako, utakaokupa mwanga sahihi katika maisha yako.  Utakuwa umekutana na fursa nyingi katika maisha yako ila woga umekufunika na kuiteka akili yako.  Sasa ni wakati wa kukataa hali hiyo na kuamua kutenda. Nyanyuka tutembee pamoja sasa. By: Frank A. Ndyanabo - FAN

VYAKULA HIVI VITAKUSAIDIA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANYO NA KUKUA KWA TEZI DUME.

Image
VYAKULA HIVI VITAKUSAIDIA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME. Kichocheo cha testosterone au kwa Kiswahili , japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme, pia kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone upungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA, KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzi...